Waterlemon
Senior Member
- Sep 2, 2016
- 143
- 199
Ndugu wananchi wenzangu,
Napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole kwa yote yaliyotukuta. Mungu awalaze pema vijana wetu waliopoteza maisha kwenye harakati hizi za uchaguzi haramu.
Vile vile napenda kuchukua fursa hiii kuzungumza nanyi kama ndugu, marafiki na kizazi kinachobeba matumaini ya Tanzania. Sisi vijana ndio nguvu za taifa, nguvu za mabadiliko, maendeleo, na matumaini mapya. lakini nguvu hizi inapaswa kutumika kwa hekima, kwa sababu bila amani, nguvu zetu hujaribika kuwa uharibifu na upotovu. Hivyo napenda kuwakumbusha wote umuhimu wa kudumisha amani, umoja, na mshikamano katika taifa letu pendwa la Tanzania. Tumekuwa mfano wa amani barani Afrika kwa miaka mingi, jambo ambalo limechangia maendeleo na ustawi wa watu wetu.
Matukio ya kusikitisha ya baada ya uchaguzi yamesababisha kuleta misuguano ya kijamii na kisiasa katika baadhi ya maeneo. Reference ya matukio hayo ni kwa yale mauaji yaliyotokea kwa visiwani Zanzibar kipindi cha baada ya uchaguzi 2000 na mara nyengine kadhaa na kwa sasa baada ya huu uchaguzi wa karibuni wa 2025. Tunapaswa kukumbuka kuwa tofauti za maoni hazipaswi kuwa chanzo cha chuki au vurugu. Badala yake, tuzitumie kama fursa ya kujenga hoja zenye tija na kutafuta marekebisho kwa njia ya mazungumzo na kuheshimiana.
Amani ni urithi muhimu tulioachiwa na waasisi wa taifa letu, japokuwa muda mwengine nguzo za amani hujaribiwa kutingishwa kwa wachache kwa manufaa ya wachache. Ni wajibu wetu sote kuilinda. Hakuna maendeleo, biashara, wala ustawi vinavyoweza kupatikana bila amani.
Natoa wito kwa viongozi wa dini, vijana, wanawake, wazee, na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa karibu kuhakikisha tunalinda umoja wetu. Tushirikiane katika mijadala ya amani, kuelimisha jamii zetu, na kuepuka lugha za uchochezi mitandaoni, haswa humu kwenye threads za Jamii Forum na pengineko popote mitaani nchini Tanzania.
Tanzania ni yetu sote — iwe ni bara au visiwani. Amani yetu ni jukumu letu. Tuwe wazalendo wa kweli kwa matendo na kwa maneno. Tujiepushe na mwendeleo na mtazamo huu wa kubaguana kwa kiTanganyika na kiZanzibari, maana tukiendelea hivi itafika kuchinjanza wenyewe kwa wenyewe, wakati wanaofaidika kwa mgawanyo huo ni wachache wenye fikra finyu na waliopo madarakani kwa agenda za kjinufaisha wenyewe. Kwa wananchi wenzangu wengi waliobaki, litakalofuata kwao baada ya hilo ni vifo, majuto na hasara.
Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani, umoja na upendo. Wakati mwengine, tunaweza kutofautiana kisiasa, kijamii, au kidini. Lakini tofauti hizi hazipaswi kutugawa. Zikitumika vizuri, zinaweza kuwa chanzo cha ubunifu na maendeleo.
Vijana wenzanu, tusikubali kutumiwa na mtu yeyote kuchochea vurugu na machafuko. Hususan, tusikubali kubaguana kati wa waTanganyika na waZanzibari. Tusisambaze chuki mitandaoni. Badala yake tutumie sauti zetu kupaza wito wa haki, uwajibikaji na upendo. Tuwe mfano wa kizazi kinachotatua matatizo kwa kupigania haki yetu kwa mifumo inayostahiki ya amani kati yetu.
Tupitie njia za mazungumzo kuweka mambo sawa na kupitia njia za amani kudai haki zetu. Tuchukue jukumu la kuwa mabalozi katika mitaa yetu, mitandaoni na popote tulipo. Tuchape kazi kwa ubunifu na kuendelea kupigania haki kwa njia za amani na heshima. Haki ya mtu haipotei, either in this life or hereafter.
“Amani haiji kwa bahati; inajengwa kwa jitihada.”
Kwa pamoja, tuendelee kuijenga Tanzania yenye upendo, usawa, na haki kwa wote.
Nawajibisha...