Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Mpaka hapa wale Team Misukule nimeona wawili tu,na mmoja yeye ni akili zinamrudirudi.

Wana JF waliandika hapa sana na kuleta picha na video,lakini hawa team misukule ilipinga kwamba si TZ,na wengine wakadai ni "photoshoped".

Naangali nani atapongeza huu uamuzi.
 
Nashauri ndugu zao waliozikwa usiku wakafungue kesi ya kudai fidia ya kudhalilisha marehemu.
Kuna watu ni wasanii sana.
 
Kwa mwendo huu endapo mitandao ya kijamii ingezimwa kipindi kile ili tubaki na radio na Television pekee sijui ingekuwaje.
Mie najiuliza mpaka kichwa kinauma!
Mungu ibariki Tanzania na watu wake!
 
Tutarajie ligi kuu soka kurudi dimbani punde, kila kitu ni hadi mkulu aseme.
 
Nadhani kuna mambo mengine ya hovyo yanafanywa na Serikali, wengi tukiamini yamekubaliwa au ni maelekezo ya Rais, kumbe ni maamuzi wa baadhi ya watendaji wenye akili ndogo ndani ya Serikali.

Kuwazika marehemu usiku, kwa kificho, bila kuwashirikisha ndugu, ulikuwa ni uhayawani.

Siamini kama kuna sababu yoyote ya maana inayoweza kueleweka. Mtu amekwishafariki. Mmetoa maelekezo kuwa msiba usihudhuriwe na watu zaidi ya 10, sasa kumzika usiku kuna maana gani? Hao virus nao huwa wanahitaji muda wa kulala, kiasi cha kusema watu wazike wakati virus wamelala usingizi?

Wati wengi tulilalamikia jambo hilo. Lakini majitu majinga kama yule Bia Yetu, yaliendelea kushabikia. Niliwahi kusema pia, mashabiki wajinga kama Bia Yetu, hawana msaada kwa Rais, nchi, Serikali wala CCM.

Tunampongeza Rais kwa kusitisha ule uhayawani wa kuzika watu usiku. Waliopoteza ndugu zao wana majonzi ua kuwapoteza ndugu zao, lakini pia kutokuwa na uhakika kama makaburi waliyoambiwa ndimo ndugu zao wamelala, ndimo kweli walimolala.

Tupunguze tutofautiane kwa fikra katika kuutokomeza ugonjwa huu lakini tusimame pamoja katika lengo kuu la kulitakia mema Taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mwendo wa kunata na beat za jiwe
 
Neno la mkuu ni agizo, hata kama ilikuwa utani... utekelezaji uanze mara moja.
 
Bams,
Mfano watu kupigwa risasi kutekwa Lissu kupigwa risasi etc......gwajiima kupanga ukabila......
Mbona mawaziri husika na rais hakemei mambo machafu yote haya?
 
Tusitumie dawa ambazo hatujashauriwa na wataalam au wizara ya afya, sasa huyu anaehimiza kujifukiza nimuweke kundi lipi?
 
Daby,
Tena hiyo kamati ingefaa zaidi iwe na chembechembe za ujeshi...(Afande Kova na ugaidi)
 
Back
Top Bottom