Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Ni ngumu kupinga chochote kwenye nchi kama hii!
1098090.jpg
 
Tukubali sheria ya Bodi ya Mikopo inayoruhusu makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mtu aliepewa huu mkopo(Siwezi kumuita mnufaika wa huu mkopo maana ni kutiana umasikini) pamoja na tozo ya asilimia 6 kama retention fee, ni sheria katili, mbaya na haistahili kuwepo katika nchi ya watu wanaojitawala.

Hivyo, natoa wito kwa wanasiasa wa upinzani (CCM ndio walileta na kupitisha hii sheria katili hivyo siwahusishi), wanaharakati na wadau wengine kuungana na kuanzisha kampeni ndani na nje ya nchi kuipinga sheria hii iliyowekwa na watu ambao wamesahau walikotoka huku baadhi yao walisoma vyuo vikuu bure kabisa kwa gharama za serikali.

Ikiwezekana,tushawishi taasisi za fedha za kimataifa na nchi wahisani kusitisha mikopo na misaada kwa serikali mpaka watapobadili au kufuta kabisa hii sheria kandamizi kama walivyofanya katika kutetea haki ya mtoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Njia mojawapo iwe ni kutumia mitandao ikiwa ni pamoja na kuanzisha hashtags za kupinga uwepo wa hii sheria kwani haizingatii mishahara na vipato duni vya watanzania walio wengi.

Niseme tu, Waafrika wanastahili kuendelea kutawaliwa kwa njia kama hizi, vinginevyo tutaumizana sana.

Sijui hizi ni roho za namna gani!!
Tatizo Watanzania tulikua tunaishi kwa mazoea Ndio maana tunanung'unika kutwa
Tii sheria za nchi bila shuruti zozote utastarehe
Hii sio serikali ya kugeuza nchi shamba la Bibi hayo mambo hakuna
Hivi wewe hauna macho ujionee vile Serikali hii imewaneemesha Wananchi?
Kila mtu mambo yake Safi na maisha mazuri mnoo
Tanzanian ya Magufuli raha sana kuanzia
1 huduma za Afya
2 shule bure
3 maji kila pahala
4 Miundo mbinu
5 ajira za kumwaga

Kweli Tanzania tupo vizuri sana mpaka nchi jirani zinatuonea wivu
 
Nakushauri ukaombewe,leo jumapili.
 
Tukubali sheria ya Bodi ya Mikopo inayoruhusu makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mtu aliepewa huu mkopo(Siwezi kumuita mnufaika wa huu mkopo maana ni kutiana umasikini) pamoja na tozo ya asilimia 6 kama retention fee, ni sheria katili, mbaya na haistahili kuwepo katika nchi ya watu wanaojitawala.

Hivyo, natoa wito kwa wanasiasa wa upinzani (CCM ndio walileta na kupitisha hii sheria katili hivyo siwahusishi), wanaharakati na wadau wengine kuungana na kuanzisha kampeni ndani na nje ya nchi kuipinga sheria hii iliyowekwa na watu ambao wamesahau walikotoka huku baadhi yao walisoma vyuo vikuu bure kabisa kwa gharama za serikali.

Ikiwezekana,tushawishi taasisi za fedha za kimataifa na nchi wahisani kusitisha mikopo na misaada kwa serikali mpaka watapobadili au kufuta kabisa hii sheria kandamizi kama walivyofanya katika kutetea haki ya mtoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Njia mojawapo iwe ni kutumia mitandao ikiwa ni pamoja na kuanzisha hashtags za kupinga uwepo wa hii sheria kwani haizingatii mishahara na vipato duni vya watanzania walio wengi.

Niseme tu, Waafrika wanastahili kuendelea kutawaliwa kwa njia kama hizi, vinginevyo tutaumizana sana.

Sijui hizi ni roho za namna gani!!
Ninyi mlioathiriwa na hiyo Bodi anzisheni movement then mtaungwa mkono.

Yaani mmekaa tu mnasubiri eti wanaharakati ingilieni kati, kweli ???

Sasa kama wewe unayeumia huoni tatizo unataka vipi mtu mwingine akupiganie
 
Nyie wakopeshwaji hamkawii kuwageuka na kuisifu mikopo na mkopeshaji!
 
