Wizara ya Elimu acheni kuwa madalali wa Scholarship za Ubalozi

Genesis 9:25-27
3:17), (2) that Africans are cursed because they are portrayed as the descendants of Ham 's son, Canaan, who was cursed by his grandparent, Noah (Gen. 9:25-27),
 
Nimeshtushwa sana khaaa
 
Nchi ngumu sana hii,
Kuna sista mmoja kitaa alinipa story yake jinsi alivyopata nafasi ya Masomo uingereza kimagumashi, kwa sasa ni meneja mkubwa tu makampuni ya simu.
Alinipa ramani niende wzarani ili nijiongeze, nlipofika nlipata somo kubwa sana tangia hapo nikajua watoto wa mafukala tuna njia ngumu sana kufikia mafanikio...
 
Ubinafsi asili yetu labda kama we ni mgeni lengo ni kucontrol watu,hata nguvu kazi tele zinatakiwa nje ya nchi lakini serikali inaweka ngumu watu kwenda kufanya kazi nchi wabakie nchini
Kwanza kitendo tu cha wao kuweka mlolongo mrefu kwenye kupata pasi ya kusafiria kunaonesha ni jinsi gani hii nchi viongozi wake walivyokuwa wabinafsi to the core na wanafurahia watu kukosa exposure, wakati huo wenyewe watoto wao hadi wenye umri wa miaka 2 tayari wamewakatia passport
 
Ni kama hizi scholarship zinazotelewa na TAEC kwa jina la Samia scholarship extended program, hadi nimeapply chuo huko UK na kwa bahati nzuri nikapata ndani ya wakati. Kuja kufungua link sasa ni apply link haifunguki na website Yao mzima haifunguki. Nikachukua iniative ya kuwasialana na wahusika wao, sababu Yao ni kwamba fibre Yao ya Arusha umepata hitilafu (kwa zaidi ya siku 10 sasa) na deadline ni Tarehe 16 mwezi huu. Kuna namna nahisi wanacheza mchezo ila I still believe things will workout in my favour.
 
Kama kuna mtu ana mdogo wake yupo sekondari basi wasiliana na Ofisi za Iqra Fm Mwanza kuna nafasi ya Scholarship. Nimepata kuambiwa kuwa fomu ni 10,000/= tu. Ni kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari.
 
Mchakato tu wa Mandela Washington Fellowship ni kipengele kikubwa ajabu sana
 
Ukifanya process za kupata passport wakikuuliza mbona una haraka usiwaambie kuwa unataka kwenda kusoma na upo kwenye deadline! Hapo ndo umefungua njia ya rushwa na kuzungushwa kama mpira wa kona
 
Wanafanya makusudi! Ila Mungu akutangulie upate haja ya moyo wako Mkuu
 
Ni kwa Ubaya Ubwela
 
Hivi sisi wengine wazee wenye miaka 50, tunaweza kweli kupata scholarship?
 
dah ukweli mchungu, nawaona makada wa chama letu pembeni hapo wameupiga usingizi, ngoja wake waliosoma Kilimani University muanze vita.
Wanakusanya Sumu huko
 
Vigezo vilikuwa nini mkuu?
Mwanzoni wakati Hungary wanadahili wenyewe moja kwa moja mambo yalikuwa mepesi tu na washkaji nawajua wanne walisepa hadi leo wapo huko changamoto ilianza baada ya wazara kuingilia kati scholarship zipitie kwao kwanza wao ndo wachuje hatua za awali halafu baadae ndo wapeleke majina huko Hungary hapo ndo kizaazaa kilipoanzia ni mwendo wa kuweka watoto wao tuu na ndugu kujuana kwingiii
 
Ninaposema kuwa hawa jamaa ni wahuni sidhani kama mnanielewa?! Wameweka tangazo tarehe 2 Agosti na deadline ni tarehe 8 Agosti aisee ni majanga.
Naombeni maadmin waweke hii:
Sambazeni kwa wadogo zenu wapate nafasi.
Site gani au njia gani rahisi ambayo mtu anaweza kuona fursa za Scholarship na nyinginezo nje ya nchi ? maana mimi namalizia Bachelor Degree hapa Tz na natamani sana fursa hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…