Tukubali sheria ya Bodi ya Mikopo inayoruhusu makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mtu aliepewa huu mkopo(Siwezi kumuita mnufaika wa huu mkopo maana ni kutiana umasikini) pamoja na tozo ya asilimia 6 kama retention fee, ni sheria katili, mbaya na haistahili kuwepo katika nchi ya watu wanaojitawala.
Hivyo, natoa wito kwa wanasiasa wa upinzani (CCM ndio walileta na kupitisha hii sheria katili hivyo siwahusishi), wanaharakati na wadau wengine kuungana na kuanzisha kampeni ndani na nje ya nchi kuipinga sheria hii iliyowekwa na watu ambao wamesahau walikotoka huku baadhi yao walisoma vyuo vikuu bure kabisa kwa gharama za serikali.
Ikiwezekana,tushawishi taasisi za fedha za kimataifa na nchi wahisani kusitisha mikopo na misaada kwa serikali mpaka watapobadili au kufuta kabisa hii sheria kandamizi kama walivyofanya katika kutetea haki ya mtoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Njia mojawapo iwe ni kutumia mitandao ikiwa ni pamoja na kuanzisha hashtags za kupinga uwepo wa hii sheria kwani haizingatii mishahara na vipato duni vya watanzania walio wengi.
Niseme tu, Waafrika wanastahili kuendelea kutawaliwa kwa njia kama hizi, vinginevyo tutaumizana sana.
Sijui hizi ni roho za namna gani!