Wizara ya Afya na Elimu: Kwanini Watoto wa shule ya msingi wamemezeshwa dawa pasipo mzazi kupewa taarifa?

mimi huku nilipo ,hizo dawa walipewa juma moja lilipita , jambo moja muhimu watoto waliambiwa wabebe chakula na wale ambao hawakubeba walirudishwa nyumbani wakabebe chakula kabla ya kupewa dawa.
afadhali huko
 
KUTOA YAARIFA NI MUHIMU Taarifa muhimu,mzazi/mlezi ana haki ya kupewa taarifa ya kina na ana haki ya kufanya maamuzi ya kukataa au kukubali.
Hata mimi mwanangu karudi shule anasema leo tumepewa dawa ??? yeye mwwnyewe hajui ni dawa gani?sisi hatujui ni dawa gani?amepewa kwa ajili gani?faida na hasara zake ni zipi?
Miili ya binadamu inatifautiana kuna wengine miili yao ina hypersensitivity aleji na dawa ,unaweza ukampa mtoto wa mtu dawa akaungua mwili au akaanguka au akapata madhara ...ndio utakuja kusema nilikuwa nampa dawa?dawa gani?ulipata ruhusa idhini ya wazazi?alikuwa anaumwa nini?wewe ni daktari una leseni ya kutoa huduma ya matibabu?umesomea?je shuleni ni sehemu sahihi ya kutolea dawa ?akipata dharura ya haraka ? hali ikibadilika kutokana na madhara ya dawa hapo shuleni kuna huduma za dharura ?kuna wataalamu na miundombinu ya kutosha??DAWA ni potential poison dawa ni sumu..unatoaji kiholela sehemu yoyote na mtu yeyote kama pipi? hapo ni hospitali au shuleni??walimu tumewapa dhamana ya kukaaa na watoto sio wajichukulie sheria mikononi ya kuwafanya wanavyotaka bila kutushirikisha wazazi,SIO SAHIHI.
 
Hii nchi imeisha uzwa hao walio nanunuwa wanatumia serikali kuhakikisha watu weusi wanaisha taratibu. Haiwezekani dawa zenye kusudi njema zitolewe bila kuhusisha wazazi. Kama wanapenda watoto mbona hawapi Bima ya afya bure ili wawe wanafanya check up mara mbili kwa mwaka kama nchi nyingine?
 
Unaleta hoja utadhani ni jambo geni, toka miaka 90 huko tumekunywa sana dawa shuleni
 
wanalengo gani hasa? wameshindwa kuwapa elimu nzuri watoto...wameanza kuwanywesha dawa!!..tena kimya kimya?....wazazi wataamini vipi kama hizo dawa ni za minyoo na kichocho?, kwakuwa watoto hawana maamuzi basi wanawapa tu dawa bila mzazi kuhusishwa?
Kweli hapo wamechemka mazima. Halafu wanajitetea eti ni Taarifa ya ghafla tena kwa simu. Haya ni majibu ya kikatili kwani Hiyo ghafla imetokea wapi? Kwani hizo dawa haziwezi kuhifadhiwa wakati utaratibu wa kutoa Taarifa kwa wazazi/walezi ukifanyika? Inashangaza bado waTz tunafanya kazi kwakukurupuka hadi kwenye mambo yanayohusisha Uhai na mustakabali wa Afya ya Jamii.
 
Hilo kundi kubwa la watoto umelikuta wapi wewe peke yako tu ndiyo waone wengine wasiwaone?
Na kama walilegea hadi macho kuwa mekundu ulitumia kipimo gan au taaluma gani kubaini hadi dawa waliyopewa ndiyo zimesababisha hali hiyo?
Serikali ndiyo mzazi wa kwanza je hizo taarifa kuwa wazazi hawajapewa taarifa umepata kwa wazazi wapi?
 
Miezi iliyopita wazungu walikuwa wanagawa biscuit kwa watoto wa kike huko mbeya, cha kushangaza ni watoto wa kike tu ndio walikuwa wanapewa hizo biscuit
 
Zama zimebadilika sana, kuna shule kila mara wanapotoa hizo dawa watoto huishiwa nguvu na kuanguka. Utapiamlo ni shida!
 
ndugu tuna watoto na tunawachunga kila wakati, na tunatambua mtoto asipokuwa sawa. yaani mwanangu aende shule mzima arudi hoi alafu uniambie maneno yako..ungekuwa karibu ningekupa bakora tuheshimiane kidogo mkuu
 
viongozi wetu hawa naona maarifa hakuna kabisa, nakumbuka sisi zamani tulikuwa tunapewa madaftari peni rula mikebe kutoka shuleni, siku hizi wapo bize kuwaywesha dawa kama shule zimegeuka hospitali sasa. Hata taarifa kwa wazazi hawatoi..hovyo sana yaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…