Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda

Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda

Kwa wanaomjua Pinda vizuri na hata wale wanafuatilia michango yake bungeni sidhani kama wanaweza kusimama kidedea kutetea kuwa hakusema maneno hayo. Huyu Mheshimiwa ana sifa ya kusema anachokifikiri bila kumung'unya maneno. Wakati mwengine inasaidia sana kuwa na kiongozi kama huyo lakini wakati mwengine ni hatari. Huu ndio mfano wake...

Nadhani itakuwa busara kwa Pinda kutoa ufafanuzi wa hili na pia kuonyesha uungwana wake kwa kukubali kuwa alikosea.

Tanzanianjema
 
Kama haya ndio yamo kwenye taaluma ya uandishi wa habari, na kama ndugu wewe ni mwandishi wa habari basi umeconfess kuwa press ya Tanzania ni crummy, na shoddy.

Yaani hapa na wewe umeponda huo uandishi vile vile, umegongelea msumari wa moto kwenye kidonda. Hivyo usiseme unatetea. Waeleze ukweli hao waandishi wajue wapi wanateleza, wajifunze na kujirekebisha.

Sijui kama umeelewa mantiki au umeng'ata maneno. Kuelewa mantiki ni hivi: ngoja nitumie mfano. Nikionyesha kwa kidole kuwa 'mwezi ule...' haina maana kuwa mwezi upo kwenye kidole bali ina maana kwamba ukiangalia kwa kufutisha kidole ninachokionyesha eventually utaona mwezi ulipo. Kung'ata maneno ina maana kwamba nikionyesha 'mwezi ule...' utaona kabisa mwezi uko kwenye kidole. Sasa wewe umelewa lipi?

Kwa hiyo, hata uandishi wa habari ni hivyo. Ni taaluma 'technical' na haitoshi tu kuona 'reporting' fulani na hapo ukaanza ku'judge' bila kujua mazingira yalikuwaje. Ndiyo maana nashauri tuwe tunajiuliza maswali (kujihoji) hata kabla ya kujenga hoja na hasa tujifunze uandishi wa habari ulivyo.
 
Uwiano Maalum, ngoja niseme hivi: uandishi wa habari ni kama taaluma nyingine - kuna mazuri na mabaya. Mazuri ni pale waandishi wanapofuata taaluma yao vizuri. Mabaya ni pale uhuru wao unapoingiliwa na wakubwa au wenye vyombo vya habari. Ila kwa ujumla waandishi wa habari walio wengi wanajitahidi kufanya kazi yao kwa uaminifu na siyo jinsi watu wanavyofikiria.
 
Sijui kama umeelewa mantiki au umeng'ata maneno. Kuelewa mantiki ni hivi: ngoja nitumie mfano. Nikionyesha kwa kidole kuwa 'mwezi ule...' haina maana kuwa mwezi upo kwenye kidole bali ina maana kwamba ukiangalia kwa kufutisha kidole ninachokionyesha eventually utaona mwezi ulipo. Kung'ata maneno ina maana kwamba nikionyesha 'mwezi ule...' utaona kabisa mwezi uko kwenye kidole. Sasa wewe umelewa lipi?

Kwa hiyo, hata uandishi wa habari ni hivyo. Ni taaluma 'technical' na haitoshi tu kuona 'reporting' fulani na hapo ukaanza ku'judge' bila kujua mazingira yalikuwaje. Ndiyo maana nashauri tuwe tunajiuliza maswali (kujihoji) hata kabla ya kujenga hoja na hasa tujifunze uandishi wa habari ulivyo.

Hapo sijaelewa chochote.

Kwa vyovyote nitakavyong'ata maneno Magobe, fani ya uandishi wewe mwenyewe unakubali indirectly kwamba imeingiliwa (kama ulivyotaja kwenye post yako iliyotangulia. Wengi wa waandishi hawajali ubora wa kazi, zaidi ya kutoa habari (prestige au mshiko).

Waandishi wa habari wa Tanzania wana kiwango cha chini sana sio tu cha kuripoti, bali hata knowledge wa wanachoripoti. Tueleze background ya habari na tupashe ipasanyo.

