KERO Wizara ya Afya na NACTVET zishughulikie matokeo yetu ya diploma kwa haraka ili yafikishwe Vyuoni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya vyuo vimefunguliwa tangu tarehe 19, na wanafunzi wanatakiwa kuripoti chuoni ili kuanza muhula mpya wa masomo. Hata hivyo, changamoto inayotukabili ni kwamba hatujapokea matokeo yetu, huku kuripoti chuoni kukihitaji kulipa ada na kujiandaa kwa mahitaji mengine ya masomo.

Tunapouliza vyuoni kuhusu matokeo, tunaelezwa kuwa bado hayajawasilishwa. Hali hii inatupa wakati mgumu katika kupanga na kujiandaa kwa muhula mpya, hasa kwa wanafunzi ambao huenda wakahitaji kufanya mitihani ya marudio (supplementary examinations).

Kwa kawaida, mitihani hiyo hufanyika muda mfupi baada ya vyuo kufunguliwa na huhusisha gharama za ziada ambazo wanafunzi wanapaswa kujiandaa nazo mapema. Kuchelewa kwa matokeo kunafanya iwe vigumu kupanga bajeti na kujiandaa kwa wakati.

Hivyo, tunaomba Wizara ya Afya na NACTVET zishughulikie suala hili kwa haraka ili matokeo ya wanafunzi wa vyuo vya afya katika ngazi ya diploma yatolewe na kufikishwa vyuoni kwa wakati.

Kutolewa kwa matokeo mapema kutatusaidia kupanga gharama za masomo, kujiandaa na mitihani ya marudio pale inapohitajika, pamoja na kuanza muhula mpya bila usumbufu usio wa lazima.

Tunaomba suala hili lipewe kipaumbele kwa maslahi ya wanafunzi na maendeleo ya elimu ya afya nchini.
 
Hii issue imekua deep sasa aisee
 
Back
Top Bottom