Wizara ya Afya: Wasafiri watapimwa covid19 kwa dola 100

Kupima malaria ni shs. 1,000/=, ila Covid19 ni 230,000/=, kweli hii biashara ndio maana imetangazwa kwa gharama kubwa sana kwenye vyombo vya habari, duu
 
AFYA YAKO FURSA YETU.
 
Wameona covid ndio pakuponea kwa kweli tunaenda mbele hatua 8 na kurudi nyuma hatua 10 huku tunajipongeza!Mh Rais atengue haya maagizo yanayoongeza usumbufu kwa wanyonge
 
Kijana wangu anatamani kwenda kuosha macho huko kwa wazungu kidogo kupanua CV yake, amefika Dar kufuatilia cheti Cha covid 19 anaambiwa kupima ni dola mia moja sawa na laki mbili na nusu kwa mtu mmoja.

Naomba kujua Kama hizi gharama zilizopitishwa toka zamani au ni mpya? Kama gharama ni kubwa kiasi hiki na watu wanatakiwa kusafiri nje pale tu wanapokuwa na covid certificate, je madreva na Watanzania wa kipato Cha chini wanaofanya shughuli zao kwa kuvuka mipaka wataziweza hizi gharama?

Mwenye kuelewa hizi gharama vizuri kwa Tanzania na nje ya Tanzania atusaidie kulinganisha.

Tujadili madhara ya kuwa na gharama kubwa kupima covid 19 na uwezo wa Watanzania kumudu gharama hizi


Tafadhali Beatrice Kamugisha soma

 
Kijana wangu anatamani kwenda kuosha macho huko kwa wazungu kidogo kupanua CV yake, amefika Dar kufuatilia cheti Cha covid 19 anaambiwa kupima ni dola mia moja sawa na laki mbili na nusu kwa mtu mmoja....
Sasa kama dola 100 ya Covid 19 inamshinda huko kwa wazungu anaenda kuosha macho au kuoshwa macho?
 
Msaada wa hela za covid walizopokea jamaa washaweka kibindoni na kubadili matumizi yake.

Hakuna namna ni kulipia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…