Wanabodi
Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.
View: https://www.youtube.com/live/u5PkOqrHdZI?si=Mtma0U4QBfJ8TJ6x
Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo, ili aweze kubadilika kutoka TAL mwanaharakati into TAL Stateanship!.
TAL lazime abadilike kuachana na vibwagizo vya uanaharakati, into real politics vinginevyo anakwenda kuizamisha Chadema kwenye a pit latrine!.
Hivyo hili ni bandiko la wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze to play the real politics of reality, hii falsafa ya TAL ya "No Reforms No Election" is not real!, ni utopian politics!.
TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!.
Hizi ni utopian politics, sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.
Mmoja wa washauri hao wa bure wa kujitolea ni huyu Mwana JF Maarufu sana, Mkuu
Mzee Mwanakijiji , msikilizeni hapa amewashauri nini Chadema na amemshauri nini TAL.
View: https://youtu.be/GUjpxNTSdig Ushauri huu ulitolewa kwa TAL miaka 5 iliyopita, Chadema mtafuteni huyu mtu atawasaidia sana!.
Mimi pia kwa upande wangu, nimeisha wasaidia sana Chadema kwa kuwashauri,
- Nilimshauri Lissu aache uanaharakati aonyeshe statemamship JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship
- 2015 Chadema ilikuwa waingie ikulu lakini kuna makosa waliyafanya, Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... sasa Chadema wana fursa tena ambayo imejotokeza kama zali, wasiridie makosa!
- Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua hapa niliwashauri Chadema namna ya kujinasua, ushauri wangu umefuatwa ndio Chadema hii inayoiona sasa, umeutambua uchaguzi na sio uchavuzi, imelitambua Bunge, imemtambua rais, sasa Chadema inalamba ruzuku ndio hii ipo!.
- Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane! hapa Chadema walikuwa hawamtambui mbunge wake, baada ya ushauri huu, sasa wanamtambua!.
- Ushauri wa bure: CHADEMA iachane na issue ya Wabunge wake 19, iwasamehe waendelee na Ubunge wao. Kwa muda uliobakia kuwatengua hakuna maslahi yoyote! hapa nimewaombea msamaha hawa wabunge, Chadema haina wanawake wowote wa calibre ya Halima Mdee, Ester Bulaya na Esta Matiko!.
- Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...
- Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini hapa niliilaumu Chadema hawajui wanataka nini na watapataje, hata sasa Chadema chini ya Lissu, bado hawajitambui!.
- CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena! hapa niliwalaumu Chadema hawajipangi!, hadi sasa chini ya TAL, Chadema haijajipanga na isiposaidiwa, haijipangi!. Huu ni mwaka wa uchaguzi, TAL anazungumzia no reforms no election, amepanga kusimamisha uchaguzi kwa maandamano!. Uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa kwa TAL na Chadema, badala ya kupanga mikakati ya kuchangamkia fursa, watu wanapanga kususia!.
Natoa wito, kwa watu wowote wenye uwezo, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa adhimu kwa Chadema kuichangamkia.
TAL na Chadema Wasaidiwe!.
Paskali