#COVID19 Wizara ya Afya hamtutendei haki, kipimo cha COVID19 ni ghali sana

#COVID19 Wizara ya Afya hamtutendei haki, kipimo cha COVID19 ni ghali sana

Mkurugenzi. Sio mkulugenzi

Mara ya mwisho. Sio mala ya mwisho

Huzuni. Sio hudhuni.

Darura. Sio dharula.

Halafu. Sio alafu.

Bora usiende kwenye huo usaili, ungepoteza nauli na tozo ya kipimo. Hujui kuandika Kiswahili, utaweza nini, kupikia chai maofisa?
Mkuu unadhani wote wanaenda interview za kuandika wapo watu hawajui kuandika wala hicho kizungu cha kuunga ila kwa kazi zao wanapiga pesa ndefu Sana kwa mwezi...
 
Ungeweza kurekebisha tu bila kejeli zako, hii sio mada ya kujifunza lugha ya kiswahili ndugu, i hate this kind/level of stupidity , watu wanaleta thread zao badala ya kurekebisha tu palipokosewa mtu unaanza kukejeli as if you are perfect in everything.
Hapo kaleta chuki ya kuona wewe umesema unaenda kutafuta kazi nje ya Nchi tu hakuna kingine hao mpaka uzi wa taarifa ya ajali wao wapo busy kujifanya kukosoa....
 
Ni wanakomoa baada ya wananchi kuwa wajinga kwa kukataa wokovu na kumpeleka Rais mataputapu ikulu!
 
Mkuu unadhani wote wanaenda interview za kuandika wapo watu hawajui kuandika wala hicho kizungu cha kuunga ila kwa kazi zao wanapiga pesa ndefu Sana kwa mwezi...
Ndefu sana. Sio ndefu Sana.
Usichanganye herufi kubwa na ndogo katikati ya tungo.

Unaenda nje ya nchi kufanya usaili mtu kuandika Kiswahili hujui, utapiga hela ndefu kwa kazi gani ya kuajiriwa, kuchimba bomba la mafuta? Brunei labda, sio Uganda!

Usiende kupoteza nauli na tozo ya kipimo cha Covid, utarudi na hasara na maambukizi ya Covid. Kaa chini jifunze kwanza kusoma na kuandika.
 
Ndefu sana. Sio ndefu Sana.
Usichanganye herufi kubwa na ndogo katikati ya tungo.

Unaenda nje ya nchi kufanya usaili mtu kuandika Kiswahili hujui, utapiga hela ndefu kwa kazi gani ya kuajiriwa, kuchimba bomba la mafuta? Brunei labda, sio Uganda!

Usiende kupoteza nauli na tozo ya kipimo cha Covid, utarudi na hasara na maambukizi ya Covid. Kaa chini jifunze kwanza kusoma na kuandika.
Muda mwingine ni simu tuu hizi tembea uone ukibaki umejifungia bandani utabaki kubisha tuu...
 
Muda mwingine ni simu tuu hizi tembea uone ukibaki umejifungia bandani utabaki kubisha tuu...
Sijajifungia bandani, nimetembea tembea duniani. Sijafika kote lakini viwanja tajiri kuliko vyote duniani nimefika, nikaona.

Ukiwa hujui kuandika na kusoma unaishia kufanya ulinzi kwenye ma saiti ya ujenzi, wanakupa filimbi na tochi, usiku baridi na giza, mchana kelele na vumbi. Pesa yake ni ya mkono uende kinywani.

Tuwekeze kwenye kusoma. "Mkulugenzi" wa wizara ya afya akiona mlalamikaji mwenyewe hajui kusoma na kuandika hawezi kukuchukulia kwa uzito.
 
Watanzania hatufatilii habari za muhimu sisi ni umbea tu.

Maabara ya Taifa walitoa tangazo tarehe 26 February kuwa kuanzia tarehe 1 march hawaruhusu watu kwenda kupima pale, walitoa orodha ya hospital.
Hospital zote za mikoa na rufaa na baadhi za private kubwa,

Hii ilitangazwa kwenye vyombo vya habari.
 
Wanataka watu wasipime ili kuokoa maisha yao! Hii serikali ni ya wananchi kweli?
 
Kwa wageni ni 180$
Yaani hii nchi inaongozwa na washamba.
They dont care! They are not there to entertain anyone.
Wanapiga kote kote
Wizi wizi, any loophole wanapiga, any chance wanapiga.

Wanajenga hotel chato
 
Na bado ukifikia aiport unachajiwa 57,500 tena wanataka cash
 
Mimi nadhan hizo gharama ziliwekwa ili ku discourage upimaji wa corona.
 
Kwako waziri wetu wa Afya Dr. Gwajima.

Sijajua sababu ilofanya hadi muweke bei ghari hivyo kuoata hichi kipimo kwa wanaosafiri, kipimo ni 235,000 Tsh. (100 USD) , hii sio sawa kiukweli mnatuumiza sana sisi wa vipato vya chini ambao tunapata visafari vya dharula katika kutafuta maisha, huu ni unyonyaji, mala ya mwisho ilikua ni elf 40 kupima na ilikuwa very fair, sijajua why mmefanya kiwe ghari, alafu kibaya zaidi hamuweki taarifa wazi, yani mtu hadi uende maabara ya Taifa ndo unaambiwa.

Haya pili kumbe mmehamishia upimaji wa Covid kwenye Hospitali zingine na maabara ya taifa imebakiza kupokea samouli tu, lakini hakuna taarifa zozote kwa umma (unless sikuona mimi) ila nilikuta watu wengi wanaenda mabara ya Taifa wanaishia getini wanaambiwa sasa hivi hawapimi. Mnatukosea jamani, yani Wizara ya afya mambo mengi hayako wazi na yaliyoko wazi hayako sahihi, huku mnasema hivi mtu akienda hospitalini au taasisi zilizo chini ya wizara anakuta mambo tofauti, hii sio sawa kabisa.

