Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Wito: Wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wadau wengine, anzeni kampeni ya kupinga sheria hii ya Bodi ya Mikopo ndani na nje ya nchi

Solution rahisi ingekuwa kila muajiriwa
Awe alikopeshwa au hakukopeshwa akatwe asilimia ndogo sana kama asilimia 3 ya mshahara kuchangia Bodi..

Waliokopeshwa wachangie asilimia 7..

Wangepata hela nyingi bila kuumiza watu
Ukope wewe mimi nikose mkopo usome vizuri nisome kwa shida halafu tulipe wote acha utani. Sema serikali iondoe Riba na ipunguze makato.
 
Na bado tutaona mengi, si wamebaki peke yao. Wanatumia nguvu nyingi kukusanya kila kona ili sifa iende kwa CCM kuwa imefanya mengi. Kwenye kampaini nilikuwa nashangaa wanavyuo wamevaa kijani Na njano wanaruka Na kushangilia. Hays ndiyo malipo
 
Akisoma aliepata mkopo akawa daktari si
Atakutibia hata wewe??
Ni kweli kaka shule yangu nimesoma kwa shida sana. Hivyo basi hili suala liende kwa mhusika. Pia tuwe na utamaduni wa kulipia watoto karo kwa kubana matumizi yetu ili mkopo unakuwa kwa wahitaji kwelikweli.
 
Kimsingi haya maisha ndiyo tuliyoamua kuyachagua na kuyaishi.... Tuvumilie... Hii sheria imepitishwa na watu wazima wanaojielewa kabisa...
Wala Si kwa bahati mbaya... Wanaelewa wanachokifanya....

Na ni wabunge wa chama pendwa, ambao tuliwachagua kwa moyo mmoja kabisa kwamba wakatuwakilishe....

So, hatuna namna nyingine..
 
Binafsi nashauri wapinzani wake kimya Wala wasiwasemee mitumishi mipumbavu maana wenyewe mliisaidia ccm kuiba kura na mkawasaliti kina Lissu ambao ndio walikuwa watetezi wenu kwasasa kila mtu ashinde mechi zake Lissu alitaka.kuuwawa kwa kuwatetea nyie mbowe kaharibiwa vitega uchumi vyake kuwatetea nyinyi wakamvunja mguu mkamwita mlevi Leo hii wanapona majeraha kwa shida walizopitia ili nyie mkombolewe mnataka kuwaita wawasaidie nooooooooo big nooooooooo Salary Slip nakuheshimu Sana ila kwa hili acheni mpate shida mpaka matako yafikiri Kama kichwa Lissu kula bata ubelgiji baba mbowe injoi utajiri wako anko na lema kaa hukohuko uliko acheni hii milofa ya Tanzania ivune ilichopanda.
Nakuunga mkono!
 
Pitia hiyo Payslip hapo juu. Itamchukua miaka 28 huyo mfanyakazi kulipa hilo deni na kama Ile riba itakuwepo basi ni zaidi ya hapo. Ni wazi hataweza kulipa hilo deni wakati wa uhai wake. Na kibaya zaidi hataweza kupata mafao yake baada ya kustaafu kazi. Huu ni mnyororo wa mateso ambao vijana wetu wamefungwa shingoni mwao. Kuna namna nyingi sana za kushusha molari za wafanyakazi. Lakini hii inavunja rekodi.
 
Hivi ule muda muafaka umefika? au tuendelee kuvuta subira!?
Kweli bora tungepata uhuru mwaka 1998 kuliko ule wa 61 wa mwl.
 
Eti wapinzani wawasemeee mavi yenu watumishi msio na shukrani Tena hayo makato yazidi Mara alfu huku salary slip zenu zikijaa madeni ya

Maboto
Nmb
Crdb
Letshego
Faidika
ABC nk

Wapuuzi nyie.
Mufindi wanasemaje apo mkuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huyo ni chamtoto. Wapo wahitimu waliosomea Urusi. Madeni yao ni kiasi cha shilingi milioni 97 (Tsh. 97,000,000) na baadhi yao makato ni kiasi cha shilingi 250,000 kwa mwezi. Kwa mwaka wanalipa shilingi milioni 3. Mungu akiwaweka hai watamalizia mikopo hiyo baada ya miaka 33 hivi na hiyo ni kama Ile riba iliyowekwa itatolewa. Wengi wao wamekwishafanya kazi kwa miaka karibia minne. Kwa hesabu za kawaida deni lao kwa sasa lingekuwa limepungua kwa shilingi 12,000,000. Cha kushangaza kwa sasa kule HESLB deni linasomeka shilingi 94,000,000. Na hii ni kwa sababu ya Ile riba ambayo ni mnyororo wa kuwamaliza hawa vijana. Swali la kujiuliza, je Waheshimiwa hawakupiga hesabu kwanza kabla ya kupitisha sheria hii kandamizi?
Nimebaki mdomo wazi baada ya kuona hii kitu, ingawa sijui kama ni kweli au ni ya kutengeneza... View attachment 1673205
 
