Wizara ya Elimu acheni kuwa madalali wa Scholarship za Ubalozi

Mkuu!

Hapa kwa Hungary hakuna kujuana hata kidogo,acha kusema uongo.

Hizo scholarships za Hungary una-apply kozi unayotaka sio wanayotaka wizara,then maombi unatuma chuo ila watu wa wizara wana-recommend tu au kuacha ku-recommend jina lako.

Wewe ulitaka mtu wa wizara akuambie ni kozi gani watapitisha mwaka huu kweli?

Haya mimi ninahafamu watu saba wameenda Hungary mwaka huu,na walikuwa hawajuani na watu wa wizara hadi walipokubaliwa na kupata admission letter ndio wa wizara wakawatafuta tena kwa ajili ya kutaarifiwa tu kuwa wamepata au hawajapata taarifa ya admission zao na scholarships.

Nadhani tukikosa hizo scholarship tujitahidi kuwa wakweli tu sio kubuni mambo.

Wewe hukuwa recommended sio kwa kuwa watu wa wizara hawakujui,ila huenda kuna vitu vilipungua.

Tukubali kukosea mkuu,nakuambia kuna mambo ulikosea lazima.

Wizara wana makosa yao ila mengine tunazidisha kama hili la issues za Hungary,huu ni uongo.

Kuna zile za China,kama huna sifa hata usiombe,ni aibu nchi ku-recommend watu wenye study plan mbovu,kuna mmoja nimeona mwaka huu anahangaika hadi leo kupata chuo,alipotuma study plan nilijua hapati chuo yule.
 
Hiyo ndo Afrika,likiwepo likurutumbi limoja tu likaona hizo nafasi,
Atapeleka ndugu yake hata toka kijijini akajaze nafasi na kuacha wenye vigezo
 
Niliposoma hapa imeniuma kinoma
 
Paragraph ya kwanza tu,nikusaidie mimi naijua hiyo Hungaricum scholarship vema tu,hivyo usiseme mimi sio muhanga,nimekaa hungary 6years kupitia hizo scholarship na zote zimepita wizarani nikiwa simjui yoyote pale.

Tuwe wakweli mkuu.

Cha pili,ni kweli hautumi chuo moja kwa moja ila unakuwa kwenye database yao wanasuburi sending partner ambaye ni wizara,aki-recommend ndio wao wanatuma maombi vyuo ulivyoomba.

Kuhusu kusema watu wa wizara wana watu wao,nakuambia hapana.

Nina mdogo kadhaa nawajua wako Hungary mwaka huu,wameondoma septemba hii,na wanasema hawakujuana na mtu yoyote wa wizara kabla.

Mengine sijui mkuu.
 
Last paragraph,kaa utulie ujifunze.
 
Nikweli swala ulilozungumzia .kumekuwa na ubinafsi sana.
KAMA KUNA MTU ANATAMANI KUSOMA NJE YA NCHI KWA GHARAMA NAFUU ANICHEKI NITAMUELEKEZA UTARATIBU WOTE KUTEGEMEANA NA NCHI ANAYO TAMANI KWENDA.
tangazo la biashara kwanini usielekeze hapahapa ili kilamtu ajaribu bahati yake
 
tangazo la biadhara kwanini usielekeze hapahapa ili kilamtu ajaribu bahati yake
Ni kweli kila kitu kiwe wazi ili tuwasaidie wengine wanaotamani kwenda nje kupata elimu! Hili jukwaa lina madini sana
 
Mkuu hizo za German volunteer kupitia kanisani naomba jina lao..
 
Mkuu hizo za German volunteer kupitia kanisani naomba jina lao..
Inaitwa UEM(united evangelical mission) zipo tofaut tofaut kasome utaona inayokufaa n ipii japo ishapita ila jiandae mana znakujaga tena
South to north volunteer
North to south volunteer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…