Wizara ya Afya: Wasafiri watapimwa covid19 kwa dola 100

Wizara ya Afya: Wasafiri watapimwa covid19 kwa dola 100

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetoa muongozo mpya wa upimaji kwa wanaosafiri kwenda nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanaoambukizwa #COVID19 na kuwepo kwa vimelea vipya kwa baadhi ya nchi

Wizara imetangaza kupanda kwa gharama za upimaji wakisema kuwa zimechangiwa na ongezeko la wasafiri wanaokwenda nje ya nchi na mabadiliko ya teknolojia ya upimaji ambapo baadhi ya vipimo vimeongezeka

Muongozo unataka msafiri aelimishwe siku tano kabla ya siku ya Safari. Aidha vyeti vya kielektroniki vya COVID19 vitatolewa kwa waliothibitika kutokuwa na maambukizi na vitadumu kwa siku 14 au kutegemea na nchi ambayo msafiri anakwenda

Majibu yatatolewa ndani ya saa 48 kabla ya safari kwa watu wa nje ya Dar na ndani ya saa 24 kwa walioko mkoa wa Dar. Gharama za Vipimo ni USD 100 sawa na Takriban Tsh 230,000 ambapo malipo yatalipwa katika akaunti ya Serikali
View attachment 1670245
View attachment 1670246
Kupima malaria ni shs. 1,000/=, ila Covid19 ni 230,000/=, kweli hii biashara ndio maana imetangazwa kwa gharama kubwa sana kwenye vyombo vya habari, duu
 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetoa muongozo mpya wa upimaji kwa wanaosafiri kwenda nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanaoambukizwa #COVID19 na kuwepo kwa vimelea vipya kwa baadhi ya nchi

Wizara imetangaza kupanda kwa gharama za upimaji wakisema kuwa zimechangiwa na ongezeko la wasafiri wanaokwenda nje ya nchi na mabadiliko ya teknolojia ya upimaji ambapo baadhi ya vipimo vimeongezeka

Muongozo unataka msafiri aelimishwe siku tano kabla ya siku ya Safari. Aidha vyeti vya kielektroniki vya COVID19 vitatolewa kwa waliothibitika kutokuwa na maambukizi na vitadumu kwa siku 14 au kutegemea na nchi ambayo msafiri anakwenda

Majibu yatatolewa ndani ya saa 48 kabla ya safari kwa watu wa nje ya Dar na ndani ya saa 24 kwa walioko mkoa wa Dar. Gharama za Vipimo ni USD 100 sawa na Takriban Tsh 230,000 ambapo malipo yatalipwa katika akaunti ya Serikali
View attachment 1670245
View attachment 1670246
AFYA YAKO FURSA YETU.
 
Wameona covid ndio pakuponea kwa kweli tunaenda mbele hatua 8 na kurudi nyuma hatua 10 huku tunajipongeza!Mh Rais atengue haya maagizo yanayoongeza usumbufu kwa wanyonge
 
Kijana wangu anatamani kwenda kuosha macho huko kwa wazungu kidogo kupanua CV yake, amefika Dar kufuatilia cheti Cha covid 19 anaambiwa kupima ni dola mia moja sawa na laki mbili na nusu kwa mtu mmoja.

Naomba kujua Kama hizi gharama zilizopitishwa toka zamani au ni mpya? Kama gharama ni kubwa kiasi hiki na watu wanatakiwa kusafiri nje pale tu wanapokuwa na covid certificate, je madreva na Watanzania wa kipato Cha chini wanaofanya shughuli zao kwa kuvuka mipaka wataziweza hizi gharama?

Mwenye kuelewa hizi gharama vizuri kwa Tanzania na nje ya Tanzania atusaidie kulinganisha.

Tujadili madhara ya kuwa na gharama kubwa kupima covid 19 na uwezo wa Watanzania kumudu gharama hizi

Tafadhali Beatrice Kamugisha soma

Kijana wangu anatamani kwenda kuosha macho huko kwa wazungu kidogo kupanua CV yake, amefika Dar kufuatilia cheti Cha covid 19 anaambiwa kupima ni dola mia moja sawa na laki mbili na nusu kwa mtu mmoja....
Sasa kama dola 100 ya Covid 19 inamshinda huko kwa wazungu anaenda kuosha macho au kuoshwa macho?
 
Msaada wa hela za covid walizopokea jamaa washaweka kibindoni na kubadili matumizi yake.

Hakuna namna ni kulipia tu.
 
102011131.jpg
 
Back
Top Bottom