Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Sasa wakati zoezi linaendelea wao walikuwa wapi?..
Ina maana wazikaji walijiamulia Tu kuzika usiku?

Maswali ya msingi hayo. Ubaya ni kuwa wakati taarifa hizi zikitolewa, wenzake na mganga mkuu walikuwa wakikanusha kuwa mambo hayo hayafanyiki!! Tumetoka “divide and rule” sasa tuko “lie and rule”!
 
Inasikitisha kwa hawa viongozi kujitengenezea mazingira ya kutoaminika kwa jamii

Tunapoambiwa mambo yamebadilika, tunapaswa tukubali na mbinu za kuendesha mambo yetu zibadilike ili kuendana na nyakati

Kipindi hiki unapaswa kuwa na mbinu za kisasa unapotaka suala lako liwe siri.

Lakini kwa hii vita uwazi ndio kifalu cha kwanza kwani husafisha njia ya siraha zingine. Siraha inayofuata ni elimu juu ya ugonjwa huo baadae maelekezo na taratibu zifuate kummalizia adui yetu corvid 19
Na usijihisi hujui mtu anapopendekeza namna bora ya kupambana na vita hii
 
Daby, Wewe unadhani nchi inaongozwa na mbumbu? Kwa kuwa hujui unyamaze tu. Tabia ya kurukia mambo ni umbea.
 
Kwenye hili naona kama huenda kutakuwa na mtego mahala !

Huenda imefanyika ile ya kusema “mtoto akililia wembe mpe”

Kilichotakiwa kufanyika ni maboresho tu.

Matharani badala ya kuzika usiku wazike mchana .

Na uwepo Uhuru wa taarifa kuhusu takwimu .

N.k

Hawa huenda wameepuka gharama Yani wamejitoa !

Hili siyo la kushabikia,

Hili linahitaji tafakuli ya kina!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kuzikwa kama wanyama usiku wa manane haikubalikik nakupongeza sana mganga mkuu prof. Abel Makubi na wizara kwa ujumla uwezo wako toka ulipokua bugando ulionekana Hongera sana...

Its not over until its over...
emoji769.png


View attachment 1438546

Hawa wanawafanya watu mabwege mtozeni kila siku wanabadilika kama vinyonga. Watangaze rasmi kuwa Corona hakuna wafungue shule na vyuo maisha yaendelee
 
Kigongo aliposema watu wa zikwa usiku walikataa.... Sasa inakuwaje wanazuia kitu ambacho hakikuwepo!!?
Huyu aliyeandika taarifa hii ya wizara hajui kitu katika uandishi wa taarifa za umma...very sad..sijui serikali inawapata wapi watu wa Aina hii..hii taarifa ni serious na sensitive Sasa unamwachia mtu asiyejua kuwa taarifa inaweza kuzua maswali mengine...hopeless kabisa...mtu mwenyewe anaandika swala baadala ya suala na maswala baadala ya masuala...
 
Kumbe bhana walikuwa wanazika usiku daaah!!utu ni muhimu sana hakuna kitu kinauma kumzika ndugu yako kama ngombe au mbwa!!kwanza kuna plastic bags unaweza kumfunga mtu vizuri tu!

Kingine kuzika mtu bila kuzingati misingi ya dini yake siyo sawa!!hakuna shee wala mchungaji mbona wakubwa getruda,ndasa,Dc yule walipata heshima za ibada kwa dini zao? View attachment 1438649

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,ulikua hufuatilii mitandaoni au? Ulikua huamini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unadhani nchi inaongozwa na mbumbu? Kwa kuwa hujui unyamaze tu. Tabia ya kurukia mambo ni umbea.
Sasa kuna mtu asiye mbumbu anaweza kujibu unavyojibu kweli.
 
Nitoke nje ya mada.

Hatuwezi kuongozwa na wanasiasa kwenye hiki kipindi kigumu kisha tutarajie kuushinda huu ugonjwa.

Ingekuwepo kamati ya wataalamu wa afya na majanga ingekuwa heri mihemko na hisia zingepungua.

Ni kosa mawaziri, wabunge na Rais wawe ndiyo wasemaje wakuu. Hawa kazi yao ilikuwa kupokea ripoti kutoka kwa kamati ya wataalamu.

Wao wanajua walau kila kitu kuhusu magonjwa...hawana mihemko...hawana chuki...wala hawana mirengo ya kisiasa wanasimamia miiko ya kazi.
Wewe unadhani nchi inaongozwa na mbumbu? Kwa kuwa hujui unyamaze tu. Tabia ya kurukia mambo ni umbea.
 
Huyu aliyeandika taarifa hii ya wizara hajui kitu katika uandishi wa taarifa za umma...very sad..sijui serikali inawapata wapi watu wa Aina hii..hii taarifa ni serious na sensitive Sasa unamwachia mtu asiyejua kuwa taarifa inaweza kuzua maswali mengine...hopeless kabisa...mtu mwenyewe anaandika swala baadala ya suala na maswala baadala ya masuala...
Unashangaa hilo wakati Rais katuma ndege Madagascar kuchukua dawa ya kutibu ugonjwa unaoathiri Mafenesi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kuwa yote uliyoyasema yanahitaji kukemewa, kuzuiwa yasitokee. Lakini hata kukiwa na mabaya 10, likarekebishwa moja, kwenye hilo moja tupongeze maana kiongozi amesikiliza sauti zetu. Tumpongeze katika hilo alilofanya vizuri, huku tukimwomba kuchukua hatua dhidi ya 9 yaliyosalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lipi zuri la kumpongeza? Kukimbilia Chato!?
 
Ndio maana katibu mkuu aliyekuwepo alikalia mambo ya uke wenza na Ummy Mwalimu mambo yakaenda ovyo. Mh Rais akaamua kumuondoa pale na kumpeleka mawasiliano. Sasa hivi ndio gwiji la afya limeteuliwa na mh Rais na tunaona sasa mambo yanaanza kubadilika

Sasa wakati zoezi linaendelea wao walikuwa wapi?..
Ina maana wazikaji walijiamulia Tu kuzika usiku?
 
Back
Top Bottom