Kama unaona circumstances zimekunyima kupata actual information at that particular time and place, subiri na endelea kutafuta habari kamili. Sio kudesa one to one mwishowe unajikuta umelishwa kasa.

Ingieni kwenye news outlets kubwa duniani, angalieni wenzenu wanavyohabarisha. Elimu ni bahari, hivyo videgree vya IJMC, SAUT na Times kudesa ili kufaulu mtihani ndio vinavyowaangusha bandugu.
 
Sijui kama umeelewa mantiki au umeng'ata maneno. Kuelewa mantiki ni hivi: ngoja nitumie mfano. Nikionyesha kwa kidole kuwa 'mwezi ule...' haina maana kuwa mwezi upo kwenye kidole bali ina maana kwamba ukiangalia kwa kufutisha kidole ninachokionyesha eventually utaona mwezi ulipo. Kung'ata maneno ina maana kwamba nikionyesha 'mwezi ule...' utaona kabisa mwezi uko kwenye kidole. Sasa wewe umelewa lipi?

Kwa hiyo, hata uandishi wa habari ni hivyo. Ni taaluma 'technical' na haitoshi tu kuona 'reporting' fulani na hapo ukaanza ku'judge' bila kujua mazingira yalikuwaje. Ndiyo maana nashauri tuwe tunajiuliza maswali (kujihoji) hata kabla ya kujenga hoja na hasa tujifunze uandishi wa habari ulivyo.

Hapo sijaelewa chochote.

Kwa vyovyote nitakavyong'ata maneno Magobe, fani ya uandishi wewe mwenyewe unakubali indirectly kwamba imeingiliwa (kama ulivyotaja kwenye post yako iliyotangulia). Wengi wa waandishi hawajali ubora wa kazi, zaidi ya kutoa habari (prestige au mshiko).

Waandishi wa habari wa Tanzania wana kiwango cha chini sana sio tu cha kuripoti, bali hata knowledge wa wanachoripoti. Tueleze background ya habari na tupashe ipasanyo.

Kama unaona circumstances zimekunyima kupata actual information at that particular time and place, subiri na endelea kutafuta habari kamili. Sio kudesa one to one mwishowe unajikuta umelishwa kasa.

Ingieni kwenye news outlets kubwa duniani, angalieni wenzenu wanavyohabarisha. Elimu ni bahari, hivyo videgree vya IJMC, SAUT na Times kudesa ili kufaulu mtihani ndio vinavyowaangusha bandugu.
 
Kwa hiyo, hata uandishi wa habari ni hivyo. Ni taaluma 'technical' na haitoshi tu kuona 'reporting' fulani na hapo ukaanza ku'judge' bila kujua mazingira yalikuwaje. Ndiyo maana nashauri tuwe tunajiuliza maswali (kujihoji) hata kabla ya kujenga hoja na hasa tujifunze uandishi wa habari ulivyo.

Unajua, Magobe, unaposema "bila kujua mazingira yalikuwaje" unakubali kwamba waandishi na kazi zao ni dhaifu, na sababu ni mazingira ya kazi.

Kwa hiyo chochote kile utakachosema kuelezea sababu za udhaifu, iwe mazingira, iwe mshahara mdogo, iwe wanapokea rushwa, iwe wanacheleweshewa mshahara wao, iwe uongozi mbaya, iwe umaskini wa makampuni yao, mwisho wa siku umekubali kwamba waandishi na kazi yao ni dhaifu. Hizo unazoeleza wewe ni sababu za udhaifu. Kwa hiyo unakubaliana na mimi kwamba kazi yao ni dhaifu. Nukta.

hapa ndipo ninaposhangaa; ungekuwa mchambuzi mzuri ungejua kuwa habari iliyokuwa kwenye mwanakijiji.com imetoka Mwananchi na imeandikwa na Victor Kinambile wa Tabora. Tulipoiupload kuna mahali ambapo unaweka jina la mwandishi au gazeti na sehemu nyingine ina default name la m.m. mwanakijiji

Kwa makosa yetu wakati tunaipandisha hatukujaza hiyo sehemu ya kwanza na hivyo inajaza sehemu ya pili. Ni mpaka hapa ninaposoma kwako ndiyo najua kosa lilipotokea na tayari tumesahihisha. Mara nyingi watu wakiona tumesahau kuweka source wanatushtua na hivyo tunasahihisha.

