Wizara: Tanzania ipo tayari Kuwezesha Wananchi kunufaika na fursa za akili unde

Wizara: Tanzania ipo tayari Kuwezesha Wananchi kunufaika na fursa za akili unde

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Tanzania imesesema ipo tayari kwa ajili ya Kuwezesha Wananchi kunufaika na fursa za akili unde ikiwemo kuwa na mifumo ,pamoja na miundombinu itakayo linda faragha na usalama wa taarifa binafsi wakati wa matumizi ya akili unde.

Akizungumza kwa niaba ya serikali ya tanzania katika jukwaa la kwanza la wadau wa akili unde linalofanyika nchini likihusisha watalaamu kutoka katika Mataifa mbalimbali ikiwemo Uingereza, Ujerumani, Estonia na Mataifa jirani ya Afrika Mashariki, mkurugenzi wa tume ya tehama Dokta Nkundwe Moses Masaga amesema, utayari huo unakuja kwa kuweka sera na kanuni ambazo zitalinda usalama na faragha ya data na taarifa binafsi za watumiaji wa akili unde

Kwa upande wake Yusufu Kilewo Mtaalamu wa masuala ya Usalama Mtandaoni, amesema utayari wa tanzania katika matumizi ya akili unde una chagizwa na ujio wa mkakati na miongozo itakayo linda maadili ya Mtanzania katika Matumizi ya akili unde

Nao baadhi ya washiri wa mkutano huo wamesema jukwa la akili unde litasaidia wadau hao kuoeana Maarifa na kuja na mikakati ikiwemo mapendekezo ya uwepo wa shwria na kanuni kwa ajili ya kusimamia matumizi ya akili unde hasa ikizongatiwa ongezwko la matumizi ya simu janja na intaneti nchini

Katika Hatua nyingine Serikali ya Tanzania na Urusi zimesaini makubalino ya ushirikiano katika sekta ya TEHAMA pamoja na kukuza uchumi wa kidigitali

Wakizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa tume ya TEHAMA Dokta Nkundwe Moses Masaga pamoja na Mwakiliahi wa Serikali ya Urusi anayeshughulikia masomo kwa nchi za Afrika Andrey Maslov, Wamesema ushirikiano huo utawezeaha mafunzo.ufanyaji tafiti pamoja na kuendeleza sekta ya teknolojia ili kukuza na kuendeleza jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wa kidigitali
 
Back
Top Bottom