Baada ya Waziri Mkuu kudaiwa kutoa kauli ambayo ilionekana kutoa kibali kwa wananchi kujichukulia sheria mikononi katika kupambana na mauaji ya Albino KLHN ilitafuta majibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu juu ya masuala mbalimbali yaliyotokana na ripoti hiyo iliyotolewa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 23 January, 2009. Baada ya kupitia majibu hayo Hoja ya Mwanakijiji iliyokataa kauli hizo za Waziri Mkuu kwenye kijarida chetu cha Cheche la jana bado inasimama. Yafuatayo ni masuali tuliyotuma kwa ofisi hiyo na majibu yake yaliyotumwa kwetu na Bw. Said Nguba, ambaye ni Mwandishi wa Waziri Mkuu aliyekuwa katika msafara huo.
Maswali yetu kwa Ofisi hiyo ya Waziri Mkuu kuhusu kauli hizo (soma eneo la Forum kupata mwanga zaidi juu ya kauli tunazozingumzia) yalikuwa ni kama ifuatavyo:
a. Ni kweli ameagiza "Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore"
b. Ni kweli ametaka UVCCM kushiriki katika kuzuia mauaji ya albino presumably katika kutekeleza hilo la (a)?
c. Kwa kuagiza UVCCM na kusema wanalo "jeshi" ina maana anakiri kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kazi?
d. Kwanini serikali isitoe dau nono kwa waganga/watu wote watakaofanikisha kukamatwa kwa wauaji na wale watafutao viungo vya Albino. Kama kinachotafutwa ni utajiri wa "haraka haraka" kwanini serikali isiamue kutajirisha watu kwa kulazimisha wasalitiane kama walivyofanya kule Iraq, hata Saddam na watoto wake wakasalitiwa?
e. Je uamuzi wa serikali kufuta leseni za waganga wote wa kienyeji siyo sawa na adhabu ya jumla (collective punishment) kwa kosa la watu wachache? Kwanini mtu ambaye hajakosea au kuthibitishwa kwenye vyombo vya sheria anaadhibiwa kwa kosa ambalo anadhaniwa anaweza kufanya? Je huu si uonevu?
NB:.1. Je tunaweza kupata nakala isiyohaririwa au kukatwa ya hotuba yake hiyo ili wananchi wawe mahakimu wa kile WM alisema?
2. Tunaombwa kuweka kwenye mailing list ya press releases za Waziri Mkuu
3. Ikiwezekana naomba unipangie kuwa na mahojiano na Waziri Mkuu kuhusu masuala haya na mengine, mahojiano ambayo pia yatarushwa "live" na kuchapwa kwenye mojwapo ya magazeti nyumbani.
Yafuatayo hapa ni majibu ya Ofisi ya Waziri Mkuu:
Nikiwa Mwandishi wa Waziri Mkuu na niliyehudhuria mikutano hiyo najibu kama ifuatavyo.
a) Alichosema Waziri Mkuu ni kwamba imefika wakati sasa mauaji haya yamechochea hasira ya wananchi wa kawaida kuwa wakimuona muuaji "red-handed" anamchinja Albino na kuchukua kiungo chake, hawawezi kumuacha muuaji huyo. Naye watamshughulikia tu na hawatasubiri kumpeleka polisi.
Watu wanaweza kuwa na tafsiri mbalimbali kuhusu maelezo hayo. Waziri Mkuu ni mwanasheria na kiongozi, siyo mtu "blood-thirsty" kama baadhi ya watu wanavyojaribu kutaka kumuonyesha.
b) Alitoa mwito kwa CCM (na hasa Umoja wa Vijana wa CCM, kwa vile wako "organized") pamoja na vyama vingine vya siasa kutokaa kimya kwa uovu huu wa kuwaua Albino nchini, kwa imani za kishirikina.
c) Kwa kuwataja UVCCM katika kushiriki kuzuia mauaji ya Albino siyo kuwa Waziri Mkuu anakiri kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kazi, bali UVCCM na wengine wote, pamoja na walinzi wa jadi, Sungusungu, watashirikiana na Polisi, chini ya utaratibu a Polisi wa "ulinzi shirikishi" unaohutaji ushirikiano wa Polisi na umma. Mapambano haya ni yetu sote.
