A
Anonymous
Guest
Watumishi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Mtwara (COHAS) tunaomba msaada wa Wizara ya Afya kutokana na changamoto tunazokabiliana nazo chini ya uongozi wa chuo chetu.
Tunadai stahiki za watumishi wanaosafiri kikazi, hazilipwi, Kiongozi wetu mkuu na Mtu wa Fedha wakitajwa kujilipa katika safari ambazo baadhi yake hazikufanyika. Tunapohoji, tunaambiwa hakuna fedha, jambo linalotukatisha tamaa.
Mtu wa Fedha anatumia vibaya fedha za taasisi lakini anatetewa na kiongozi huyo. Miradi mbalimbali ya chuo, ikiwemo mradi wa sare za wanafunzi, imekuwa na changamoto ya kutopatikana kwa taarifa za mapato na matumizi.
Watumishi wanapohoji, kiongozi huyo huwa mkali na kuwajengea chuki, tukidai uchunguzi kunakuwa na vikwazo vingi.
Tumekuwa tukijaribu kumshauri mkuu wa chuo kuhusu malipo ya stahiki na matumizi ya fedha za taasisi, lakini hali imekuwa ngumu. Watumishi wengi wanaogopa kupeleka malalamiko yao kwa uongozi wa juu wa Wizara kwa kuwa kiongozi huyo wa juu huwaambia hakuna atakayemchukulia hatua, akitaja ukaribu wake na kiongozi wa idara ya mafunzo.
Tunaomba Wizara ya Afya iingilie kati, ichunguze tuhuma hizi, ihakikishe watumishi wanalipwa stahiki zao na hatua stahiki zinachukuliwa kwa wahusika endapo makosa yatathibitika. Hali ya watumishi imekuwa mbaya, wamekata tamaa na hawana pa kusemea.
Tumeamua kuwasilisha kero hizi kwa matumaini ya kupata msaada na kurejesha uwajibikaji chuoni, kwani tumeshuhudia mengi mfano kuna mtu/watu analipwa malipo ya safari wakati hajasafiri, hiyo ni kwa kuwa tu yeye ana/wana nguvu kuliko Watumishi wengine.