Wizara ya Elimu liwekeni sawa hili la watoto kutoka shule saa 11:30 jioni

Wizara ya Elimu liwekeni sawa hili la watoto kutoka shule saa 11:30 jioni

Maamuzi yalitolewa kisiasa, yakatekelezwa kisiasa, na sasa hawataki kurudisha ratiba ya kawaida kwa kisingizio cha barua. Mnaumiza watoto.
 
Sio watoto tu hata wazazi tumeumizwa, kwani baadhi ya shule walipiga hesabu ya hayo masaa 2 yaliyoongezeka pamoja na siku za kufunga shule December zilizosogezwa mbele wakauita robo muhula na wakaongeza ADA wakasema hayo ni maamuzi ya bodi za shule.
 
Watoto wanaumia sana na hii ratiba hasa kwa mazingira ya shule zetu watoto wanafika majumbani saa mbili hadi saa tatu usiku ukiwauliza wanadai foleni mara daladala zinasumbua.

Hebu serikali mlione hili hata kama ndio kusoma hapana.
Ni wapi huko mkuu
 
Hiyo ratiba ya kutoka saa kumi na moja nafikili waliangalia kwa mikoani tu lakini sio kwa dar maana sio kwa foleni hizo
Huko mikoani kwenyewe swala sio foleni tena ni watoto wanatembea porini kilometres 7+ kurud nyumbani na ni giza
 
Wahusika wanawatesa watoto bure. Eti CCM inahuruma na wanyonge, badala yake imewatesa
 
halafu anarudi nyumbani saa tatu halafu saa 12 asubuhi yupo barabarani kusubiri daladala nadhani hapa wizara ilienda haraka bila kutafakari mazingira ya shule zetu ingawa ratiba hii kwa shule za bweni haina shida
Sipati picha vijijini watoto wanaokaa mbali na shule.

Hadi km 15 toka nyumbani na shuleni.
 
Hiyo ratiba ya kutoka saa kumi na moja nafikili waliangalia kwa mikoani tu lakini sio kwa dar maana sio kwa foleni hizo
Hata huko mikoani kuna wanafunzi wanakaa mbali sana na shuleni.
 
Me huwa hata sioni mantiki ya watoto kukaa shuke siku nzima.... Watoto wangewekewa utaratibu wa kukaa masaa machache shuleni
 
Watoto wanaumia sana na hii ratiba hasa kwa mazingira ya shule zetu watoto wanafika majumbani saa mbili hadi saa tatu usiku ukiwauliza wanadai foleni mara daladala zinasumbua.

Hebu serikali mlione hili hata kama ndio kusoma hapana.
mbona kwa jiji la mwanza washarekebisha maana ratiba ile ya zamani imerudi toka wiki iliyopita. sasa hivi hakuna kutoka saa 11 labda kwa shule zilizokua na shifti.
 
mbona kwa jiji la mwanza washarekebisha maana ratiba ile ya zamani imerudi toka wiki iliyopita. sasa hivi hakuna kutoka saa 11 labda kwa shule zilizokua na shifti.
Mwendo ni uleule wa saa 11
 
Utaratibu wa kutawanyika 11:30 jioni ni utaratibu wa kuumiza watoto
 
Mimi jumatatu ilopita nililia...bahat nzuri nilikua mjini jaman mwanangu akawa ni mdogo bas anasukumwa balaa na wanafunzi wa sekondari..nilijiskia huzuni. !kanafika kametepeta balaa! Yaan nna kibarua Cha kwenda kila siku mjini jion kumfata..arghhh inasumbua sana
Pole Sana!!Ila kuna waraka unaohusu ratiba walitoa.....vp hawajautekeleza??
 
Baadhi ya wahusika ngazi ya wilaya wanasema waraka ule haujaandikwa kupita kwa RAS's hivyo bado wanasubiri maelekezo kimaandishi na sio barua ya inayizagaa katika mitandao ya kijamii
 
Hii kitu itawaumiza sana watoto,kuna mtoto mmoja 5yrs anaamshwa saa 11 asubuhi,gari inawapitia 11:30 alfajili na anarufi 12:00 jioni hadi huruma.Ndani ya hizi siku mtoto amedhoofika kabisa,Wazazi inatakiwa tuangalie hata shule za kupeleka watoto siyo mashindano tuu or school bus itamuacha mara Junio junio,,,Nikole nikole n.k kumbe tunaleta athari kubwa ubongoni mwa Watoto
 
Ratiba ya awali imesharejeshwa,Sasa kama kuna wanaokiuka,yakitokea yakitokea wataijibu Jamhuri!
 
Back
Top Bottom