Wito: Rais Samia Toa Maelekezo ya Kumfukuza Anayetajwa Mwalimu na Mhamasishaji wa Ugaidi, Ili Kuokoa Tanzania ya Kesho

Kila jambo baya lilikuwa na mwanzo mdogo, lakini wahusika hawakuushughulikia mwanzo, na baadaye wakaangamia au wakalazimika kutumia gharama kubwa kuokoa Taifa au jamii yao.

Tanzania hii ya leo, pamoja na matatizo mengi tuliyo nayo, umoja wetu usiozingatia dini, kabila au eneo mtu atokalo ni jasho na jitihada nyingi za muasisi wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere (Mwenyezi Mungu Umjalie Pumziko Jema la Milele).

Baada ya jitihada hizi za watangulizi wako, Rais Samia usikubali kuingia kwenye historia mbaya kuwa wewe ulikuwa mtawala wa kwanza kuruhusu mambo yanayopalilia chuki na ugaidi wa kidini.

Kuna mtu ameingia nchini, mtu huyu ni mhalifu, nchini kwake India amepigwa marufuku kuonekana na anatafutwa kwa kuhamasisha ugaidi. Mataifa mengi Duniani, yamempiga marufuku kuonekana katika mataifa yao kutokana na mafundisho yake hatari kwa usalama wa Dunia.

Mtu huyu anayedaiwa kuendesha midahalo ya kidini ni mtu ambaye amesikika mara kadhaa katika mihadhara yake akitamka kuwa waislam wote wanatakiwa kuwa magaidi dhidi ya wale aliowaita ni maadui wa uislam.

Hivi kweli waislam wa Tanzania wamekosa watu wa kuwafundisha watu kuhusiana na imani yao mpaka aletwe mtu ambaye anatafutwa kwa uhalifu na mafunfisho ya uovu?

Rais ingilia kati, usiruhusu watu wahalifu kuja kupandiza mbegu za chuki na ugaidi nchini mwetu. Kinachopandwa leo na watu waovu kama huyo mhubiri, matunda yake yatakuwa kuvisumbua vizazi vyetu vya baadaye.

Dini haifanyiwi mdahalo wala mashindano, dini hufundishwa na kuhubiriwa.

Samia, wewe ni muislam, na huyu mhubiri mhalifu anayetafutwa, ni muislam, ukiruhusu haya mambo ya kidini yanayokiuka misingi ya utengamano wa Taifa letu, inaweza kuleta tafsiri mbaya kwa watu wengine. Usikubali hilo litokee, litakuathiri sana wewe binafsi na Taifa letu.

Mshikamano wetu, umpja wetu, vinatakiwa kulindwa kwa nguvu zote.
Kelele za kijinga, je km amemwalika..huo ujumbe wako unaleta maana?
 
Mbona mnateseka kiasi hiki kila siku kulalama ? Kwa Nini Magalatia mmekuwa hovyo kiasi hiki wakati mnadai kulalamika sana ni inferiority complex.

Poor Galatians..
 
Ifike Hatua hata kama Viongozi wa Interest Binafsi Wakatae Mpasuko ndani ya Taifa kwa sababu hata wao pia Wanaweza kupoteza Walivyopambania katika muda wao wote wa maisha na kazi
 
Hakutakuwa na athari za kidiplomasia afukuzwe tu huyo mhamasishaji huyo wa mambo ya hovyo
 
Eti mdahalo unaongelea Jesus vs Muhammad!! Anyway, ngoja tusuburi tuone lengo kuu hasa ni lipi!.
 