Waziri Gwajima wewe ndo waziri wa sasa na unajitahidi sana lakini hili la kipimo cha Covid hapana jamani msifanye kama ndio kitegauchumi mtakua mnatuumiza, sio kila anaeenda nnje ya nchi ana uwezo, wengine ni waganga njaa tu, au hata wale tunaosafiri East Africa basi mngeangalia upya bei za kupima, kaeni na wadau muone mnatusaidiaje wananchi wenu.

Hapa nimeandika kwa hudhuni sanan sababu nahisi nakosa interview yangu ya kazi sababu sina uwezo na nimepata kazi Uganda huko na natakiwa nisafiri, nimejichanga kwa ndugu jamaa na marafiki ila la Covid nimeshindwa na sijui nafanyaje manake nimeenda hadi Maabara ya Taifa kupeleka ombi langu nisaidiw nipimwe ili niwahi kazi wamekataa wanasema kipimo hakina exemption , [emoji24][emoji24][emoji24] Kama mkulugenzi upo humu unisikie , hii sio sawa jamani. Nakosa hata cha kuandika sababu nimeghafirika na sijui la kufanya, yani budget yangu nzima ya kwenda na kurudi na kuishi huko ndio bei ya kupima Covid....

Mkuu nchi gani inapima bure kwa certificate ya kusafiria. Mara ya mwisho kwenda Tz. Nilipimwa kwa euro 130 private. Kusafiri nje ni private na kurudi ndo nikapimwa kwa 40 .

Huku nje Antigen ya kukatia mitaa huku huku ni bure. Ila hii Antigen haikubariki kwenye ndege nyingi. PCR Sawa. Na Ni ghali. Inawezekana kuwa Tz hawapti bure kwa kuwa wako nje ya maelekezo ya WHO so inakuwa issue kidogo Lakini pia shukuru kwamba kipo. Kipindi kile 40 Elfu. Aghakan ilikuwa US D 150.

All in all, tuwe wa Kweli. Utaenda nje na huna uwezo wa dollars 100 kwa ajili ya uzima wako na wa wengine. Utawezaje kumudu bima za afya ambayo hiyo itakuwa kwa mwezi na lazima. Watanzania mmezidi sana kulalamika na wepesi sana kuhonga hela na kutumia kwa mambo yasiyo na tija.

Kama wanapata bure, Sijui. Mana hata hizi antigentest hapa ulaya kuna mahali wanatozwa euro 35-50. Ukiwa mfano Munich Bahnhof Ni bure tu. That’s Antigentest.
 
Mkurugenzi. Sio mkulugenzi

Mara ya mwisho. Sio mala ya mwisho

Huzuni. Sio hudhuni.

Dharura. Sio dharula.

Halafu. Sio alafu.

Bora usiende kwenye huo usaili, ungepoteza nauli na tozo ya kipimo. Hujui kuandika Kiswahili, utaweza nini, kupikia chai maofisa?
Ww mwnye kujua kiswahili kimekiwezesha hata kwenda Malawi??

Sent from my CPH1909 using JamiiForums mobile app
 
Mkurugenzi. Sio mkulugenzi

Mara ya mwisho. Sio mala ya mwisho

Huzuni. Sio hudhuni.

Dharura. Sio dharula.

Halafu. Sio alafu.

Bora usiende kwenye huo usaili, ungepoteza nauli na tozo ya kipimo. Hujui kuandika Kiswahili, utaweza nini, kupikia chai maofisa?
Mkuu ulishiriki kupanga bei ya kipimo nn?maana unaonekana kujawa na chuki bila sababu ya msingi juu ya Mtanzania mwenzio sio poa roho za kichawi hizo ndio nyie mnaolifikisha kwenye hali hizi Taifa letu kwa roho mbaya jitahidi kuficha uchawi wako bwa mdogo
 
Mm hua natamani sana kua na viongozi wanao angalia hali haliasi ya wananchi.Huku mtaani hali ni mbaya sana ukisema watakuambia ww mpiga dili wakati watu wanapambana hasa .Sio huko tu hapa na mama mjamzito hizo gharama kila akiambiwa mavipimo mpaka najiuliza hivi sisi tuna mali asili kibao na zinachimbwa ,vivutio kibao na vinaingiza pesa ambayo ingepunguza gharama ktk baadhi ya vitu.Ukienda tu hapo zambia vitu ni bei chee sana na hawana bandari.Kuna tatizo kubwa sana ktk watunga sera zetu.
 
Yani ni biashara kabisa hii, tena anaeifanya anataka apate faida mala dufu wakati ni taasisi ya serikali
Wewe umeona kipimo cha covid tuu?. So bora huko nje ya nchi unaweza kuamua kuacha kusafiri. Fikiria ukandamizaji unaofanywa makusudi kabisa na askari wa usalama bara bara ni waliopewa zile Pos. Usilogwe utoke na Suzuki carry yako nyumbani. Traffiki anasama amepewa malengo lazima yatimie. Kwa kubambika makosa au kwa kufuata sheria. Sasa sijui Taasisi ya TRA yenye jukumu la kukusanya kwa mujibu wa nahitaji ya bajeti ya taifa wanakusanya na kuvuka malengo hizi zinazotokana na makusanyo haramu zina pelekwa wapi. Mungu atusaijie tuu siku ya judgment inakuja na hakika kila mtu atalipwa kwa Bali tena hapa hapa duniani.
 
Back
Top Bottom