Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Nimekuelewa sana.Ila ukombozi wa kweli ni mgumu mno.Lazima kuvumiliana.
 
Hii mikopo ingetafutiwa namna ama njia bora ili iwe inatolewa na taasisi imara imara za fedha hasa mabenki. Taasisi hizi ndizo zenye wajibu wa kukopesha na kudai kisheria na pia kuwa na uzoefu, maarifa, weledi na maadili ya kukusanya madeni kwa muda mrefu.

Ingetafutiwa njia sahihi ya kukokotoa riba kupitia njia ya 'reducing balance" badala ya hii ya sasa ambayo imejaa wizi na ubabaishaji mkubwa. Kiwango cha riba kingefanywa kuwa "single digit" mathalani 7.5% ilikumfanya mnufaika kuwa na "saving component" kubwa kwa ajili ya maendeleo yake binafsi.

Haingii akili makato yanoyafanyika kupitia "salary slip" ya mnufaika na kumbukumbu ya salio la deni mtu analodaiwa yakatofautiana na taarifa iliyopo ktk "loan statement" ya Bodi ya Mikopo. Hapo kuna mazingira ya watu kupigwa mchana kweupe.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri:
  • Kila jimbo, waadhirika wa mkopo HESLB wamwandikie barua Mbunge wao na kumuomba alipeleke suala hili bungeni likajadiliwe upya. Katika hilo waainishe karaha wanazokumbana nazo katika ulipaji wa mkopo huo na kuweka mapendekezo yao. Kopi ya barua hiyo wapewe madiwani, mkurugenzi HESLB, waziri wa elimu na mkuu wa mkoa.
  • Ifanyike petition (zikusanywe sahihi za watanzania) wanaotaka sheria hiyo ibadileshwe na baadae apewe Spika na nakala zitumwae kwa hao wote niliowaorodhesha hapo juu.
  • Iandikwe barua maalum ya pamoja kwa mheshimiwa Raisi kumuomba awaangalie wahusika kwaq jicho la huruma na kuwasaidia.
  • Mitandao ya kijamii itumike kama platform ya kuunda umoja wao.
 
Pambaneni wenyewe wasomi wa nchi hii ndio wanaongoza kwa woga na kulalamika pasi na kuchukua hatua.

Wapinzani muwaache wapumzike pambaneni wenyewe.
 
Solution rahisi ingekuwa kila muajiriwa
Awe alikopeshwa au hakukopeshwa akatwe asilimia ndogo sana kama asilimia 3 ya mshahara kuchangia Bodi..

Waliokopeshwa wachangie asilimia 7..

Wangepata hela nyingi bila kuumiza watu
With all the due respect no brother..
Still we are paying taxes na wengine tumemaliza huo mkopo wenye deni la kila siku..
Kila mtu abebe msalaba wake kwa kwel...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…