Sasa hiyo habari haikuandikwa na mimi bali na Victor. Natumaini hiyo itasaidia katika uchambuzi wako ujao kwa sababu yawezekana umesoma ukiwa na mawazo "mwandishi ni mwanakijiji" and hence your scathing attacks on Tanzanian journalists which has has become a standard banner for you rightly or wrongly.

Mkuu,

Sasa kumbe unakubali umekosea, na umesema uliposhtuliwa umerekebisha, sasa badala ya kuuchuna unanilaumu mimi kwamba nimefanya "scathing attacks on Tanzanian journalists...rightly or wrongly" wakati uliyoambiwa umekubali yamefanya usahihishe makosa. Sasa kosa langu nini hapo?

Halafu kama nimesema kitu "rightly or wrongly" basi huwezi kunilaumu kwa hilo maana inawezekana nimekisema rightly.
 
Nimepata majibu rasmi ya maswali yangu kwa Waziri Mkuu.. nayafanyia kazi.. yakiwa tayari.. yako exclusive.. Badala ya kulalamika waandishi na mapungufu yao.. I go ahead take steps to find the answers.. unlike our steady critic.
 
Thats the SPIRIT,if we really need to move forward.
Its not enough to do good if you can do better!
 
Baada ya Waziri Mkuu kudaiwa kutoa kauli ambayo ilionekana kutoa kibali kwa wananchi kujichukulia sheria mikononi katika kupambana na mauaji ya Albino KLHN ilitafuta majibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu juu ya masuala mbalimbali yaliyotokana na ripoti hiyo iliyotolewa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 23 January, 2009. Baada ya kupitia majibu hayo Hoja ya Mwanakijiji iliyokataa kauli hizo za Waziri Mkuu kwenye kijarida chetu cha Cheche la jana bado inasimama. Yafuatayo ni masuali tuliyotuma kwa ofisi hiyo na majibu yake yaliyotumwa kwetu na Bw. Said Nguba, ambaye ni Mwandishi wa Waziri Mkuu aliyekuwa katika msafara huo.

Maswali yetu kwa Ofisi hiyo ya Waziri Mkuu kuhusu kauli hizo (soma eneo la Forum kupata mwanga zaidi juu ya kauli tunazozingumzia) yalikuwa ni kama ifuatavyo:

a. Ni kweli ameagiza "Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore"

b. Ni kweli ametaka UVCCM kushiriki katika kuzuia mauaji ya albino presumably katika kutekeleza hilo la (a)?

c. Kwa kuagiza UVCCM na kusema wanalo "jeshi" ina maana anakiri kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kazi?

d. Kwanini serikali isitoe dau nono kwa waganga/watu wote watakaofanikisha kukamatwa kwa wauaji na wale watafutao viungo vya Albino. Kama kinachotafutwa ni utajiri wa "haraka haraka" kwanini serikali isiamue kutajirisha watu kwa kulazimisha wasalitiane kama walivyofanya kule Iraq, hata Saddam na watoto wake wakasalitiwa?

e. Je uamuzi wa serikali kufuta leseni za waganga wote wa kienyeji siyo sawa na adhabu ya jumla (collective punishment) kwa kosa la watu wachache? Kwanini mtu ambaye hajakosea au kuthibitishwa kwenye vyombo vya sheria anaadhibiwa kwa kosa ambalo anadhaniwa anaweza kufanya? Je huu si uonevu?

NB:.1. Je tunaweza kupata nakala isiyohaririwa au kukatwa ya hotuba yake hiyo ili wananchi wawe mahakimu wa kile WM alisema?

2. Tunaombwa kuweka kwenye mailing list ya press releases za Waziri Mkuu

3. Ikiwezekana naomba unipangie kuwa na mahojiano na Waziri Mkuu kuhusu masuala haya na mengine, mahojiano ambayo pia yatarushwa "live" na kuchapwa kwenye mojwapo ya magazeti nyumbani.

