Wito: Mdahalo uitishwe baina ya Lissu na viongozi wa CCM kuhusu hoja ya 'ubaguzi wa kimuungano'

Kama sio kumuogopa Lissu aletwe Samia mwenyewe...utasikia "hili nalo mkalitazame"
 
Kumetokea patashika ya kisiasa tangu Tundu Lissu aushambulie muungano wa Tanzania kwenye kona ya kumgusa Rais Samia Suluhu kama mzanzibar katika kuamua (kikatiba) mambo mahususi ya watanganyika yenye kuathiri mustakabali wa maisha ya watanganyika moja kwa moja.

Lissu ametoa hoja zake akijificha kwenye kivuli cha katiba ya Tanzania (yenye kumpa mamlaka Rais Samia kuamua mustakabali wa watanganyika) na katiba ya Zanzibar (yenye kumtambua rais Samia kama raia kamili wa nchi ya zanzibar, na hapo hapo kutomtambua mtanganyika mwingine yoyote kwenye maslahi ya Zanzibar). Viongozi wa CCM wao wamejificha katika kivuli cha uzito wa maneno aliyotumia Lissu kuwa yana taswira ya kibaguzi na yenye kuchochea chuki dhidi ya rais halali wa Tanzania mwenye asili ya uzanzibar.

Kwa kuwa hoja inagusa muungano wetu, katiba yetu na umoja wa taifa letu, wadau mbalimbali wameomba kuitishwe mdahalo wa kisiasa wenye lengo la kumleta Lissu na kiongozi wa juu wa CCM katika kupambana kwa hoja ili watanzania tujifunze na kupima hoja zao.
Tunataka mjadala wa hoja
 
Huu Muungano toka nipo darasa la tano sijui kuna maswali nilihitaji ufafanuzi kwa mwalimu wangu ndugu Sijaona ila na yeye alizunguka zunguka tu mwisho nikaonekana sio mwelewa ila hayo maswala ndio pasua kichwa mpaka leo.
 
Kumetokea patashika ya kisiasa tangu Tundu Lissu aushambulie muungano wa Tanzania kwenye kona ya kumgusa Rais Samia Suluhu kama mzanzibar katika kuamua (kikatiba) mambo mahususi ya watanganyika yenye kuathiri mustakabali wa maisha ya watanganyika moja kwa moja.

Lissu ametoa hoja zake akijificha kwenye kivuli cha katiba ya Tanzania (yenye kumpa mamlaka Rais Samia kuamua mustakabali wa watanganyika) na katiba ya Zanzibar (yenye kumtambua rais Samia kama raia kamili wa nchi ya zanzibar, na hapo hapo kutomtambua mtanganyika mwingine yoyote kwenye maslahi ya Zanzibar). Viongozi wa CCM wao wamejificha katika kivuli cha uzito wa maneno aliyotumia Lissu kuwa yana taswira ya kibaguzi na yenye kuchochea chuki dhidi ya rais halali wa Tanzania mwenye asili ya uzanzibar.

Kwa kuwa hoja inagusa muungano wetu, katiba yetu na umoja wa taifa letu, wadau mbalimbali wameomba kuitishwe mdahalo wa kisiasa wenye lengo la kumleta Lissu na kiongozi wa juu wa CCM katika kupambana kwa hoja ili watanzania tujifunze na kupima hoja zao.
Kwa hiyo hoja ni muungano tu. Tayari Lissu anafaa kuwa, Rais. Hakuna hoja nyingine?
 
Back
Top Bottom