Wizara ya Elimu acheni kuwa madalali wa Scholarship za Ubalozi

Wizara ya Elimu acheni kuwa madalali wa Scholarship za Ubalozi

Mfano Israel hata nchi za ulaya zinataka sana wafanyakazi wa mashambani hii deal SUA wameibana hadi usome pale badala ya kuwapa vijana hata wasiowanachuo maadamu tu ni wakulima waende wakafanye shamba darasa huko
 
Sijui sasa hali ikoje ila miaka ile nipo high school watu walikua wanaenda balozini wenyewe kuulizia scholarships na walipewa instructions. Pia mnaweza pitia websites za balozi husika au kutuma emails. Balozi za nje huwa zinajibu tena in a timely manner tofauti na bongo mtu kujibu email yako anaona kama anapoteza muda wake, contacts info kwenye taasisi zote za bongo ni mapambo tu hamna anayejibu.
 
nenda katafute passport uone watakavyokuzungusha balaa
 
Sijui sasa hali ikoje ila miaka ile nipo high school watu walikua wanaenda balozini wenyewe kuulizia scholarships na walipewa instructions. Pia mnaweza pitia websites za balozi husika au kutuma emails. Balozi za nje huwa zinajibu tena in a timely manner tofauti na bongo mtu kujibu email yako anaona kama anapoteza muda wake, contacts info kwenye taasisi zote za bongo ni mapambo tu hamna anayejibu.
Tatizo mfumo ndo umeoza!
 
Inabidi ucheze nje ya mfumo. Ukifuata mifumo ya bongo utasubiri sana. Nenda mwenyewe balozini, ingia kwenye sites zao, tafuta scholarships online etc.
Tafuta watu wa ubalozi wawe rafiki zako! Jenga mahusiano nao
 
Kuna kipindi nilikuwa naomba sana scholarship za Hungary aisee wale jamaa pale wizarani mungu anawaona vigezo kibao wakati Hungary wenyewe hawakuwa na mambo mengi wala.
Pole ni mfumo tu! Hapo unakuta Educational Officer anapewa maelekezo kuwa zikija fomu kutoka kina fulani ziweke huku na zingine ziweke hapa.
 
halafu utasikia watz wakarimu sana.
ukarimu wa kinafiki. watz ni wana roho mbaya kama oil chafu. ukarimu wa kinafikifiki ukimzidi lazima akuchukie.
Oil chafu haijafikia viwango vya roho zetu hata mzigo wa toilet haujafikia vigezo kuna watu walisomeshwa na kulipwa mishahara kwa kodi zetu lakini wanachokifanya ni kukwamisha jambo lolote jema kwa mtz wa kawaida na mambo wanayoweza kwa ufasaha ni ulozi na kula au kuliwa mbususu
 
Mungu atusaidie sana
 
Nikweli swala ulilozungumzia .kumekuwa na ubinafsi sana.
KAMA KUNA MTU ANATAMANI KUSOMA NJE YA NCHI KWA GHARAMA NAFUU ANICHEKI NITAMUELEKEZA UTARATIBU WOTE KUTEGEMEANA NA NCHI ANAYO TAMANI KWENDA.
Huo utaratibu uweke hapa. Otherwise nawe ni walewale.
 
Huo utaratibu uweke hapa. Otherwise nawe ni walewale.
Utaratibu huwa unaeleweka Mkuu.
Kitu kikubwa ni kuwa na passport, motivation letters pamoja na vyeti vyako original sio transcripts.. Ukiona mambo mengine ambayo hayana msingi ujue dalali ameingia.
 
halafu utasikia watz wakarimu sana.
ukarimu wa kinafiki. watz ni wana roho mbaya kama oil chafu. ukarimu wa kinafikifiki ukimzidi lazima akuchukie.
Watanzania/wabongo hawana ukarimu wowote ule labda kwa raia wa kigeni na pengewe huwa ni tunajikomba komba tu hasa tukiona mgeni huyo anatoka kwenye yale mataifa yaliyoendelea.....

Ila sisi kwa sisi tunachukiana na kudharauliana sana, tuna roho mbaya sana, wabogo tuna baniana sana....yaani ukiona mbongo amemsaidia mbongo mwenzie na hawajuani basi ujue kuna ama rushwa imetembea hapo au kuna mtu nyuma amemshurutisha....
 
Jana nilipata nafasi ya kukutana na Kiongozi mmoja wa Ubalozi wa New Zealand nchini Tanzania, tulipata wasaha wa kula chakula cha jioni yeye pamoja na familia yake. Tulikuwa kwenye hoteli moja maarufu sana haa Dar es Salaam, na baada ya kupata chakula tulizungumza mambo mengi na kupiga stori mbili tatu, na tukiwa kwenye stori nikapata mshawasha kuwa nimuulize kuhusu suala la scholarships haswa kwa wanafunzi wanaotoka Afrika hususani Tanzania.

View attachment 3058653

Nilimuuliza mengi kuhusu hili ila malengo yangu yalikuwa ni kwenye kufahamu haswa je mchakato wa kupata wanafunzi unakuwa ni mchakato wa namna gani? Lakini pia ushirikiano wao kama ubalozi na nchi husika unakuwaje linapokuja suala la ufadhili wa masomo (scholarship). Yule mzee alibaki kushangaa sana kuwa sifahamu namna mifumo ya Afrika ilivyokaa kihasarahasara tu.

