Wito: Waliomrekodi na kusambaza video ya Mbunge mstaafu Prof Jay akiwa ICU wachukuliwe hatua

Wito: Waliomrekodi na kusambaza video ya Mbunge mstaafu Prof Jay akiwa ICU wachukuliwe hatua

Mi nasemaje, huyu kesho mapema inabidi afungiwe hiyo app yake, na ikiwezekana ukikutwa nayo kwenye simu iwe ni kosa kama la uhujumu uchumi..., tumevumilia tumechoka sasa, njaa zake zinamuondolea utu..!!
Ubaya ile app iko kama open sourced. Inapokea taarifa from individuals kwahio kuna option ya kumuuzia habari yeye mule ndani! It seems kuna mtu kamuuzia hio habari
 
Uyo dada kavuka mipaka na kihalisia uyo dada hayupo sawa kichwani Kuna kitu kinamsumbua tena sana atakuwa na uchizi upo kichwani mwake
 
Umejuaje ni madaktari na wauguzi ndio waliohusika?
Hiki kitendo kimefanyika si Cha kiungwana hata kidogo na kimefanywa na watu ambao huwezi kutegemea.

Inadaiwa kuwa madaktari na wauuguzi waliokua ICU wakimhudumia Prof J wamechukua video na kwenda kumuuzia yule dada ili aisambaze mtandaoni. Sio uungwana hata kidogo.

Serikali kupitia hiyo video mnaweza kuwajua waliofanya hivi na nashauri wachukuliwe hatua kali sana. Itumike namna ya kuwabaini waliofanya hivi najua mna mkono mrefu na hamshindwi.

Mtu yupo ICU amelazwa anapigania uhai wake, mnamhudumia kumbe mnarecord. Amewafanyiaa kitu gani kibaya huyu hadi mfikie huko?
 
Duh! Ila hela hizi.
Sasa kama hiyo ya Ruge imemfikiaje Mange. Maana yake ni familia yake aliyokuwa nayo huko South ndio wamemuuzia.
Ndio ni mwanafamilia itakuwa Kaitoa.si unajua unalipwa vijidola?? Watu wamekosa utu kisa pesa
 
Mazingira ya kumuhudumia mgonjwa na mazingira ya kumsalimia mgonjwa yanafanana? Eitherway, Kwahiyo huyo Mange anaruhusiwa kudhalilisha watu kisa aliyerekodi ni ndugu, jamaa au rafiki?

Hujaelewa. Hakuna aliyesema Mange yupo sahihi. Hoja ya Msingi ni why mnarukia kulaumu wauguzi wa Hosp ?

Huyo Ruge nae alirekodiwa na wauguzi wa Hosp ? Think

Siku hizi watu wanarekodi ndugu zao hasa wakiwa kwenye hali hizo kama ukumbusho kwao , wengine hurekodi wake zao wakiwa wanazaa, wengine hurekodi ndugu zao wakiwa wanakufa . Acheni Ujinga kuwa Na assumption bila ya elimu yoyote .

Mazingira Hosp ndio nini ,ndugu wanaingia lundo kumuona mgonjwa... at that time wauguzi wanakuwa hawapo wanawaachia muongee na ndugu yenu

Chance ya kuwa imerekodiwa na ndugu au marafiki wanaoenda kumuona ni asilimia 95% , kama Ruge alivyorekodiwa his last words

Acheni Ujinga
 
Ila kuna haja yule bibi kijana achukuliwe hatua. Hii cyber bullying anayofanya imekithiri sasa.

Kupitia njaa yake ya kutaka pesa za watu za subscription amekosa mipaka ya utu kabisa.

Hakuna alie salama kwake. Kila mtu amekuwa guinea pig wake wa kupatia pesa kwa kumuandika kutokujali ukweli wa habari ama athari ya habari anazoandika, nyingi ya hizo zikiwa ni za kuzusha tu.

TCRA wa ban hiyo app tu kama kianzio.
Mlimtukuza wenyewe!

Wakati anamtukana Magufuli mlikuwa mnashangilia.
 
Binafsi imenisikitisha sana. Ila kupitia haya nafikiri tunaendelea kujifunza. Mtu peace kama Jay hakustahili haya!

Ila tujiandae kisaikolojia maana ziko mbegu zimepandwa, zimemwagiliwa, zimetiwa mbolea na sasa kidogo kidogo zinaanza kuchipuka! Mbaya zaidi zinachipukia hata kwa wasio na hatia.
Mkuu!..

Wakati mange anamtukana Magufuli na viongozi wengi ambao hatuwapendi tukikuwa tunashangilia sana,

Sasa yamegeukia kwetu tunalaumu! Mange kafika pale sababu yetu kumpa jeuri!

Wacha tuvune tulichopanda.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Too much aisee.... kila siku fulani kachafua hali ya hewa!

Naamini watu watachoka tu.
Watanzania wengi hawana shughuli za kufanya zaidi ya kukalia ujinga,yaani hapo watakuwa wamefurahi kuona Ile clip,Mimi Kama Mimi Ile clip imeniumiuza Sana,kwanza mgonjwa Yuko very serious halafu mpumbavu mmoja anachukulia Kama Mambo ya utani..Ila Mange Mungu afanye Jambo Sasa ili atulie.
 
Back
Top Bottom