Uchaguzi 2020 Wito: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake yote wajiuzulu

They are there like figureheads
 
RAIS TUNDU LISSU ATUPE TU GREEN LIGHT TUINGIE MTAANI TUMECHOKA NASEMA TUMECHOKA. SIOGOPI KUFA KWA AJILI YA TAIFA LANGU DHIDI YA MKOLONI MWEUSI NIMESEMA TUMECHOKA NASEMA BAAS MAAMAE.

Hahaha skia hii mbuzi ingine uku
 
Hadi hapa huu uchaguzi ni invalid, tunarudia, hatukubali matokeo yoyote yale, kura zimekamatwa kibao je ambazo zishapitishwa ni ngapi? na majimbo mangapi?
Huu uchaguzi tushau-cancel tunarudia mwingine tukiwa na tume huru sio hii ya sasa hivi.

Naona una usingizi,
 

Ebu lala kwanza
 
Viongozi ni watu wenye vision, nadhani viongozi wa upinzani wanazingua.
Cha msingi viongozi ingizeni watu road kuanzia kesho
 
Ngojeni dawa iwaingie vizuri naona mnaanza kuwashwawashwa. Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Mkuu kujiuzulu kwao (japo ni jambo lisilowezekana kabisa) sidhani kama kutarejesha haki zinazochezewa na wapuuzi wachache.
 
Reactions: BAK
Baada ya uchaguzi huu hawa watendaji wa tume waanze kushikishwa adabu mmoja mmoja kimya kimya
Yaani unahamasisha wauwawe. Je, unajuwa ni jinai kuunda mbinu au kuhamasisha murder/assassination?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] BAVICHA tuliwambia piganieni Tume huru ya uchaguzi toka 2015, nyie mkaishia kujadili kingereza cha Magu
 
Kila uchaguzi mambo yaleyale yanajirudia kila upande(state na opposition)hawachukui hatua.

Hapa wakulaumiwa ni wote, sio tume ya uchaguzi tu
Sio kweli, mwaka huu hayajajirudia nafikiri mwaka huu ni hovyo kuliko miaka yote!
 
Tukiwaambia msusie chaguzi, hamsikii.

Sasa mnalialia nini? Kwani hamkujua zitakuwepo figisu?
Kususia Uchaguzi haiwezi kuwatisha CCM hata kidogo.

Wamesajili vyama vingi bandia vya upinzani kama mbadala endapo CHADEMA wataleta mambo ya kususa na kukacha.

CHADEMA ndio tegemeo pekee la wananchi kwa sasa.

Ni juu ya wananchi wenyewe kupambana na hawa maharamia wa kijani, la sivyo CHADEMA itakufa na ndio utakuwa mwisho wa demokrasia nchini. Tutabaki na maigizo ya hawa makachero uchwara wenye wafuasi watano.

Bila wananchi kuamka na kuchukua mamlaka yao, naona giza kubwa sana mbele. CCM itatawala miaka mia hamsini ijayo.
 
Hawana akili kabisa hao.
Mkuu kwa hili hapana. Sikubaliani na wewe.

Mchakato wa kupata tume huru hauwezi kufanywa na chadema pekee. Haiwezekani.

Mfumo wa sheria ya kubadili na kutengeneza Katiba, unampa Rais mamlaka yote ya kuamua Katiba mpya itungwe ama isitungwe.

Tume ya uchaguzi ni Taasisi iliyoundwa na Katiba. Kutaka kuibadili mfumo wake, lazima mchakato wa kubadili Katiba au kutunga Katiba mpya ufanywe.

Rais akisema hakuna katiba mpya, hakutakuwa na katiba mpya hata mfanye nini.

Na hata wakijaribu kufanya mabadiliko ya Katiba kupitia bunge, bado akidi yao ni ndogo hawatoshi.

Narudia tena, nchi hii bila WANANCHI WENYEWE kuamka na kupambana na hawa maharamia, ccm haiwezi kutoka madarakani abadani.

Hapa tutawaonea chadema bure. Wanaostahili lawama ni hawa maharamia wanaoharibu nchi na kutawala kidhalimu kinyume na matakwa ya wananchi.
 
Harakati za kudai katiba mpya na tume huru si za CHADEMA peke yake.

Hilo kwangu halina ubishi.

Ni wajibu wa kila mpenda demokrasia kudai hivyo vitu.

Bado naamini kwamba kwa kuendelea kushiriki chaguzi zao [yes, hizi chaguzi ni za kwao CCM], kunawapa CCM uhalali ambao hawaustahili.

Ingekuwa ni juu yangu, ningesusia kabisa kushiriki hizo chaguzi mpaka kuwepo na mazingira ya kueleweka na yanayotoa fursa sawa kwa washiriki wa mchakato wote.

Siwezi kushiriki shughuli iliyo na ushindani ambayo mahindani wangu ndo anaweka mwamuzi, timekeeper, kamisaa, mashabiki, na kila kitu kingine kinachompa yeye advantage dhidi yangu.

Never.
 
Hii ndio justification yako ya wizi wa kura mlioufanya leo?!

Umeandika maelezo mengi ambayo hayaendani kabisa na mada iliyopo mezani, unajaribu kujiliwaza kwa kuficha uozo mnaoufanya sasa chini ya kapeti!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…