Wizara ya Elimu ipitie upya Mtaala wa Masomo ya Sayansi wa A-Level

Wizara ya Elimu ipitie upya Mtaala wa Masomo ya Sayansi wa A-Level

Ata o level pia matatizo yana exist nlikua nashangaa madogo wanajaa kwa HIDDEN pale mtaalamu wa mathematics 😅
Hidden mzee wa majohe...unachukua hii unaweka pale...dah jamaa alikuwa anajaza nyomi la kufa mtu aisee enzi hizo pindi shilingi Mia .Watoto wa juzi hawawezi kuelewa
 
Ila watu wa sayansi mna uwanja mpana sana wa kusomea mambo mengi kwasababu wengi form four mmefanya vizuri. Kuna mwanangu mmoja alipiga zero form six PCM. Alichofanya ni kutumia matokeo ya form na kuanza diploma mambo ya maabara. Alipomaliza akafanya kazi kidogo Azam akajiendeleza degree DIT... tunavyoongea tayari yuko kwa mkemia mkuu na ni afisa mkubwa. Kimaisha anatuchapa bakora karibu wote ambao six tulipita salama. Nashauri vijana tusisomee sifa. Kuliko uende kusoma kozi ambayo haina madili au ajira za kutosha kisa upate sifa bora uende zako hata chuo cha nyuki ukitoka huko unafuga zako nyuki na kuuza asali. Wengi wa watu waliosomea sifa wanahangaika mtaani.
Sio sifa ni kukosa watu wa kuwashauri na tatizo lingine ni TCU, Unakuta mwanafunzi kipindi kile kakaza sana msuli labda aje kusomea udaktari, matokeo ya form six yanakuja amepata labda div 2 ya 11...TCU wanamchagulia kozi.za ajabu ambazo hazipo hata ktk.soko la ajira na kwa kuwa kijana kwao ni masikini basi anaamua aende kusoma hiyo kozi hivyohivyo, mwisho wa siku.ana hitimu na kazi hakuna anabaki kuwa jobless mtaani
 
Sawa nakubaliana na wew tuwalipe walimu mshahara mkubwa kuzuia uvivu wao ,suala la private kufaulisha Lina factor nyingi kwasabab hata shule za serikal znafaulish pia ,una hakika vitabu wanavyotumia feza ni ivo ivo vya Pugu au Minaki!!
Kiwango cha ufaulu wa shule za serikali kidogo o sn ukifananisha na private. Mitihani wanayofanya ni ileile na syllabus ni ile ile, Ubaya au uzuri wa elimu ya advance kuna vitabu vingi na hakuna kitabu maalumu za darasani, unaweza kusoma CHAND, NELKON, MATHEMATICAL ENGINEERING, n.k, muhimu zinapatikana topics za kwenye syllabas. Sioni kama kuna haja sana ya kujua vitabu wanatumia tofauti au sawa ila cha muhimu wote wanafuata syllabas moja.
 
Muda ni kweli mdogo, lakini kwa mwanafunzi aliye serious kufaulu ni simple tu.

Na trend inaonesha ufaulu wa advance ni mkubwa kushinda wa Ordinary.

Huo muda uliwekwa kwa standard za kimataifa wala hakuna shida yoyote kwenye sylabus.

Ukitaka kujua nachoongea ni kweli, nenda hapo Kenya ambako wanasoma secondary miaka 4 tuu vitu vyote vinavyofundishwa kwa miaka 6 hapa Tanzania.
Umefuatilia ufaulu wa PCB/M au unaongelea Vasco Dagama alifika Ras ya Tumaini Jema mwaka 1497
By the way, usilete hoja za kijiweni kuwa Elimu ya Form 1V kenya ni sawa na Elimu ya Form Six Tanzania. Somesha mtoto hadi form four Kenya halafu fuatilia ni vyuo vingapi vya ulaya vitamkubali kwa degree ya kwanza hata kama una hela ya kulipia???
Ungekuwa umebahatika kusoma PCB/M ningekuambia uangalie Syllabus ya kenya na TZ uone coverage yake naamini ungedelete hii post yako
 
Umefuatilia ufaulu wa PCB/M au unaongelea Vasco Dagama alifika Ras ya Tumaini Jema mwaka 1497
By the way, usilete hoja za kijiweni kuwa Elimu ya Form 1V kenya ni sawa na Elimu ya Form Six Tanzania. Somesha mtoto hadi form four Kenya halafu fuatilia ni vyuo vingapi vya ulaya vitamkubali kwa degree ya kwanza hata kama una hela ya kulipia???
Ungekuwa ubebahatika kusoma PCB/M ningekuambia uangalie Syllabus ya kenya na TZ uone coverage yaake naamini ungedelete hii post yako
Ufaulu unajulikana mkuu, hizo PCB/M ni rahisi ndiyo maana hata ma TO huwa wanatoka combinations hizo...
 
Pamoja na hayo mazingira kuna watu wamesoma shule za kata, akaenda advance sehemu ambazo walimu wa masomo hayo hakuna na bado wakafaulu vizuri tu. hayo maoni yako sioni kama yana tija. ishu ni kuboresha miundo mbinu na maslahi kwa walimu wa hayo masomo lakini nje ya hapo yatakuwa yaleyale
Mtoa mada ana hoja ya msingi sana,wengi wanaofauru ni wale wazee wa kukalili ila sio wa kuelewa. Ndio maana wengi wakijoin vyuo wahadhiri wanalalamika kuhusu ubora wa wanafunzi.
 
Back
Top Bottom