Sasa maziko yoote kufanyika mchana na ndugu kushirikishwa na
=========
Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeelekeza maafisa Afya na waganga wakuu wa wilaya na mikopa kuhakikisha familia za wafiwa zinashirikishwa kikamilifu na bila hofu na haraka katika kuandaa mazishi ya wapendwa wao
Pia Wizara imewataka raia kutotumia dawa zinazoshauriwa na watu wasio na utaalamu katika masuala ya tba, badala yake wasubiri muongozo kutoka Wizarani. Kwa sababu hakuna dawa ya kutibu au kuzuia #CoronaVirus hadi sasa
-
Dawa zinazotumika na wengi zinatumika kutibu maradhi mengine na sio #CoronaVirus. Hivyo wizara imewataka Baraza la Famasia kusimamia uuzwaji holela wa dawa hizo ambazo zinashauriwa a watu mitandaoni
Wizara imesema haya baada ya kuzuka uvumi mtandaoni kuwa kuna dawa zinatibu #CoronaVirus hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kutumia dawa kiholela hasa dawa za Azithromycin, Aspirin, Prednsolone, Zinc, Ascorbic Acid (Vitamini C) na ARV. Wizara imekanusha, dawa hiz haziwezi kutibu #CoronaVirus
Kuhusu tiba asili/mbadala za mitishamba, wizara imesema itatoa maelezo baada ya kupata ushahidi kamili kutokana na Tafiti zinazoendelea