Wizara husika imchunguze Pastor Dominick (kiboko ya wachawi)

Wizara husika imchunguze Pastor Dominick (kiboko ya wachawi)

Kwakuwa amepita kwenye njia ya dini sidhani kama serikali itatoa tamko hapo.
Wenye dini yao waacheni "wahudumiwe"
 
Yule mwamba tapeli sana eti alihamisha ukichaa kwa mgonjwa wa kichaa akampa mwingine yani matukio yake anayapanga kitoto sana na baunsa lake mwarabu fighter yule aliyekua baunsa wa diamond atakua anajua siri nyingi sana za jamaa yule
Ndo staged miracles hizo mkuu ,wanapangwa kitoto,Mwarabu atakua anajua
 
Naomba kuwasilisha hoja/ mjadala juu ya huyu kiboko ya Wachawi, Serikali inapaswa kumchunguza kupitia wizara husika kabla hatujafika hatua ya Mackenzie wa Kenya, wanaanzaga taratibu baadae yatakua makubwa.

1. Mahubiri yake na maombi ni chonganishi(ni kama ramli), anagombanisha ndugu bila ushahidi.

2. Simu zake za wagonjwa ni za mchongo wanapangwa(staged miracles).

3. Mamlaka husika zichunguze miamala ya account zake kuna element za utakatishaji fedha(MUHIMU SANA)

4. Radio times 100.5 kama wanaweza wasijali pesa za kurushia matangazo wasikilize kinachofanyika kisha waamue kuendelea kutangaza ama wanawe mikono kama pilato kwa kukwepa hatia ya siku za usoni.
Sikuhizi wanaoenda kwa waganga wanapoteza muda waende kwa manabii tu.
 
Yaachie majinga yapigwe usiyahurumie ,tena ikiwezekana huyo nabii awatoboe na washeri zao wote wake kwa waume.
Tehtehtehtehteh nimecheka kama mazuri
 
Back
Top Bottom