Wizara ya Afya: Wasafiri watapimwa covid19 kwa dola 100

Wizara ya Afya: Wasafiri watapimwa covid19 kwa dola 100

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetoa muongozo mpya wa upimaji kwa wanaosafiri kwenda nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanaoambukizwa #COVID19 na kuwepo kwa vimelea vipya kwa baadhi ya nchi

Wizara imetangaza kupanda kwa gharama za upimaji wakisema kuwa zimechangiwa na ongezeko la wasafiri wanaokwenda nje ya nchi na mabadiliko ya teknolojia ya upimaji ambapo baadhi ya vipimo vimeongezeka

Muongozo unataka msafiri aelimishwe siku tano kabla ya siku ya Safari. Aidha vyeti vya kielektroniki vya COVID19 vitatolewa kwa waliothibitika kutokuwa na maambukizi na vitadumu kwa siku 14 au kutegemea na nchi ambayo msafiri anakwenda

Majibu yatatolewa ndani ya saa 48 kabla ya safari kwa watu wa nje ya Dar na ndani ya saa 24 kwa walioko mkoa wa Dar. Gharama za Vipimo ni USD 100 sawa na Takriban Tsh 230,000 ambapo malipo yatalipwa katika akaunti ya Serikali
1609959672015.png

1609959685809.png
 
Wanajua bila certificate huvuki boda. Piga picha watu 1000 kila siku kwa siku 30
 
Si walishasema hakuna COVID-19.
Nini dola 100. Kipimo hiki hakitakiwi kuwa zaidi ya TSh. Elfu 40 sawa na dola 18 kwenda 20.
Duuh mapato ya kulazimisha.
 
No sasa yatosha. Yafaa tusimame kwa umoja kupinga hili. Baada ya serikali kusaidia kupunguza ugonjwa wao wanataka hela
 
Sisi HATUNA korona. Ya nini kupima korona tena?Sisi ni taifa huru.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetoa muongozo mpya wa upimaji kwa wanaosafiri kwenda nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanaoambukizwa #COVID19 na kuwepo kwa vimelea vipya kwa baadhi ya nchi

Wizara imetangaza kupanda kwa gharama za upimaji wakisema kuwa zimechangiwa na ongezeko la wasafiri wanaokwenda nje ya nchi na mabadiliko ya teknolojia ya upimaji ambapo baadhi ya vipimo vimeongezeka

Muongozo unataka msafiri aelimishwe siku tano kabla ya siku ya Safari. Aidha vyeti vya kielektroniki vya COVID19 vitatolewa kwa waliothibitika kutokuwa na maambukizi na vitadumu kwa siku 14 au kutegemea na nchi ambayo msafiri anakwenda

Majibu yatatolewa ndani ya saa 48 kabla ya safari kwa watu wa nje ya Dar na ndani ya saa 24 kwa walioko mkoa wa Dar. Gharama za Vipimo ni USD 100 sawa na Takriban Tsh 230,000 ambapo malipo yatalipwa katika akaunti ya Serikali
View attachment 1670245
View attachment 1670246
 
Jamaa makatili hayo sijapata kuona....hayana tofauti na majambazi unawaumiza watu wako kienyeji watu wanaosafiri wengi wanaleta Mali ndani ya nchi unawaongezea gharama tena za safari badala ya kupunguza au kutoa gharama maana pesa mnapata za covid 19 ninyi ndio mnaongeza utadhani hamjawahi chukua msaada wa covid yaani kila siku ninyi ni kuongeza vipengele tuu Kama Zimbabwe tambueni Kuna corona dunia yote imeathirika sio kila kukicha kufikiria vyanyo vya ajabu ajabu wakati Kuna mdororo wa uchumi duniani...
 
Kumbe wizara inafuatilia yanayoendelea huko Duniani nilifikiri hawana habari na kugundulika kirus kipya chenye uwezo wa kumuangusha hadi Jiwe
 
Watalii, waja kwa mikutano.. walipie visa.. waje.. waondoke kwa gharama ingine kama vile ni ya visa... hata kumukumbu wasinunue zawadi.. kupeleka makwao!!! wawazie kubakiza $100 au hawataondoka nchini!!! nchi jirani wenye kupokea watalii wao vipi huko kiasi cha kupima serikalini? na watu wafanya biashara kwani hata wa kuanza ndio hivi..
 
Watu mnaolalamika kama vile mnasafiri vile huko nje ya nchi [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu mnaolalamika kama vile mnasafiri vile huko nje ya nchi [emoji23][emoji23][emoji23]
wewe ndiye hutoki nje ya mipaka. ni kama vile utakuta watu wanalalamika maisha magumu ilhali wengine kila siku ni sherehe.. hata vidole havilingani
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom