Wito: Waliomrekodi na kusambaza video ya Mbunge mstaafu Prof Jay akiwa ICU wachukuliwe hatua

Wito: Waliomrekodi na kusambaza video ya Mbunge mstaafu Prof Jay akiwa ICU wachukuliwe hatua

Mimi ningekubali hoja yako hii kama ukiweka kitu kibaya kimoja au tusi ambalo Mange alimtukana Jiwe zaidi ya kumweleza yale ambayo Jiwe hakutaka kuyasikia.
Kwa sababu akili yako ni sawa na ya mange ndio maana hukuona tusi!

Hata kigogo sasa hivi hawatukani chadema bali anawaambia ukweli kama alivyikuwa anafanya kwa jiwe

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli hili la mgonjwa a step too far,anajua Marekani confidentiality ya mgonjwa ni muhimu mtu aki breach anaadhibiwa,anaona Tanzania anaweza kufanya vyovyote na asifanywe lolote
 
Sherehe ya kifo cha Jiwe ilifanywa na watu wengi mpaka makada wa fisiemu. Kwa hilo binafsi sioni tatizo. Labda mengine ya kutukana watu
Liongo likubwa. Inawezekana haupo Tanzania. Kwa ufupi nikudokeze, Mama Samia anachukiwa sana tena sana tena hapendwi mno na makundi yenye ushawishi ya watanzania. Sababu kubwa ni viashiria vya kukandia misingi ya Dkt Magufuli. Mfano kuruhusu mgambo kupora bidhaa za machinga, na kuwarudisha kwenye nafasi wenye madoa ya uadilifu na pia kuonekana wazi wazi kuajiri watu nafasi za serikali kwa misingi ya dini
 
NJIA NZURI YA KUACHA NA MTU YULE NI KUACHA KUFUATILIA YA KWAKE KWENYE PAGE ZA SOCIAL MEDIA NA APP YAKE.
 
Kabla hujapost video ya Jay, ulionywa sana na wadau wako wa Instagram kwamba kupost video ya mgonjwa si Jambo jema, lakini ukakaidi, ukapost.

Alipoku Waziri Mkuu Peter Pinda alisema kama umeonywa na umekaidi, upigwe TU.

Ndivyo ilivyokuwa kwako, umeonywa, umekaidi kichapo kiwe juu yako.

Kama asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, na sis walimwengu wa taifa hili tumechoshwa na tabia zako za hovyo za kushambulia utu wa watu, kuingilia Uhuru wao wa faragha, kuwatukana, kuwadhalilisha na kuwatendea kila ubaya.

MangeKimambi, Mungu hayupo likizo, na amesikia kilio Cha muda mrefu. Machozi ya Watanzania wengi walio umizwa na wewe yamefika kwenye kiti cha enzi.

NI wakati wako sasa kutubu na kuomba msamaha.

Ivumayo haidumu, ngoma ikilia sana mwisho wake NI kupasuka

alipokuwa anatukanwa makifuli mpaka amekufa anashambuliwa mbona hujalalamika makonda anashambuliwa hulalamiki
 
Kwa hiyo na J analipwa kwa kadri ya matendo yake?
J hana matendo yoyote maovu kustahili kulipwa hayo. Kwakuwa ni mwanadamu anaweza kuwa na madhaifu yake lakini hayako kwa public au yahusianayo na kutoa uhai wa mtu ukilinganisha na bwana yule aliyekuwa katili, muuaji na mwenye chuki za wazi kwa yeyote atakayempinga.
 
Mange Kimambi ni mtanzania anayeishi nchini Marekani kwa muda kitambo sasa.

Amejizolea umaarufu kupitia Page yake ya Instagram,kutokana na kutumia muda mwingi kupost mambo ambayo mara nyingi ni mashambulizi binafsi kwa watu mbalimbali nchini mwetu.

Mambo hayo yamekuwa aidha ni yanayohusu Udaku au Umbea wa mitaani au kashfa na matusi kuhusu watu maarufu hususan wasanii na wanasiasa nchini.

Lakini huwa haishii hapo bali huwa anaenda mbali pia kwa kuwashambulia viongozi wakubwa wa kisiasa na kidini nchini mwetu.kwa matusi mazito.
Akiwemo aliyekuwa Rais wa JMT[emoji1241] awamu ya tano,na kipenzi cha wanyonge marehemu JPM. (R.I.P).

Hakuishia hapo tu,bali kuna wakati aliwahi kumtukana hadharani kiongozi mkubwa kabisa wa madhehebu ya dini ya kiislamu nchini Sheikh Mussa Alhad.

Na kisiasa Mange huyu huyu amewahi kushirikiana na baadhi ya wanasiasa wa upinzani nchini kupitia mitandaoni na kuandaa maandamano waliyokusudia yafanyike nchi nzima kuipinga serikali ya JPM.

Ingawa yalishindwa kufikia malengo yao,lakini Mange kimambi aliendelea kuwa mtu wao.
Na wakimchukulia kama shujaa wao.bega kwa bega na Kigogo14

Matukio mengi anayoyapost Mange huwa yanatokea hapa hapa kwetu na kwa watu wetu humu humu nchini,ambao wanakuwa na malengo yao binafsi chini ya Carpet.

Post ya Profesa J akiwa ICU Muhimbili.

Hii imewaibua watanzania wengi kulaani tukio hilo ambalo kimsingi ni la kusikitisha na ni kinyume na haki za binadamu.kwa sababu
Ugonjwa au maradhi ya mtu,hupaswa kubaki kuwa privacy ya mgonjwa na tabibu wake tu.

Si vema kuchukua video ya mgonjwa anayepigania uhai wake ICU na kuitumia ili kujiingizia kipato.

Mange Kimambi amefungua application yake binafsi ambayo iko Appstore na anatoza pesa ili kuipakua na kusoma ujinga wake.

Amekuwa mjanja kwa kutumia Appstore sababu huko Instagram kwa sasa masharti ni magumu hivyo wasingekawia kumfungia.

My Take!

Kinachonishangaza kwa sasa ni jinsi walewale waliokuwa wakimsapoti bega kwa bega Mange kimambi,kutokana na kuwashambulia watu waliowaona kama mahasimu wao wakubwa.

Tena wengine wakihusika kwa kumtumia matukio kutoka huku.

Sasa ndio wamegeuka kuwa mstari wa mbele kulaani video hiyo ambayo imewekwa na Mange kimambi ikimuonyesha Profesa Jay akiwa mahututi ICU, kinyume na maadili ya kitanzania.

Binafsi ningewaomba hao ndugu zetu,badala ya kumlaani Mange Kimambi.
Wasiishie hapo bali watumie nafasi hii kujifunza madhara ya unafiki.

Isiwe ile habari ya mkuki kwa nguruwe.....ila kwa Binadamu Mchungu

Walikuwa wapi wakati Mange akiporomosha matusi tena ya Aibu kwa watanzania wengine wakiwemo viongozi wa kidini na kisiasa.
Mbona kule walishangilia na kumuona shujaa wao?

Watanzania tuacheni Unafiki......
 
J hana matendo yoyote maovu kustahili kulipwa hayo. Kwakuwa ni mwanadamu anaweza kuwa na madhaifu yake lakini hayako kwa public au yahusianayo na kutoa uhai wa mtu ukilinganisha na bwana yule aliyekuwa katili, muuaji na mwenye chuki za wazi kwa yeyote atakayempinga.
Mliua wote?

Mememlea huyo sasa hivi anawavua nguo,kusifia mbio kapitiliza kwao/chizi kapewa rungu.
 
Back
Top Bottom