#COVID19 Wizara ya Afya hamtutendei haki, kipimo cha COVID19 ni ghali sana

#COVID19 Wizara ya Afya hamtutendei haki, kipimo cha COVID19 ni ghali sana

Mkuu nchi gani inapima bure kwa certificate ya kusafiria. Mara ya mwisho kwenda Tz. Nilipimwa kwa euro 130 private. Kusafiri nje ni private na kurudi ndo nikapimwa kwa 40 .

Huku nje Antigen ya kukatia mitaa huku huku ni bure. Ila hii Antigen haikubariki kwenye ndege nyingi. PCR Sawa. Na Ni ghali. Inawezekana kuwa Tz hawapti bure kwa kuwa wako nje ya maelekezo ya WHO so inakuwa issue kidogo Lakini pia shukuru kwamba kipo. Kipindi kile 40 Elfu. Aghakan ilikuwa US D 150.

All in all, tuwe wa Kweli. Utaenda nje na huna uwezo wa dollars 100 kwa ajili ya uzima wako na wa wengine. Utawezaje kumudu bima za afya ambayo hiyo itakuwa kwa mwezi na lazima. Watanzania mmezidi sana kulalamika na wepesi sana kuhonga hela na kutumia kwa mambo yasiyo na tija.

Kama wanapata bure, Sijui. Mana hata hizi antigentest hapa ulaya kuna mahali wanatozwa euro 35-50. Ukiwa mfano Munich Bahnhof Ni bure tu. That’s Antigentest.
Mkuu hakuna pahala nimesema nnje wanapima bure hapana, ila nimecompare na nnchi chache mfano Kenya, is more cheaper than hapa kwetu, Uganda pia, na hata ukicheck taarfifa za nnchi nyingi Africa ni rahisi sana sana sawa na bure.

Second; Sio kila aneenda nnje pia anaenda kuishi moja kwa moja, watu wengine kila mwezi au baada ya wiki mbili wanaenda kufunga mzigo wa biashara Uganda au Kenya wanarudi, hawahitaji hata hizo bima za huko nnje, sasa fikilia mfanya biashara huyu awe analipa USD 100 katika kila safari,manake certificate inaexpire after 14 days, sasa hapo huoni kama ni kuumiza wafanyabiashara wadogo, pia wale watu wa mishe mishe za hapa na pele mala leo yupo Kisumu mala yupo Bunjumbula mala wapi inawaumiza pia.

Third; nabaki pale pale, sio kila anaeenda nnje ana uwezo, watu hujitahidi kupata angalau kidogo ya kuwawezesha kwenda nnje kufanya mambo yao mbali mbali katika utaftaji, na pia safari za ghafla kama misiba, fursa nakadharika, sasa hawa watu ambao wanakua hawana uwezo kifedha, ukizidi kuwaongezea tena gharama namna hiyo ni kuumiza raia.

PIA SIO SAWA KUFANINISHA NCHI ZA AMBAZO UCHUMI WA WATU WAKE NI MKUBWA NA NCHI KAMA ZETU ZA KIAFRIKA, NDIO SABABU MIMI SIKUTAKA KUCOMPARE NA HUKO ULAYA, NILICOMPARE NA HAPA HAPA AFRICA.
Sababu hiyo Euro 35 -50 unazoziongelea, is just nothing kwa huko na ukimuuliza mtu atakwambia very cheap, ila ukiicomvert kwa pesa zetu za madafu ni nyingi, hasa ukuzingatia vipato vya wananchi walio wengi, hiyo USD 150 pia kwa huko bado ni cheap, ila ukiibadilisha kwa haya madafu utaona kwamba ni nyingi sana.
 
Back
Top Bottom