d) Hayo ya "kwa nini serikali isitoe dau nono kwa waganga/watu wote watakaofanikisha kukamatwa kwa wauaji na wale watafutao viungo vya Albino", ni ushauri wako na mimi binafsi sina majibu nao.
e) Kufuta leseni za waganga wa jadi. Leseni walipewa na Serikali na hivyo Serikali imeamua kuzifuta zote sasa hivi baada ya kubainika kuwa waganga wa jadi wanapiga ramli na kuelekeza mauaji ya Albino au Vikongwe. Leseni zinafutwa ili kujipanga upya kwamba mganga wa jadi ambaye ana mitishamba itakayothibitishwa, kwa utaalamu wa kisasa, kuwa inatibu ugonjwa fulani basi wa mganga wa aina hiyo anayetumia tiba asilia, baada ya uthibitisho huo ataendelea na kazi yake.
Ipo Sheria ya mwaka 2002 ijulikanayo kuwa ni "Tiba Asilia na Tiba Mbadala" (Traditional and Alternative Medicine). Isitoshe karne hii nayo siyo ya kushabikia ramli kwamba mtoto ameshikwa na malaria iliyopanda kichwani, unakwenda kwa mganga wa jadi anayepiga ramli kwamba sababu ya ugonjwa wa mwanao huyo ni "Mzee mwenye macho myekundu pale jirani ambaye amekukalia vibaya". Kwa vile kuna hili tatizo lililozuka la mauaji ya Albino yanayolitia aibu taifa na kuwafanya watu wahoji amani Tanzania iko wapi wakati Albino wanauliwa ovyo, inabidi kwanza kuchukua hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na janga hilo ili baadaye kujipanga upya!
Said Nguba
Program Note: Mahojiano yetu na Dr. Harrison Mwakyembe yaliyofanyika Jumapili yako hewani kwenye tovuti hii na pia kupitia tovuti yetu tanzu ya
KLH News
Meanwhile:
Hii ni sehemu ya habari iliyoandikwa na Citizen leo kuhusiana na kauli ya Pinda, bado ameng'ang'ania alichokisema
PM: Yes, killers of albinos should die
By Mkinga Mkinga
People caught red-handed killing albinos should also be killed on the spot, Prime Minister Mizengo Pinda has reiterated.
Mr Pinda told The Citizen on Monday that people who were condemning his remarks did not have an idea of the senseless brutality being wrought upon albinos by killers who were after their body parts.
He said his remarks were in line with the urgency and seriousness with which the Government treated the wave of albino killings in some parts of the country, and reflected its commitment to putting an end to the atrocities once and for all.
Mr Pinda added that his statement would not
have shocked anybody who knew the extent of suffering the killings had caused.
"It may be an unusual statement by a prime minister, and I wish to confirm that I made the remarks to send a clear message to albino killers? they should know that if they are caught, they will have to face the fate they had hoped their victims would suffer," he said in an exclusive interview with The Citizen.
Mr Pinda said he and the Government would no longer tolerate the senseless and brutal killings of human beings just because they happen to be of a different colour.
The Citizen had sought clarification from the prime minister after he was quoted as directing members of the ruling CCM's youth wing to kill people caught in the act of killing albinos. The remarks drew sharp criticism from human rights activists, legal experts and the opposition leaders.
The opposition NCCR-Mageuzi said in a news conference on Sunday that Mr Pinda's remarks were ?irresponsible and totally unacceptable?, and asked President Jakaya Kikwete to immediately sack him.
The party's secretary-general, Mr Samuel Ruhuza, said the remarks made a mockery of the principles of the rule of law and encouraged mob justice.
But Mr Pinda brushed aside the criticisms, saying the Government had decided to take the bull by the horns in its war against albino killers.
"A person who knows that he will be killed when caught in the act of killing an albino will think twice before embarking on such an evil mission," he said. Mr Pinda said his statement was not meant to encourage people to take the law into their own hands, but to show that the Government was serious on the issue.
Mr Pinda also said he had directed regional police to place special emphasis on the security of albinos in their areas of jurisdiction.
More than 40 albinos have been killed and mutilated in the past year.
The killers take various body parts which witchdoctors use to make concoctions supposed to make their clients rich.
Last week, Mr Pinda announced the revocation of all licences issued to traditional healers across the country.
Habari ndiyo hiyo.