Nimesikitishwa sana kuona leo watoto wa shule ya msingi "serikali" wakirudi kutoka shuleni wakiwa wamedhoofika sana, miili ikiwa dhaifu na macho mekundu kabisa.
Nilipowauliza, walisema wamepewa dawa shuleni na kumeza bila kula. Dawa hizo wamesema ni za kichocho na minyoo, na wamepewa pasipo wazazi kuarifiwa wala kuulizwa ridhaa yao.
Walimu nao wameeleza kuwa walipewa taarifa ghafla kwa njia ya simu kwamba waandae watoto kumeza dawa hizo.
Najiuliza, shuleni wana lengo la kuua watoto au kuna shida gani? Je, shule za msingi za serikali zimegeuzwa kuwa sehemu za majaribio ya dawa kwa watoto? Kila mzazi ana utaratibu wake wa kutibu watoto wake. Kwa nini watoto wanalazimishwa kumeza dawa bila taarifa kwa mzazi?
Mnawapa dawa za kichocho na minyoo, lakini mnajuaje kama tayari wazazi wao wamewapa dawa nyumbani?
Lengo la kupeleka mtoto shuleni ni kujifunza na kusoma, si kumeza dawa. Wanapata wapi ujasiri wa kuwamezesha watoto dawa kinyemela pasi na ridhaa ya wazazi? Serikali yangu inasikitisha sana kwa matendo haya.