Yafuatayo hapa ni majibu ya Ofisi ya Waziri Mkuu:
Nikiwa Mwandishi wa Waziri Mkuu na niliyehudhuria mikutano hiyo najibu kama ifuatavyo.

a) Alichosema Waziri Mkuu ni kwamba imefika wakati sasa mauaji haya yamechochea hasira ya wananchi wa kawaida kuwa wakimuona muuaji "red-handed" anamchinja Albino na kuchukua kiungo chake, hawawezi kumuacha muuaji huyo. Naye watamshughulikia tu na hawatasubiri kumpeleka polisi.

Watu wanaweza kuwa na tafsiri mbalimbali kuhusu maelezo hayo. Waziri Mkuu ni mwanasheria na kiongozi, siyo mtu "blood-thirsty" kama baadhi ya watu wanavyojaribu kutaka kumuonyesha.

b) Alitoa mwito kwa CCM (na hasa Umoja wa Vijana wa CCM, kwa vile wako "organized") pamoja na vyama vingine vya siasa kutokaa kimya kwa uovu huu wa kuwaua Albino nchini, kwa imani za kishirikina.

c) Kwa kuwataja UVCCM katika kushiriki kuzuia mauaji ya Albino siyo kuwa Waziri Mkuu anakiri kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kazi, bali UVCCM na wengine wote, pamoja na walinzi wa jadi, Sungusungu, watashirikiana na Polisi, chini ya utaratibu a Polisi wa "ulinzi shirikishi" unaohutaji ushirikiano wa Polisi na umma. Mapambano haya ni yetu sote.

d) Hayo ya "kwa nini serikali isitoe dau nono kwa waganga/watu wote watakaofanikisha kukamatwa kwa wauaji na wale watafutao viungo vya Albino", ni ushauri wako na mimi binafsi sina majibu nao.

e) Kufuta leseni za waganga wa jadi. Leseni walipewa na Serikali na hivyo Serikali imeamua kuzifuta zote sasa hivi baada ya kubainika kuwa waganga wa jadi wanapiga ramli na kuelekeza mauaji ya Albino au Vikongwe. Leseni zinafutwa ili kujipanga upya kwamba mganga wa jadi ambaye ana mitishamba itakayothibitishwa, kwa utaalamu wa kisasa, kuwa inatibu ugonjwa fulani basi wa mganga wa aina hiyo anayetumia tiba asilia, baada ya uthibitisho huo ataendelea na kazi yake.

Ipo Sheria ya mwaka 2002 ijulikanayo kuwa ni "Tiba Asilia na Tiba Mbadala" (Traditional and Alternative Medicine). Isitoshe karne hii nayo siyo ya kushabikia ramli kwamba mtoto ameshikwa na malaria iliyopanda kichwani, unakwenda kwa mganga wa jadi anayepiga ramli kwamba sababu ya ugonjwa wa mwanao huyo ni "Mzee mwenye macho myekundu pale jirani ambaye amekukalia vibaya". Kwa vile kuna hili tatizo lililozuka la mauaji ya Albino yanayolitia aibu taifa na kuwafanya watu wahoji amani Tanzania iko wapi wakati Albino wanauliwa ovyo, inabidi kwanza kuchukua hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na janga hilo ili baadaye kujipanga upya!

Said Nguba

Program Note: Mahojiano yetu na Dr. Harrison Mwakyembe yaliyofanyika Jumapili yako hewani kwenye tovuti hii na pia kupitia tovuti yetu tanzu ya KLH News

Meanwhile:

Hii ni sehemu ya habari iliyoandikwa na Citizen leo kuhusiana na kauli ya Pinda, bado ameng'ang'ania alichokisema

PM: Yes, killers of albinos should die

By Mkinga Mkinga

People caught red-handed killing albinos should also be killed on the spot, Prime Minister Mizengo Pinda has reiterated.

Mr Pinda told The Citizen on Monday that people who were condemning his remarks did not have an idea of the senseless brutality being wrought upon albinos by killers who were after their body parts.

He said his remarks were in line with the urgency and seriousness with which the Government treated the wave of albino killings in some parts of the country, and reflected its commitment to putting an end to the atrocities once and for all.