Naamini kabisa kama huyu bwana mafundisho yake yangekuwa asilimia mia moja ni ugaidi basi serikali isingemruhusu kuja hapa,kwakuwa kabla ya kuja kwake lazima kwanza aombewe kibali

Huyu ni mwanazuoni wa kiislamu ambaye ana mahubiri mengi mazuri sana tu,na anasilimisha wasio waislamu wengi sana kwa mafundisho yake,huenda kwa wasio waislamu wanamuogopa kwakuwa mafundisho yake yanatoa mwanga kuhusu imani na kumuamini mungu mmoja

Huyu mahubiri yake nimeyashuhudia kupitia PEACE TV ,ni mlinganiaji mzuri sana wa dini na mhubiri mzuri pia

Sasa ni rahisi sana watu kumuamini mtoa mada kwakuwa huwa tunapenda kupokea mambo kibubusa tu bila kufanya utafiti,na hii ndio hulka ya watu wavivu,hawana mda wa kutafiti ukweli wa mambo

Kwahiyo tusiwe wepesi wa kupokea habar na kuiamini moja kwa moja,binafsi nasema mtoa mada anaandika kwa chuki zake binafsi na sio hali halisi ilivyo
 
Wahubiri wa Kimataifa wa Dini ya Kikristo wanapokuja TZ wanahubiri Injiri ya Yesu Kristo tu.
Hawataji Dini nyingine wala kusoma vitabu vyao.

Huyo Naik akihuburi ni lazima autaje Ukristo kwa kuukebehi na kuupinga huku akinukuu na kuisoma Biblia.

Kampeni yake kuu ni kuudhohofisha Ukristo na kuueneza Uislamu.

Tatizo lake ananukuu nukuu Aya za Biblia na kuzitafsiri kiislamu islamu, hivyo kupotosha ukweli wa Ukristo makusudi.

Ngoja aje muone anavyo ropoka ropoka hovyo kuhusu mafundisho ya Biblia.

Kwake Qurani na Uislamu haumtoshi kabisa.
Cha ajabu haitaji kabisa Dini yake ya Asili UHINDU wala kusoma Kitabu cha hiyo Dini.
Wala hagusi kabisa Dini ya Majirani zake Ubudha na Ushinto.

Salman Rushdie kamwalika mala kibao ili ajadiliane naye maswala ya dini yake ya Kiislamu anamkimbia hadi hii leo.
Hadi nashangaa ni kwanini anagoma kujadiliana na msomi mwenzake wa dini ya Kiislamu aliye andika kuhusu "Uislamu ni Ushetani"

Ameshindwa kabisa kuutetea Uislamu dhidi ya shutuma za Rushdie.
Badala yake anatafuta watu wasio na elimu ya dini ya kutosha na kuwaongopea ongopea.
 
Kila jambo baya lilikuwa na mwanzo mdogo, lakini wahusika hawakuushughulikia mwanzo, na baadaye wakaangamia au wakalazimika kutumia gharama kubwa kuokoa Taifa au jamii yao.

Tanzania hii ya leo, pamoja na matatizo mengi tuliyo nayo, umoja wetu usiozingatia dini, kabila au eneo mtu atokalo ni jasho na jitihada nyingi za muasisi wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere (Mwenyezi Mungu Umjalie Pumziko Jema la Milele).

Baada ya jitihada hizi za watangulizi wako, Rais Samia usikubali kuingia kwenye historia mbaya kuwa wewe ulikuwa mtawala wa kwanza kuruhusu mambo yanayopalilia chuki na ugaidi wa kidini.

Kuna mtu ameingia nchini, mtu huyu ni mhalifu, nchini kwake India amepigwa marufuku kuonekana na anatafutwa kwa kuhamasisha ugaidi. Mataifa mengi Duniani, yamempiga marufuku kuonekana katika mataifa yao kutokana na mafundisho yake hatari kwa usalama wa Dunia.

Mtu huyu anayedaiwa kuendesha midahalo ya kidini ni mtu ambaye amesikika mara kadhaa katika mihadhara yake akitamka kuwa waislam wote wanatakiwa kuwa magaidi dhidi ya wale aliowaita ni maadui wa uislam.

