Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema Wizara yake inajipanga kuanzisha Kliniki ya Ardhi katika mashindano kama ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) ili kuzidi kusogeza huduma za ardhi kwa wananchi.
Mhandisi Sanga ametoa kauli hiyo leo Oktoba 6, 2026, alipowatembelea wachezaji wa Ardhi Sports wanaoendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa fainali wa mpira wa miguu kati yake TAKUKURU unayofanyika viwanja vya Magereza Moshi mkoani Kilimanjaro leo hii Oktoba 6, 2026.
Amesema, mwananchi anapomuona mtumishi wa Wizara ya Ardhi mahali popote basi taswira yake ya kwanza ni kupata huduma, hivyo Wizara inapaswa kutumia fursa kama za michezo ya SHIMIWI kutoa huduma na elimu kuhusu masuala ya Ardhi.
Aidha, Mhandisi Sanga amewataka wanamichezo wa Ardhi Sports Club wanaoshiriki mashindano ya SHIMIWI kuongeza bidii na kujituma katika mashindano hayo.
Amewapongeza wachezaji hao kwa nidhamu wanayoionesha wakati wote wa mashindano, huku akiwataka kuendelea kushirikiana na kujenga mshikamano ili kufikia malengo ya timu na kuzidi kuiwakilisha vyema Wizara ya Ardhi katika michuano hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Ardhi Sports Club, Bw. Swagile Msananga, amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi kwa kuwatembelea na kuwapa moyo wanamichezo huku akiahidi kuzidi kuleta makombe na kuiwakilisha vyema Wizara hiyo.