Mr Pinda added that his statement would not
have shocked anybody who knew the extent of suffering the killings had caused.

"It may be an unusual statement by a prime minister, and I wish to confirm that I made the remarks to send a clear message to albino killers? they should know that if they are caught, they will have to face the fate they had hoped their victims would suffer," he said in an exclusive interview with The Citizen.

Mr Pinda said he and the Government would no longer tolerate the senseless and brutal killings of human beings just because they happen to be of a different colour.

The Citizen had sought clarification from the prime minister after he was quoted as directing members of the ruling CCM's youth wing to kill people caught in the act of killing albinos. The remarks drew sharp criticism from human rights activists, legal experts and the opposition leaders.

The opposition NCCR-Mageuzi said in a news conference on Sunday that Mr Pinda's remarks were ?irresponsible and totally unacceptable?, and asked President Jakaya Kikwete to immediately sack him.

The party's secretary-general, Mr Samuel Ruhuza, said the remarks made a mockery of the principles of the rule of law and encouraged mob justice.
But Mr Pinda brushed aside the criticisms, saying the Government had decided to take the bull by the horns in its war against albino killers.

"A person who knows that he will be killed when caught in the act of killing an albino will think twice before embarking on such an evil mission," he said. Mr Pinda said his statement was not meant to encourage people to take the law into their own hands, but to show that the Government was serious on the issue.

Mr Pinda also said he had directed regional police to place special emphasis on the security of albinos in their areas of jurisdiction.
More than 40 albinos have been killed and mutilated in the past year.

The killers take various body parts which witchdoctors use to make concoctions supposed to make their clients rich.
Last week, Mr Pinda announced the revocation of all licences issued to traditional healers across the country.

Habari ndiyo hiyo.
 
Hivi huyu waziiri mkuu hazijui hasira za wananchi mpaka abaelezee. Si wananchi hao hao wamekuwa wakichoma moto vibaka kwa kosa la kukwapua kipochi chenye labda buku mbili tu...............

Hu ufafanuzi ni wizi mtupu na hasa ukizingatia huyo mwandishi wa Pinda ndio yule yule wa EL. Wapi said Ngubaaaaaaaaaaaaa?
 
Majibu ya Mwandishi wa habari wa Waziri yako 'shallow" sana na yanaelekea ku-justify kauli za Waziri Mkuu.
Kwa hili Waziri Mkuu aliteleza. Lakini kwa taratibu zetu sisi, mkubwa huwa hakosei.
 
Mwanakijiji,

Umeona Maelezo ya Waziri Mkuu..Umeyakubali sasa?Mie nashangaa sana kulazimisha jambo wakati wewe mwenyewe hauwapo na unakataa na kulazimsiha jambo ulitakalo..Maswali yako yote ni speculations tu na hakuna hoja ya Msingi uliyouliza!
 
Mkuu Gembe kumbuka magazeti mengi tu kama vile mwananchi, citizen na Majira yaliandika habari hii kwa hiyo maswali ya mwanakijiji yalikuwa na msingi wa kuutafuta ukweli. Na bado still ukweli unaweza kuendelea kutafutwa!
 
PM: Yes, killers of albinos should die

By Mkinga Mkinga (The citizen)

Hapa vp mkuu Gembe?????

People caught red-handed killing albinos should also be killed on the spot, Prime Minister Mizengo Pinda has reiterated.

Mr Pinda told The Citizen on Monday that people who were condemning his remarks did not have an idea of the senseless brutality being wrought upon albinos by killers who were after their body parts.

He said his remarks were in line with the urgency and seriousness with which the Government treated the wave of albino killings in some parts of the country, and reflected its commitment to putting an end to the atrocities once and for all.

Mr Pinda added that his statement would not
have shocked anybody who knew the extent of suffering the killings had caused.

"It may be an unusual statement by a prime minister, and I wish to confirm that I made the remarks to send a clear message to albino killers� they should know that if they are caught, they will have to face the fate they had hoped their victims would suffer," he said in an exclusive interview with The Citizen.