Hivi kweli waislam wa Tanzania wamekosa watu wa kuwafundisha watu kuhusiana na imani yao mpaka aletwe mtu ambaye anatafutwa kwa uhalifu na mafunfisho ya uovu?

Rais ingilia kati, usiruhusu watu wahalifu kuja kupandiza mbegu za chuki na ugaidi nchini mwetu. Kinachopandwa leo na watu waovu kama huyo mhubiri, matunda yake yatakuwa kuvisumbua vizazi vyetu vya baadaye.

Dini haifanyiwi mdahalo wala mashindano, dini hufundishwa na kuhubiriwa.

Samia, wewe ni muislam, na huyu mhubiri mhalifu anayetafutwa, ni muislam, ukiruhusu haya mambo ya kidini yanayokiuka misingi ya utengamano wa Taifa letu, inaweza kuleta tafsiri mbaya kwa watu wengine. Usikubali hilo litokee, litakuathiri sana wewe binafsi na Taifa letu.

Mshikamano wetu, umpja wetu, vinatakiwa kulindwa kwa nguvu zote.
Ww hiyo chuki dhidi ya waisilam iliyo kujaa mpaka matakoni umefundishwa na nani?
 
Kasemaje?mumjibu kwa hoja sio kusema afukuzwe Tanzania watu hawajahi kuuwana sababu ya dini!
Wamjibu kwa hoja Waislamu wenzake.

Mkristo ana haja gani kumuuliza Naik kuhusu Dini ya Kiislamu au ya Kikristo ?
Yeye ni Askofu au Mchungani?

Majibu ya Naik ni kwa mujibu wa Dini ya Kiislamu na Qurani anataka Wakristo wamwulize maswali kwa lengo lipi ?

Yaani Wakristo wafundishwe maswala ya Dini yao na Mwislamu?
Kwani yeye Naik anaukubali Ukristo?
Na kama sio Mkristo, anawataja Wakristo kwa muktadha gani ?
 
Nilipoona tangazo lao nikajua huenda mh raisi hayajui haya au kidogo amevutwa na udini ikizingatiwa anayekuja ni wa dini yake. Tangazo lipo wazi sana ati YESU NA MUHAMAD.
Yesu wa Biblia alikufa na kufufuka. Issa bin Maryam wa kitabu chako hakufa.

Sasa hapo hata kama mimi ningekuwa mwenye mamlaka Je, ningeruhusu upuuzi huu? Jibu ni hapana.

Je, wanakuja kuzungumzia Yesu wa kitabu kipi. Je, kwanini wasizungumzie dini yao pekee?
 
Wamjibu kwa hoja Waislamu wenzake.

Mkristo ana haja gani kumuuliza Naik kuhusu Dini ya Kiislamu au ya Kikristo ?
Yeye ni Askofu au Mchungani?

Majibu ya Naik ni kwa mujibu wa Dini ya Kiislamu na Qurani anataka Wakristo wamwulize maswali kwa lengo lipi ?

Yaani Wakristo wafundishwe maswala ya Dini yao na Mwislamu.
Kwani yeye Naik anaukubali Ukristo?
Na kama sio Mkristo, anawataja Wakristo kwa muktadha gani ?
Kuutaja ukristo tatizo liko wapi kama huna cha kumuuliza kaa kimya akikosa maswali ya kuulizwa atakwenda zake!
 