Tuache kuzunguka hii shida kaileta Magufuli tusione aibu wala woga kuisema, think tank uchwara na waoga wakamkubalia baada ya kuja na mikakati mfuu ya kiuchumi ya ndege, vivuko, reli mpya, bwawa la umeme, kuhamia dodoma, serikali ilitanua wigo mithili ya watoa tigo kwenye matumizi wakati kapu halisia halitoshi,huyu labda awe mamluki ila atakuwa na maisha mafupi baada ya kuondoka 2025, atazodolewa live live maana anatumia uchumi wa kijima sana. Miundombinu mingi budget items za kupiga pesa, 10%, shareholder syndrome katika ufisadi, ukizoea kupitia wizara ya ujenzi na fursa ya migodi mipya haipo hii ndio aina endelevu ya ufisadi wa Marais wajao pia kauli mbiu ya kula na kipofu. Tanzania inawatu wa kipumbavu sana mnajua ukweli tatizo nani mnakuwa wanafiki semeni ukweli bodi ya mikopo kikwete aliiacha vizuri tu. Rais ana wajibu wa kuwa baba wa huruma, mfariji, msikivu, mwenye hekima, busara, mstahimilivu, mkomavu, jasiri wa kuhimili kukosolewa vinginevyo hataongeza thamani yoyote kupitia hicho cheo.
 
Eti wapinzani wawasemeee mavi yenu watumishi msio na shukrani Tena hayo makato yazidi Mara alfu huku salary slip zenu zikijaa madeni ya

Maboto
Nmb
Crdb
Letshego
Faidika
ABC

Ninyi mlioathiriwa na hiyo Bodi anzisheni movement then mtaungwa mkono.

Yaani mmekaa tu mnasubiri eti wanaharakati ingilieni kati, kweli ???

Sasa kama wewe unayeumia huoni tatizo unataka vipi mtu mwingine akupiganie
Mnafiki tu wewe.Nyie ndio watetezi wa Jiwe.
 
FAHAMU KIDOGO KUHUSU LOAN BOARD NA SHERIA MPYA

```Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao . Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA Yaani watoto wa maskini.

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi ( Watz wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano.
Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.

Basic salary yake ni 1.5 Mil
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo,

Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000

Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha!

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil ( 225,000X12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8

Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil

Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

Mapendekezo

1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.

USHAURI.

1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.
 
Walibadilisha sheria ya makato kutoka 8% mpaka 15%. Mabadiliko haya yakawahusu hadi wale ambao walikuwa wanakatwa 8% katika mshahara. Wadau walipiga kelele lakini bodi hawakujali.

Sasa wameanza tena uhabaishaji wao kwa kuongeza makato (retention fee) kitu ambacho hakipo katika mikataba ambayo tulisaini miaka hiyo mfano mkataba wa bodi wa mwaka 2009.

Bodi wanatakiwa waheshimu mikataba tuliyosainishana, mfano mkataba wao wa mwaka 2009.

Bodi wakumbuke kuwa, mabadiliko yoyote hayapaswi kuwaathiri wale ambao tayari wamo katika makubaliano ya awali.

Kukaa kwetu kimya wasidhani tunaridhika na unyanyasaji wao. La hasha! tunasubiri muda tutapata haki yetu na kulipwa fidia kubwaaa.

Ni kwamba, nimeitunza nakala ya mkataba wa bodi niliousaini mwaka 2009.

Pia, kwa sasa, kila mwezi nadownload salary slip, nazi save kwenye mtandao, pia naziprint mpaka nitakapomaliza deni mwaka 2026.Salary slip ikiwa nyeupe, itakuwa ngumu kukubali makato mengine ya bodi, bodi wakilazimisha, itabidi kwenda mahakamani.

Kutokana na kuvunja mkataba, nimepanga kuwashitaki bodi ya mikopo hata kama ni mwaka 2040! Najua ipo siku mahakama itakuwa huru. Kwahiyo, chonde chonde bodi, jaribuni kufikiria future. Mtakuja kulipa fidia kubwa huko mbeleni.

Kwa sasa mmeshika mpini tumekaa kimya ila wengine tuna jambo letu, tunakusanya ushahidi. Cha ajabu, ikifika mwaka 2040 mahakama ikiamua tulipwe pesa ndefu kama fidia, wapo watakaotuona sisi siyo wazalendo, wakati leo tunavunjiwa mikataba, na wamekaa kimyaa.

Ushauri wa bure, bodi iombeni serikali hela ya kuwakopesha wanafunzi, mana ni jukumu la serikali kuwasomesha raia wake. Mnapotaka kujiendesha ndipo mnapoanza kutubambikia madeni, mwisho wa siku tunaishi maisha ya bila furaha.
Umeongea kwa uchungu mno. Pokea like yangu ya upendo.
 
Back
Top Bottom