Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Kumbe kweli walikuwa wanazika usiku?

Sent using Jamii Forums mobile app
Juzi walikanusha hadi misuli ya nanihii ikawasimama, Leo wote wamekubalia na akina Bia yetu kama kawaida watakuja na kushangilia tena
IMG-20200503-WA0060.jpg
 
Master Mind,
Amri or agizo la kuzika watu usiku inaonekana lilitoka kwa beberu moja kwa moja mpaka kwenye vichwa vya wafanyakazi wa serikali.Yaani huwezi niambia wazo lilitoka no where na si wizara au magu aliyejua kuwa watu wanazikwa usiku.Yaani azikwee mtu mmoja hadi kumi na sita ndani ya ardhi ya nchi hii usiku then wizara na rais wasijue.Anyway Mungu anisamehe tu
 
Watu kuzikwa kama wanyama usiku wa manane haikubalikik nakupongeza sana mganga mkuu prof. Abel Makubi na wizara kwa ujumla uwezo wako toka ulipokua bugando ulionekana Hongera sana...

Its not over until its over...
emoji769.png


View attachment 1438546
Wako wapi sasa wale woooote waliokuwa wakibisha kuwa wanazikwa usiku usiku? Kuna watu walifika hadi kutoa audio kusema kuwa sio kweli, haya sasa njooni hapa muombe radhi.
 
Tena hiyo kamati ingefaa zaidi iwe na chembechembe za ujeshi...(Afande Kova na ugaidi)
Hapana Monk wanajeshi hawafai...hapa wangepewa kazi madaktari..

Rais angekuwa anapokea ushauri na taarifa ya watalaam. Sasa kamati iliyoundwa inaongozwa ma yeye na nyingine eti waziri mkuu.

Wanajua nini kuhusu magonjwa! Wanasiasa wangeshughulika na siasa. Sasa hapa kwetu ukishakuwa mwanasiasa basi wewe ni daktari, mchumi, mwalimu, askari, mwanasheria na kila kitu.
 
Mfano watu kupigwa risasi kutekwa Lissu kupigwa risasi etc......gwajiima kupanga ukabila......
Mbona mawaziri husika na rais hakemei mambo machafu yote haya?
Ukweli ni kuwa yote uliyoyasema yanahitaji kukemewa, kuzuiwa yasitokee. Lakini hata kukiwa na mabaya 10, likarekebishwa moja, kwenye hilo moja tupongeze maana kiongozi amesikiliza sauti zetu. Tumpongeze katika hilo alilofanya vizuri, huku tukimwomba kuchukua hatua dhidi ya 9 yaliyosalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kigongo aliposema watu wa zikwa usiku walikataa.... Sasa inakuwaje wanazuia kitu ambacho hakikuwepo!!?
Watanzania mna mdomo sana. This will cost you! Fanyeni Michezo! Maswala ya msingi mnafanya ujuaji! Duniani kote wagonjwa wa corona wamekuwa. Wakizikwa na serikali! Ndugu hawajarubusiwa kugusa maiti wala kuwa karibu.
 
Daby,
Ndugu yangu Daby nakuelewa unachotaka kukisema hapa, lakini amini nakwambia nadhani kwenye majanga kama haya unahitaji wanasiasa wenye taaluma ya uongozi na uraia kuliko kutaka wataalamu. Jambo la msingi kusema ni kwamba viongozi wetu ni lazima wafuate ushauri wa kitaalamu na kufanya maamuzi sahihi. Viongozi ambao ni wanasiasa wana ukaribu na raia na rahisi kuwatuliza.

Japo lazima nikubali kwamba uongozi wa awamu hii umepwaya kidogo hasa kwenye kushughulikia suala zima la ugonjwa wa korona. Shida zote hizi zinatokea kwasababu raia wamepoteza imani na serikali yao hasa Mkuu wa nchi. Hili limesababishwa na sababu nyingi sana ambazo zina mlolongo mrefu kidogo, mfano viongozi kutoa kauli zenye kukinzana na utaalamu, viongozi kutokuwa wawazi katika kutoa takwimu sahihi na viongozi wa nchi hasa Mkuu wa nchi kuonyesha kutokujali kabisa na kutoa majibu marahisi kwenye maswali magumu.

Hili lisikukatishe tamaa na kuona kwamba wanasiasa hawatakiwi kuwa wazungumzaji. Kisheria na kibusara wao ndiyo inabidi wawe wazungumzaji wakuu kwasababu wao ndiyo wenye dhamana ya kutoa maamuzi ya katika ngazi ya kiraia. Wataalamu wao kazi yao ni kuchunguza na kuleta suluhu, wenye kazi sasa ya kuchagua suluhu ipi inafaa wananchi ni viongozi. Wakati wa majanga maamuzi hayatakiwi yawe yenye hisia sana na wala yawe hayana hisia sana: Lazima tupime na kuangalia kwamba kila uamuzi ambao utachukuliwa utakuwa na madhara kwa idadi gani ya raia, madhara yake ya muda mfupi ni yapi , madhara ya muda mrefu ni yapi, madhara kiuchumi ni yapi, madhara kisiasa ni yapi, madhara kijamii ni yapi na madhara kiulinzi na usalama ni yapi.

Wataalamu hawana ujuzi wa kupima madhara ya kimaamuzi katika ngazi ya kiraia, pia hawana ujuzi wa kuzungumza na raia katika lugha ambayo haitaleta taharuki. Tunahitaji wataalamu na tunahitaji wanasiasa pia, kitu cha msingi ni kuweza kuweka mzani mzuri (To strike a balance) katika ushirikiano wa hawa wawili.

NB: Kuzika raia usiku siyo sawa kiungwana na kisiasa kwasababu kuficha kiwango cha tatizo hakuwezi kuondoa tatizo na inaonyesha serikali ilifanya hivyo kwasababu za kisiasa(Political Expediency) ili kumuepusha mkuu wa nchi na aibu. Lakini pia kuhusisha ndugu kwenye mazishi ni jambo la hatari zaidi kiafya kwasababu lolote linaweza kutokea huko: Muhimu ni kwamba serikali iendelee kuzika na kufuata kanuni za kiungwana za mazishi mpaka pale suluhu itakapopatikana.
 
Aisee!
Nasikiaga jeshini unaweza pewa maelekezo nenda kushoto (ili hali uelekeo sajihi ni kulia), ukiwa njiani unaambiwa rudi nenda kulia.

OK! OK!
 
Tatizo liko hapa, hao wataalamu mbona hawawezi kujitokeza na kuwapinga hawa wanasiasa? Nangalia USA kwa mfano, Dr. Anthony Fauci anajibu technical questions daily, wanapredict vifo na cases za COVID 19. Trump anatekeleza bila ubishi wowote. Maseneta wanapokea reports za majimbo toka kwa wanasayansi, nk Daby,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa huo usiku mbona kuna ulinzi babkubwa au tuseme polisi wamekodiwa tu kwa kazi maalum
 
Mbona walikuwa wanakanusha kwamba hawaziki usiku, bila mitandao ya kijamii wanayoibeza kwamba inapotosha watu haya mambo wala wasingetolea ufafanuzi. Msipotoa takwimu au maelezo ya kweli wakati mambo yote yanatokea ndani ya jamii ambayo hata nyinyi mnaishi humo kila siku mtakuwa mnawalaumu watu bure.
 
Back
Top Bottom