Naamini kabisa kama huyu bwana mafundisho yake yangekuwa asilimia mia moja ni ugaidi basi serikali isingemruhusu kuja hapa,kwakuwa kabla ya kuja kwake lazima kwanza aombewe kibali

Huyu ni mwanazuoni wa kiislamu ambaye ana mahubiri mengi mazuri sana tu,na anasilimisha wasio waislamu wengi sana kwa mafundisho yake,huenda kwa wasio waislamu wanamuogopa kwakuwa mafundisho yake yanatoa mwanga kuhusu imani na kumuamini mungu mmoja

Huyu mahubiri yake nimeyashuhudia kupitia PEACE TV ,ni mlinganiaji mzuri sana wa dini na mhubiri mzuri pia

Sasa ni rahisi sana watu kumuamini mtoa mada kwakuwa huwa tunapenda kupokea mambo kibubusa tu bila kufanya utafiti,na hii ndio hulka ya watu wavivu,hawana mda wa kutafiti ukweli wa mambo

Kwahiyo tusiwe wepesi wa kupokea habar na kuiamini moja kwa moja,binafsi nasema mtoa mada anaandika kwa chuki zake binafsi na sio hali halisi ilivyo
Weka mihemko pembeni. Toa maoni yako kwa utashi wa hekima.

Unasema kuwa mimi nina chuki binafsi na huyu Nakir, niwe na chuki naye binafsi kwa sababu zipi? Hivi mtu ambaye hujawahi kukutana naye, wala maisha yenu hayagusani popote, unawezaje kuwa na chuki naye binafsi?

Nchini kwake India walikompiga marufuku, na kumfungulia mashtaka ya ugaidi, utakatishaji fedha na mahubiri ya chuki, nao wana chuki naye binafsi?

Huko Bangladesh, Canada, US, Uk na Sri Lanka, alikopigwa marufuku, wote hao wana chuki naye binafsi?

Na wale waliofanya ugaidi, na kisha kukamatwa na kushtakiwa, nakukiri kuwa walikuwa wanatekeleza mafundisho ya huyu Nakir, nao walikuwa na chuki naye binafsi?

Mtu mwerevu na mwenye hekima hujifunza kutokana na makosa yawenzake, hasubirii mpaka yampate yeye mwenyewe, ndiyo ajifunze.
Ni mafundisho ya watu kama haya ndiyo yaliyosababisha ugaidi kule Zanzibar. Walimwua padre, wakachoma makanisa.

Hatumtaki mtu yeyote anayeweza kutuletea ugaidi nchini. Lakini haijawahi kutokea mtu yeyote kuzuiwa kuhubiri imani yake nchini mwetu. Hubiri hicho unachokikua na u achokiamini, lakini usipalilie ugaidi dhidi ya wale wasiokiamini unachokiamini wewe.

Kauli yake huyu gaidi, ya kusema kila muislamu anatakiwa kuwa gaidi, inatosha sana kuwa ni mtu asiyekubalika nchini mwetu
 
Ww hiyo chuki dhidi ya waisilam iliyo kujaa mpaka matakoni umefundishwa na nani?
Hoja ni kwaajili ya watu wenye akili timamu. Wewe haikuhusu.
 
TANGAZO

Fuatilia ratiba hii:

AZAM MEDIA LTD PAMOJA NA THE ISLAMIC FOUNDATION …

UJIO WA DR ZAKIR NAIK TANZANIA - RATIBA YAKE YOTE

View: https://m.youtube.com/watch?v=PLO0zcQm7ok

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA WANAKULETEA MHADHIRI MASHUHURI WA KIMATAIFA , DKT ZAKIR NAIK AKIAMBATANA NA MWANAE SHEIKH FARIQ NAIK KATIKA MDAHALO WA MASWALI NA MAJIBU :

TAREHE 31/12/2024 MSIKITI ZINJIBAR, UNGUJA ZANZIBAR KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA

TAREHE 2/01/2025 DIAMOND JUBILEE DAM KUANZIA SAA 1 USIKU HADI SAA 6 USIKU

TAREHE 5/01/2025 BENJAMIN MKAPA STADIUM UWANJA WA TAIFA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA

MATANGAZO HAYA YATAKUJIA LIVE - MUBASHARA KUPITIA CHANEL YA ZBC2 WEMA UNAOENDELEA

SOURCE : DUA TV Tanzania (Tz)
 
Back
Top Bottom