Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Binafsi nashauri wapinzani wake kimya Wala wasiwasemee mitumishi mipumbavu maana wenyewe mliisaidia ccm kuiba kura na mkawasaliti kina Lissu ambao ndio walikuwa watetezi wenu kwasasa kila mtu ashinde mechi zake Lissu alitaka.kuuwawa kwa kuwatetea nyie Mbowe kaharibiwa vitega uchumi vyake kuwatetea nyinyi wakamvunja mguu mkamwita mlevi Leo hii wanapona majeraha kwa shida walizopitia ili nyie mkombolewe mnataka kuwaita wawasaidie nooooooooo big nooooooooo Salary Slip nakuheshimu Sana ila kwa hili acheni mpate shida mpaka matako yafikiri Kama kichwa Lissu kula bata ubelgiji baba mbowe injoi utajiri wako anko na lema kaa hukohuko uliko acheni hii milofa ya Tanzania ivune ilichopanda.
Nimekuelewa sana.Ila ukombozi wa kweli ni mgumu mno.Lazima kuvumiliana.
 
Tukubali sheria ya Bodi ya Mikopo inayoruhusu makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mtu aliepewa huu mkopo(Siwezi kumuita mnufaika wa huu mkopo maana ni kutiana umasikini) pamoja na tozo ya asilimia 6 kama retention fee, ni sheria katili, mbaya na haistahili kuwepo katika nchi ya watu wanaojitawala.

Hivyo, natoa wito kwa wanasiasa wa upinzani (CCM ndio walileta na kupitisha hii sheria katili hivyo siwahusishi), wanaharakati na wadau wengine kuungana na kuanzisha kampeni ndani na nje ya nchi kuipinga sheria hii iliyowekwa na watu ambao wamesahau walikotoka huku baadhi yao walisoma vyuo vikuu bure kabisa kwa gharama za serikali.

Ikiwezekana,tushawishi taasisi za fedha za kimataifa na nchi wahisani kusitisha mikopo na misaada kwa serikali mpaka watapobadili au kufuta kabisa hii sheria kandamizi kama walivyofanya katika kutetea haki ya mtoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Njia mojawapo iwe ni kutumia mitandao ikiwa ni pamoja na kuanzisha hashtags za kupinga uwepo wa hii sheria kwani haizingatii mishahara na vipato duni vya watanzania walio wengi.

Niseme tu, Waafrika wanastahili kuendelea kutawaliwa kwa njia kama hizi, vinginevyo tutaumizana sana.

Sijui hizi ni roho za namna gani!
Hii mikopo ingetafutiwa namna ama njia bora ili iwe inatolewa na taasisi imara imara za fedha hasa mabenki. Taasisi hizi ndizo zenye wajibu wa kukopesha na kudai kisheria na pia kuwa na uzoefu, maarifa, weledi na maadili ya kukusanya madeni kwa muda mrefu.

Ingetafutiwa njia sahihi ya kukokotoa riba kupitia njia ya 'reducing balance" badala ya hii ya sasa ambayo imejaa wizi na ubabaishaji mkubwa. Kiwango cha riba kingefanywa kuwa "single digit" mathalani 7.5% ilikumfanya mnufaika kuwa na "saving component" kubwa kwa ajili ya maendeleo yake binafsi.

Haingii akili makato yanoyafanyika kupitia "salary slip" ya mnufaika na kumbukumbu ya salio la deni mtu analodaiwa yakatofautiana na taarifa iliyopo ktk "loan statement" ya Bodi ya Mikopo. Hapo kuna mazingira ya watu kupigwa mchana kweupe.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Tukubali sheria ya Bodi ya Mikopo inayoruhusu makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mtu aliepewa huu mkopo(Siwezi kumuita mnufaika wa huu mkopo maana ni kutiana umasikini) pamoja na tozo ya asilimia 6 kama retention fee, ni sheria katili, mbaya na haistahili kuwepo katika nchi ya watu wanaojitawala.

Hivyo, natoa wito kwa wanasiasa wa upinzani (CCM ndio walileta na kupitisha hii sheria katili hivyo siwahusishi), wanaharakati na wadau wengine kuungana na kuanzisha kampeni ndani na nje ya nchi kuipinga sheria hii iliyowekwa na watu ambao wamesahau walikotoka huku baadhi yao walisoma vyuo vikuu bure kabisa kwa gharama za serikali.

Ikiwezekana,tushawishi taasisi za fedha za kimataifa na nchi wahisani kusitisha mikopo na misaada kwa serikali mpaka watapobadili au kufuta kabisa hii sheria kandamizi kama walivyofanya katika kutetea haki ya mtoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Njia mojawapo iwe ni kutumia mitandao ikiwa ni pamoja na kuanzisha hashtags za kupinga uwepo wa hii sheria kwani haizingatii mishahara na vipato duni vya watanzania walio wengi.

Niseme tu, Waafrika wanastahili kuendelea kutawaliwa kwa njia kama hizi, vinginevyo tutaumizana sana.

Sijui hizi ni roho za namna gani!
Ushauri:
  • Kila jimbo, waadhirika wa mkopo HESLB wamwandikie barua Mbunge wao na kumuomba alipeleke suala hili bungeni likajadiliwe upya. Katika hilo waainishe karaha wanazokumbana nazo katika ulipaji wa mkopo huo na kuweka mapendekezo yao. Kopi ya barua hiyo wapewe madiwani, mkurugenzi HESLB, waziri wa elimu na mkuu wa mkoa.
  • Ifanyike petition (zikusanywe sahihi za watanzania) wanaotaka sheria hiyo ibadileshwe na baadae apewe Spika na nakala zitumwae kwa hao wote niliowaorodhesha hapo juu.
  • Iandikwe barua maalum ya pamoja kwa mheshimiwa Raisi kumuomba awaangalie wahusika kwaq jicho la huruma na kuwasaidia.
  • Mitandao ya kijamii itumike kama platform ya kuunda umoja wao.
 
Pambaneni wenyewe wasomi wa nchi hii ndio wanaongoza kwa woga na kulalamika pasi na kuchukua hatua.

Wapinzani muwaache wapumzike pambaneni wenyewe.
 
Solution rahisi ingekuwa kila muajiriwa
Awe alikopeshwa au hakukopeshwa akatwe asilimia ndogo sana kama asilimia 3 ya mshahara kuchangia Bodi..

Waliokopeshwa wachangie asilimia 7..

Wangepata hela nyingi bila kuumiza watu
With all the due respect no brother..
Still we are paying taxes na wengine tumemaliza huo mkopo wenye deni la kila siku..
Kila mtu abebe msalaba wake kwa kwel...
 
Back
Top Bottom