Wizara ya Afya, mnawaachiaje watu wenye dalili ya Corona waendelee na shughuli zao?

Wee tulia watu wafanye kazi zao , usiwafundishe kazi kama kufa utakufa tu kelele za nini.
Wewe huko kazini kwako nani anakuingiliaga maamuzi???
 
Tume survive Ebola, Nzige....nina imani hata hili litapita.
Mtanzania ukigundulika na huo ugonjwa walai madaktari wanakuzika ukiwa hai useendelee kuueneza
 

Attachments

  • Abstract.PNG
    35 KB · Views: 1
Missile of the Nation,
aliyekuambia jitihada za wizara ya afya ndio vinaifanya tanzania kuwa salama pasi na milipuko ya magonjwa kama ebola na corona ni nani vile! Mungu asipoulinda mji walinzi hukesha bure! Tz tupo salama kwa kuwa Mungu ndie atulindaye! Siyo huyu waziri Ummy na jamaa zake!
 
ilipaswa Ummy (wizara) ifanye juhudi za makusudi kudhibiti hao wageni (quarantine)


badala yake anafanya juhudi za makusudi kuwaruhusu na kuwaacha waende na wakazagae huko mtaani..


''...ee Mola tuokoe na hiki kiama" hard blasters

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ummy Mwalimu amepiga sheria pale UDSM akafanya masters ya sheria kule Pretoria South Africa.Naibu waziri Dr.Faustine Ndungulie yeye ndio Medical Doctor(MD) na MPH,waziri hatoi maamuzi peke yake anajadiliana na makamu wake.

Kuwa waziri hakuitaji huwe mtaaram wa sekta uliyopewa,japo sijawahi kuwa waziri ila natamani sana hicho cheo .
 
Ni heri ithibitike kuwa ipo ili watu waanze kutumia akili. Rais mzima anasema hata usiku msipigane mabusu na patakuwa na raha tu halafu anasema eti tunapambana na corona? Naona sasa wana show zao za kusalimiana kwa miguu!
kama hukumuelewa rais usikurupuke kumbeza!
 
Basi washauri wa huyo waziri hawako makini. Au na yeye hashauriki kama mzee baba?
 
Missile of the Nation, Serikali yetu ni dhaifu sana katika mambo mengi. Yawezekana hawana weledi, lakini kinashangaza ni kuwa wanakosa hata ile intelligent reasoning.

Wanakosa ubunifu lakini wanashindwa hata kutazamia na kucopy. Inashangaza sana!!
 
Basi washauri wa huyo waziri hawako makini. Au na yeye hashauriki kama mzee baba?
Makamu ndio anamshauri waziri na ndiye mtaaramu kwenye hiyo sekta,yeye ndio kasomea udktari wa binadamu na afya ya jamii sasa unasemaje kwamba hamshauri vizuri au unakitaka cheo cha unaibu huwe mshauri wa waziri???
 
huyu bi dada wanam-0713!
Ila uzuri mmoja huu ugonjwa hauchagui, uwe tajiri;/masikini, msafi/mchafu, waziri/layman etc!

So waendelee kufanya mzaha na afya za watanzania, na kama hayo ndo maelekezo alopewa ayaropoke.
Uingie tu nchini, pengine utatusaidia kupunguza wafuasi wa mbogamboga za kijani maana wamezidi kumsifu "MASIHA",

Pengine pia unaweza ukapenya pale nyumba kubwa na masiha akaupata angalau turelax, tushachoka
 
Makamu ndio anamshauri waziri na ndiye mtaaramu kwenye hiyo sekta,yeye ndio kasomea udktari wa binadamu na afya ya jamii sasa unasemaje kwamba hamshauri vizuri au unakitaka cheo cha unaibu huwe mshauri wa waziri???
Soma mada ya mleta uzi kisha soma comment yangu.
 
Jmn si wamewafanyia uchunguzi wakagundulika hawana. Tatizo liko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Fuatilia uelewe huo ugonjwa.

Vipimo pekee havitoshi kuthibitisha kuwa mtu hana corona. Vipimo, dalili, historia yake - vyote kwa pamoja vinasaidia kumwelewa aliyeambukizwa.

Huko ulikoanzia, wanasema kuwa kuna wagonjwa wa corona ambao vipimo vinaonesha negative, lakini wanao. Taarifa za karibuni kabisa zinasema kuwa wamegundua hata wagonjwa waliotibiwa, ikaaminika wamepona, wakaruhusiwa, lakini baadhi bado wameinekana wana uwezo wa kuambukiza.

Mengi hayajafamika kuhusu huu ugonjwa. Mapya yanazidi kugundulika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…