Wanapokuwa na wazo la kutaka kuchukua wanafunzi waende nchi yao huwa wanalazimishwa maombi yapitie Wizara ya Elimu na sio njia nyingine, Wizara ya Elimu ndo inabeba dhamana ya kutafuta watu wenye vigezo ambavyo Ubalozi husika inakuwa inahitaji. Lakini ajabu ni kuwa Tangazo la scholarship la Ubalozi linabadilishwa mwanzo mwisho na kutengenezwa tangazo jingine kabsa ambalo linakuwa na upungufu wa taarifa au taarifa zisizo sahihi.

View attachment 3058654

Halmashauri huwa zina utaratibu wa kuweka matangazo kwenye mbao za matangazo ambazo mara kadhaa zinakuwa nje ya ofisini husika, lakini ukisoma matangazo ya scholarship mara kadhaa taarifa na maelekezo yake sio sahihi kwani zinaweka vigezo vingine visivyotakikana kwa ubalozi. Mfano, huweka kigezo cha muombaji awe mwajiriwa wa serikali ilihali tangazo halisi la ubalozi linadai waombaji wawe watanzania, unakutana na kigezo cha Mwaka wa kumaliza chuo au shule ya Sekondari.

Hizo pesa za kuwasomesha wanafunzi zinzotolewa na serikali husika za huko Ughaibuni sio pesa zenu, kwanini mnaweka ngumu hivyo watu kupata ambao mnataka nyie, sio sahihi. Pia alizunguzia suala la kujuana na kubebana sana. Binafsi nashangaa sana kuona nafasi ya kwenda kusoma nje kwa watanzania wanaoweka vikwazi ni watanzania, sijui tuna roho gani?

Kuna kiongozi mmoja mwaka fulani aliwahi kusema “Mnakwenda kusoma kwenye nchi za Ughaibuni ili iweje, Wakati tuna vyuo vingi bora hapa Tanzania? Kwanini uende Ughaibuni? Je ukipata matatizo? Na ajabu ni kuwa kiongozi huyu amesoma Shahada yake UDSM na viwango vingine vya elimu amesomea Japani pamoja na Uingereza. Ni wivu gani wa kijinga huu kiasi kwamba unaweka ngumu kwa Mtanzania mwenzako kwenda kuosha hata macho?

View attachment 3058655

Sikatai kuwa Tanzania kuna vyuo bora ila hivyo vyuo bora vipo vingapi? UDSM, Muhimbili, Sokoine, UDOM, Mzumbe na SAUT, NELSON MANDELA vilivyobaki sidhani kama vinaingia kwenye orodha ya kushindana na vyuo vikubwa vya nje. Lakini wapo wanaotamani kusoma nje ya nchi na kupata nafasi za kuzuru maeneo kadha duniani.

Kwa hakika nimeumia sana kuona watu walio na roho za ajabu sana kwenye maendeleo ya watanzania wenzao. Baadhi ya balozi wameanza kukataa kutumia mfumo ambao Wizara wameuweka kwani ni mfumo kandamizi sana na usiotoa nafasi kwa watu. Ni kawaida kukutana na majina ya walimu wa vyuo wakipelekwa kwenye usahili na kupewa endorsement za kila aina. Tanzania yangu tunarudishana nyuma mwenyewe.

Rai yangu:
1. Wapatie nafasi balozi wenyewe wafanye usahili na kuwafadhili watu kulingana na utaratibu wao, nyie kama Wizara ya Elimu mbakie kama washauri tu kwa wale ambao wamepata nafasi ya kwenda kusoma. Msiwe madalali wa kuonesha yupi ni bora na yupi sio bora kwa viongozi husika ndani ya balozi zilizopo ndani ya Tanzania.

2. Walimu na wakufunzi sio lazima wawe miongoni mwa watu watakaopewa ufadhili, kwa sababu moja, kila chuo kina mahusiano mazuri na vyuo vingine vya kimataifa duniani kote wanaweza kubadilishana watalaamu hivyo sio lazma wakabanane kuchukua nafasi za vijana ambao hutamani kwenda kusoma elimu nje ya nchi.

3. Waajiriwa ambao ni wazawa (watanzania) acheni chuki wajameni, kumkazia mtanzania mwenzako asipate nafasi sio faida kwako bali ni uchoyo wa kipuuzi sana. Kuna dada yupo Ubalozi wa Uswisi, aisee mbinguni sidhani kama utaingia. Dada ana roho mbaya utadhani anaishi Uswisi. Sio kitu kizuri kabsa.
SIO KWA UBAYA! SIO KWA UBAYA!
Naunga mkono hoja
 
Watanzania/wabongo hawana ukarimu wowote ule labda kwa raia wa kigeni na pengewe huwa ni tunajikomba komba tu hasa tukiona mgeni huyo anatoka kwenye yale mataifa yaliyoendelea.....

Ila sisi kwa sisi tunachukiana na kudharauliana sana, tuna roho mbaya sana, wabogo tuna baniana sana....yaani ukiona mbongo amemsaidia mbongo mwenzie na hawajuani basi ujue kuna ama rushwa imetembea hapo au kuna mtu nyuma amemshurutisha....
umepigilia sumari la mwisho.
 
Watz ukarimu wao kwa wageni lakini sio watz wenzao. Mtz atamthamini mgeni wewe mtz mwenzake atakuona kama takataka. Sijui nani alituroga watz!!
Hii ni kasumba moja ya kipumbavu sana sijui nani mwanzilishi wake.

Yaani mbongo anamuona mgeni ni mtu wa thamani sana wakati huo akimdharau na kumchukulia poa mbongo mwenzie, ukienda pale Airport ndio utaona huu ujinga wazi wazi....!!

Ukienda nchi zingine za hapa hapa Afrika tu hakuna huu ujinga, hata hapo zambia tu wanathaminiana sana wao kwa wao hawana tabia ya kujipendekeza pendekeza kwa foreigners
 
Back
Top Bottom