Wizara ya Afya: Tutafunga kila mtu kwa wizi wa dawa

Wizara ya Afya: Tutafunga kila mtu kwa wizi wa dawa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amesema kama wataamua kuwachukulia hatua watumishi wanaojihusisha na wizi wa dawa watawafunga watumishi wote.

Amesema hayo alipokuwa katika hospitali ya Mount Meru ambapo amesema kiwango cha dawa kinachoingia sio sawa na kinachonunuliwa.

Wakati anazungumza na watumishi wa Hospitali ya Mount Meru aliwauliza kama alete ushahidi wa dawa kuibwa Hospitalini hapo ambapo walimuomba asilete ushahidi kwa wakati huu.

Amesema watumishi hao wanaharibu taswira ya watumishi wote wa sekta ya afya kuonekana ni wezi wa dawa na kuwaonya kuwa watumishi hao watafungwa kwa wizi wa dawa.
 
"wapigaji" wa dawa za serikali/wananchi acheni tabia hiyo badilikeni vinginevyo kipindi hiki mtaishia jela, waziri huyu hatanii.
 
Kuna mwamba mmoja ni daktari Muhimbili ana Hosp yake ni kubwa na inahuduma zote na hadi machine ambazo huwezi kuzikuta kwenye dispensary za serikali.
 
Waziri wangu rekebisha kauli yako SIO utawafunga wote kisheria wewe huna mamlaka hayo,mamlaka ya kuhukumu yapo chini ya COURT,wewe uwezo wako ni kufungua mashitaka polisi.

Na polisi watachunguza ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidi then wanashauriana na prosecutors kuona kama wana winnable case,always waziri wangu fanya kazi zako kwa mujibu wa sheria, hili la kuwekana ndani ni kinyume cha sheria na elewa hauna hatia mpaka ukutwe na hatia na mahakama!.
 
Anawaomba wamruhusu alete ushahidi, sidhani km alikuwa siriaz na amedhamiria kumaliza tatizo.
 
Waziri wangu rekebisha kauli yako SIO utawafunga wote kisheria wewe huna mamlaka hayo,mamlaka ya kuhukumu yapo chini ya COURT,wewe uwezo wako ni kufungua mashitaka polisi.

Na polisi watachunguza ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidi then wanashauriana na prosecutors kuona kama wana winnable case,always waziri wangu fanya kazi zako kwa mujibu wa sheria, hili la kuwekana ndani ni kinyume cha sheria na elewa hauna hatia mpaka ukutwe na hatia na mahakama!.
Hujaelewa Nini wewe? Waziri kasema watawafunga wote wanaojihusisha na wizi wa dawa. Sasa wewe kaibe halafu useme waziri Hana uwezo wa kusema wezi wa dawa watafungwa.
 
Back
Top Bottom