Wizara ya Elimu liwekeni sawa hili la watoto kutoka shule saa 11:30 jioni

Wizara ya Elimu liwekeni sawa hili la watoto kutoka shule saa 11:30 jioni

polokwane

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2018
Posts
3,361
Reaction score
5,842
Watoto wanaumia sana na hii ratiba hasa kwa mazingira ya shule zetu watoto wanafika majumbani saa mbili hadi saa tatu usiku ukiwauliza wanadai foleni mara daladala zinasumbua

Hebu Serikali mlione hili hata kama ndio kusoma hapana
 
Mimba naziona kwa madent [emoji41]
 
Watoto wanaumia sana na hii ratiba hasa kwa mazingira ya shule zetu watoto wanafika majumbani saa mbili hadi saa tatu usiku ukiwauliza wanadai foleni mara daladala zinasumbua.

Hebu serikali mlione hili hata kama ndio kusoma hapana.

Mimi jumatatu ilopita nililia...bahat nzuri nilikua mjini jaman mwanangu akawa ni mdogo bas anasukumwa balaa na wanafunzi wa sekondari..nilijiskia huzuni. !kanafika kametepeta balaa! Yaan nna kibarua Cha kwenda kila siku mjini jion kumfata..arghhh inasumbua sana
 
Watoto kusoma mpaka saa kumi na moja in ukichaa wa aina yake. Halafu usifikiri wanasoma, ikifika saa nane ni kucheza tuu. Watoto wakirudi wako hoi.
 
Pengine wanaingia darasani 6.30 Am mpaka 4.30 pm. Usiku wanaliunga kuanzia 7.30 pm hadi 10.00pm
 
Kwani Ile waraka wa kamishna wa kamishna wa elimu wa tarehe 1 July wa kutengua agizo la waziri wa elimu ulikuwa fake? Mbona hawajaukanusha Kama ulikuwa fake?
Nimejaribu kumdodosa rafiki yangu ambaye ni afisaelimu wa wilaya kaniambia anasubiri barua kutoka tamisemi sijui ya Nini ilihali waraka wa kamishna anao kwenye faili lake la kazi! Inashangqza Sana.
 
Wahusika wanadai waraka haujawafikia
 
Wahusika hasa Mama Ndalichako please usikae kimya hili la watoto kurudi usiku
 
Yaaani Huu ni Upuuuzi mm kma mwanafunzi binafsi kwnza ina bana san sabbu unfik nyumbn umechok alaf bado homework bado hujasom duh yan wangefnya hata saa8 jaman
 
Hiyo ratiba ya kutoka saa kumi na moja nafikili waliangalia kwa mikoani tu lakini sio kwa dar maana sio kwa foleni hizo
 
kinachokera ikifika sa8 unusu hakuna mwalimu zaidi ya mwalimu wa zamu tu shuleni .
yanini kuwapotezea mda watoto
 
Back
Top Bottom