Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Kwanini NHIF wanaendelea kuondoa baadhi ya DAWA? Shida ni nini ?
Salaam Ntwale.

Tunashukuru sana kwa swali lako. Tunaomba utambue kuwa hakuna dawa iliyoondolewa katika huduma ya NHIF katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika ngazi zote. Niwaombe tu, ikitokea wewe au mwanachama yeyote amepata au kukutana na changamoto yoyote juu ya huduma zitolewazo na NHIF tunaomba sana awasiliane nasi tuweze kumsaidia.

Tafadhali sana, utupigie tu kwa namba 0800110063. Tumeboresha Afya Nchini, na kazi inaendelea kuwasogezea zaidi huduma wananchi karibu na maeneo yao wanayoishi.

Aksante.
 
Salaam Musa.

Tunashukuru kwa swali lako.
Mara nafasi zitakapopatikana na kuridhiwa kwa ajira tutatangaza kama utaratibu wa Serikali ulivyo.

Aksante.
 
Salaam Marxlups.

Tunashukuru kwa hoja zako, tumepokea na tunazifanyia kazi.

Aksante.
 
Wizara ya afya mnampango gani wa kuwaajiri vijana waliokua wameajiriwa na benjamin mkapa foundation katika utumishi wa umma hasa ukizingatia kua mikataba yao na taasisi ya Benjaminmkapa imeisha na watu walipangwa mikoa tofaut na makazi ya kwao?

Asante
 
Hizi Bima za afya mziangalie upya zina shidackidogo, ukienda hoapitali unaambiwa, pima baada ya hapo, ugonjwavukishajulikana ,unaambiwa dawavhakuna .

Ukanunue hasa hospitalivya Makole-Dodoma, wachunguzeni kwa ninibhawana dawa,? Serikali yote ipo hapa na wizara ni dharau, makusudi, kiburi, uzembe, nadhani kuna tatizo.!
 
Salaam Oswald.
Tunashukuru, tumelipokea tutafuatilia na NHIF watalifanyia kazi kujua changamoto au tatizo ni nini.
Aksante sana.
 
Kinga ipo na inafanya kazi kwa nguvu sana kupita kitengo cha Environmental health Sciences.
Watu wa maendeleo ya jamii msiingilie kazi ambazo tayari zina wataalamu ambao ni maafisa afya..walio somea public health protection and promotion.

#MaendeleoHayanaChama
 
Naomba kuuliza hili suala lilo trend kwenye akaunti ya kigogo..kuhusu hali ya uchafu uliokithri katika hostel za Nursing chuoni hapo je?wizara imechukua hatua gani mpaka hibi sasa..ili kuweza kulinda afya za wanafunzi hao na kuepusha ueneaji wa magojwa ya mlipuko kama kipindupindu n.k

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizi Bima za afya mziangalie upya zina shidackidogo,ukienda hoapitali unaambiwa,pima baada ya hapo,ugonjwavukishajulikana ,unaambiwa dawavhakuna .Ukanunue hasa hospitalivya Makole-Dodoma,wachunguzeni kwa ninibhawana dawa,?Serikali yote ipo hapa na wizara ni dharau,makusudi,kiburi,uzembe,nadhani kuna tatizo.!
Haya mzee baba utoe ushirikiano sasa
Oswald Daudi Mwakibete

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Nhif nana zingine pia sio hizo tuu kama ni muhusika nenda kapime uone kama utapewa dawa sio majungu ndo ukweli
 
Unapoint lakini nadhani hujaiweka kwenye usahihi,nadhani bima hapo hazina matatizo ila pia nadhani ungeuliza inatokeaje kuwa na bima halafu unaambiwa dawa hakuna?tatizo hapo litakua ni dawa wala sio bima na hilo tatzo sio kwako tu ni kwa sehemu kubwa hasa zinapotumika bima za iCHF ndio mambo hayo hutokea.
 
Niko sawa mkuu,maana kila nikienda na hiyo bima naambiwa hakuna dawa,lakini nikiwa na pesa bila bima sipati shida,hivyo hisia zangu lazima ziniaminishe kwamba shida ni Bima!au wewe ungelionaje hilo?
 
Safi sana wizara ya afya kwa kupanua wigo wa kupata maoni.

Mie naishauri wizara izikusanye ilani hasa vyama vya upinzani iyapitie maelezo yao kuhusu eneo la kuboresha sekta ya afya na iyachukuwe mawazo yao na kuyafanyia kazi, nina imani yatakuwa na mchango mkubwa sana katika kuboresha sekta hiyo, isipokuwa wakati wa kuyachukua usimwambie yeyote kuwa umeyachukuwa toka Ilani ya CHADEMA, ACT au ADC etc.

Maana nasema hivyo maana kuna watu wana aleji na upinzani wakati hata serikali yenyewe inatekeleza sera za kutoka huko!
 
Kupima Corona shs ngapi kwa sasa?
Na mimi nina swali hilo hilo. Ni dhahiri corona sasa imekuwa kitega uchumi.

Nilikwenda Aghakan tarehe 15 Januari 2021 kupima. Wanakuambia ulipe Tsh 360,000 (au kiasi hicho kwa fedha ya kigeni) na baada ya malipo ndipo wanachukua sampuli za kwenda kupima.

Majibu baada ya saa 48. Serikali nayo imepandisha kutoka US$50 hadi US$100. Jee, ni kitu gani kilichofanya gharama iongezeke mara mbili kama nyenzo zinazotumika kupima ni zile zile?
 
Niko sawa mkuu,maana kila nikienda na hiyo bima naambiwa hakuna dawa,lakini nikiwa na pesa bila bima sipati shida,hivyo hisia zangu lazima ziniaminishe kwamba shida ni Bima!au wewe ungelionaje hilo?

Hapo chief umeongea point husika, yaan ukiwa na bima no services lakini pt user fee services available hapo directly tunatupia lawama kwenye bima, labda nikufafanulie kidogo,unajua hizi bima zote zinakua na kelele kwa sababu zifuatazo;watoa huduma wanatoa huduma hzo but malipo yao stahiki hayatolewi kwa wakati na isitoshe kunavikwazo vingi sana, sambamba na yote hayo unakuta kituo hakipokei dawa za kutosha na unaambiwa dawa hzo ziwerelvolved sasa unarevolve nn wakati unachotoa sio sawa na unacholipwa,nadhan hlo ni tatzo linalisababisha kuwepo ugumu.

nadhan wizara inahaja ya kuliangalia suala hli la bima na kuondoa vikwazo vingi vilivyopo ili kulipa vituo vinavyofanya claims za NHIF NA ICHF ili huduma ziendelee kuwa nzuri.
 
Umenufumbua macho!Mbaya zaidi wanasiasa wanatuhamasisha tuwaambie na wengine!Utafanyeje promotion ambayo huwezi kuitetea?
 
Wizara ya afya tunaomba mtoe tamko rasmi. Tanzania ugonjwa wa corona upo au hamna?
Kukaa kwenu kimya mnawapa nafasi watu wengine wasiohusika wazidi kuwaletea wananchi taharuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…