Huyo ni chamtoto. Wapo wahitimu waliosomea Urusi. Madeni yao ni kiasi cha shilingi milioni 97 (Tsh. 97,000,000) na baadhi yao makato ni kiasi cha shilingi 250,000 kwa mwezi. Kwa mwaka wanalipa shilingi milioni 3. Mungu akiwaweka hai watamalizia mikopo hiyo baada ya miaka 33 hivi na hiyo ni kama Ile riba iliyowekwa itatolewa. Wengi wao wamekwishafanya kazi kwa miaka karibia minne. Kwa hesabu za kawaida deni lao kwa sasa lingekuwa limepungua kwa shilingi 12,000,000. Cha kushangaza kwa sasa kule HESLB deni linasomeka shilingi 94,000,000. Na hii ni kwa sababu ya Ile riba ambayo ni mnyororo wa kuwamaliza hawa vijana. Swali la kujiuliza, je Waheshimiwa hawakupiga hesabu kwanza kabla ya kupitisha sheria hii kandamizi?
Alafu unakuta kuna watu bado wanaichagua CCM kwa maana ya Raisi na Wabunge wa CCM waliotuletea sheria katili kiasi hiki.
 
Pendekeza slotutions unazoona zinafaa lengo likiwa ni kupinga hii sheria na kutaka iondolewe au kufutwa kabisa.

Kwa maneno mengine, taja hizo solutions hapa na utakuwa umesaidia sana.
Solution ni kupanga njia za kulipa deni nasio kupanga njama za kukwepa kulipa deni,

Wewe unapanga namna ya kukwepa kulipa deni ambalo kwa namna furani limekuwezesha kupata hako ka digrii kako wakati pesa yenyewe ni chini ya 20M ilikhali kuna watu tunadaiwa 20M+ ambazo tuliko Benki kwaajili ya biashara mwisho Wa siku biashara zikakwama na bado tunalipa deni.

Think big brother.
 
Upo sawa kabisa. Deni lazima lilipwe hakuna njia mbadala kwani dawa ya deni ni kulipa. Tatizo hapa ni jinsi hilo deni linavyolipwa. Katika kitabu cha William Shakespeare "The Merchants of Venice" (Mabepari wa Venice) Shylock aliweka sharti la kupewa ratili moja ya nyama iwapo mdeni wake angeshindwa kulipa deni hilo kwa wakati. Kama siyo busara ya Hakimu basi mdaiwa huyo angekufa baada ya kutoa hiyo ratili ya nyama yake. Hakimu aliagiza kwamba deni lazima lilipwe. Lakini pia alitoa sharti kwamba nyama itakayokatwa iwe ni ratili moja, isizidi wala isipungue. Pili iwe ni nyama tu na siyo damu kwani damu haipo katika mkataba wa mkopo aliompatia mdeni wake. Shylock hayo yakamshinda na ndio ikawa ahueni kwa yule mdaiwa.
Kitendo cha kuweka riba ambayo inaendelea kwa pesa ambayo haijalipwa inalifanya deni kuongezeka kwa wale ambao hata hawana ajira kiasi cha kwamba wakianza kulipa deni linakuwa kubwa sana. Hao wanaolipa deni linapungua kwa kasi ndogo sana kwa vile kunakuwepo na riba ambayo huongeza ukubwa wa deni hilo. Ipo mifano inaonesha hata baada ya kustaafu bado wapo ambao watatumia mafao yao kulipa baki ya deni hilo. Ni kweli deni lazima lilipwe, lakini utafutwe utaratibu mzuri ambao haumuumizi mdaiwa.
 
Kwa jina la yesu wafanyakazi siio watu wakutetewa kabisaaa maana niwanafiki mno ifikapo maymosi utawaona namabango yao yakumsifia mkulu utazani hawana changamoto
Nb
Yale mabago yasifa nautukufu yatawasaidia waacheni wafanyakazi
Gwara again[emoji69]
 
Yaani mwanafunzi anamaliza chuo ajira hakuna, halafu unamwambia kila akipitisha muda hajamaliza kulipa deni unaongeza riba, hii maana yake tutaendelea kuwa wafungwa wa kulipa hiyo mikopo miaka yetu yote.

Kwanini serikali angalau isitoe muda fulani atleast miaka mitano ndio waanze kuweka riba ili kumpunguzia mzigo huyu mwanafunzi aliemaliza chuo asie na ajira, na wala hajui ataipata lini? japo binafsi nashauri riba iondolewe kabisa.

Riba ni sawa na wizi, kama nimetumia mfano milioni 5 kulipia gharama zangu za chuo mpaka kumaliza, kwanini nije kulipia zaidi hata ambazo sikutumia? au huu mchezo umewekwa makusudi kuwakatisha tamaa waombaji wa mikopo?

Naishauri serikali itafute vyanzo vingine vya mapato, kumkamua mwanafunzi asie na ajira mtaani ni dhambi.
Halafu anajitokeza mtu anasema "serikali ya wanyonge", "serikali sikivu",n.k.
 
Kwa jina la yesu wafanyakazi siio watu wakutetewa kabisaaa maana niwanafiki mno ifikapo maymosi utawaona namabango yao yakumsifia mkulu utazani hawana changamoto
Nb
Yale mabago yasifa nautukufu yatawasaidia waacheni wafanyakazi
Gwara again[emoji69]
Yote sawa,Ila nakuomba usitumie jina la Yesu humu.Tafadhali,Yesu ni zaidi ya tunavyomfahamu.
 
Back
Top Bottom