Mr Pinda said he and the Government would no longer tolerate the senseless and brutal killings of human beings just because they happen to be of a different colour.

The Citizen had sought clarification from the prime minister after he was quoted as directing members of the ruling CCM's youth wing to kill people caught in the act of killing albinos. The remarks drew sharp criticism from human rights activists, legal experts and the opposition leaders.

The opposition NCCR-Mageuzi said in a news conference on Sunday that Mr Pinda's remarks were �irresponsible and totally unacceptable�, and asked President Jakaya Kikwete to immediately sack him.

The party's secretary-general, Mr Samuel Ruhuza, said the remarks made a mockery of the principles of the rule of law and encouraged mob justice.
But Mr Pinda brushed aside the criticisms, saying the Government had decided to take the bull by the horns in its war against albino killers.

"A person who knows that he will be killed when caught in the act of killing an albino will think twice before embarking on such an evil mission," he said. Mr Pinda said his statement was not meant to encourage people to take the law into their own hands, but to show that the Government was serious on the issue.

Mr Pinda also said he had directed regional police to place special emphasis on the security of albinos in their areas of jurisdiction.
More than 40 albinos have been killed and mutilated in the past year.

The killers take various body parts which witchdoctors use to make concoctions supposed to make their clients rich.
Last week, Mr Pinda announced the revocation of all licences issued to traditional healers across the country.

The announcement yesterday received the support of some traditional healers in Manyara Region. They said they supported the Government's crackdown against some of their colleagues who were fanning ritual killings.

Those who spoke to this newspaper yesterday in Babati, the regional headquarters, pledged to cooperate with the police in uncovering "fake" healers.

Mr Nyaki Nyaki, an official of the Manyara Traditional Healers Association, said yesterday that they have been ordered by the authorities to reveal the names of their colleagues who were not registered.

Some fortune-tellers said the meeting was hastily convened and that many of their colleagues were not informed in advance.

Manyara regional police boss Luther Mbuttu said police in the region were ready to implement the directive issued by the prime minister.

More than 58 people have been arrested in Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, and Mbeya regions where the belief that albino body parts can make one fabulously wealthy virtually overnight is rife among fortune seekers.

Additional reporting by Mashaka Kibaya in Babati.
 
Hilo la kupatiwa nakala ya hotuba limefikia wapi ?
 
Mwanakijiji,

Umeona Maelezo ya Waziri Mkuu..Umeyakubali sasa?Mie nashangaa sana kulazimisha jambo wakati wewe mwenyewe hauwapo na unakataa na kulazimsiha jambo ulitakalo..Maswali yako yote ni speculations tu na hakuna hoja ya Msingi uliyouliza!

Mkuu Gembe....

...hebu ona majibu aliyotoa Nguba on behalf of PM Pinda

"Alichosema Waziri Mkuu ni kwamba imefika wakati sasa mauaji haya yamechochea hasira ya wananchi wa kawaida kuwa wakimuona muuaji "red-handed" anamchinja Albino na kuchukua kiungo chake, hawawezi kumuacha muuaji huyo. Naye watamshughulikia tu na hawatasubiri kumpeleka polisi....."

1.hivi unahitaji kwenda darasa la saikolojia kujua kuwa hii statement ni hatari!!

2.Kiongozi unatakiwa kuwa mstari wa mbele kusisitiza na kuzingatia sheria........be it kanuni.....be it taratibu.....mbele ya wananchi.....alichotakiwa ni kufanya ni kulaani mauaji...na kusema serikali itachukua hatua kali kuzuia mauaji hayo.......in addition alitakiwa kuomba msaada........kutoka kwa wananchi kwani vyombo vya serikali pekee havitaweza bila msaada huo........
 
Mwanakijiji, Umeona Maelezo ya Waziri Mkuu..Umeyakubali sasa?Mie nashangaa sana kulazimisha jambo wakati wewe mwenyewe hauwapo na unakataa na kulazimsiha jambo ulitakalo..Maswali yako yote ni speculations tu na hakuna hoja ya Msingi uliyouliza!

Mkuu Gembe, ulitaka Mwanakijiji aulize maswali gani?, ili tujue hayo ya msingi.
 
Back
Top Bottom