Huyo ni chamtoto. Wapo wahitimu waliosomea Urusi. Madeni yao ni kiasi cha shilingi milioni 97 (Tsh. 97,000,000) na baadhi yao makato ni kiasi cha shilingi 250,000 kwa mwezi. Kwa mwaka wanalipa shilingi milioni 3. Mungu akiwaweka hai watamalizia mikopo hiyo baada ya miaka 33 hivi na hiyo ni kama Ile riba iliyowekwa itatolewa. Wengi wao wamekwishafanya kazi kwa miaka karibia minne. Kwa hesabu za kawaida deni lao kwa sasa lingekuwa limepungua kwa shilingi 12,000,000. Cha kushangaza kwa sasa kule HESLB deni linasomeka shilingi 94,000,000. Na hii ni kwa sababu ya Ile riba ambayo ni mnyororo wa kuwamaliza hawa vijana. Swali la kujiuliza, je Waheshimiwa hawakupiga hesabu kwanza kabla ya kupitisha sheria hii kandamizi?