Wizara ya Katiba na Sheria inasimamia mikataba na majadiliano yote ya kisheria ya Tanzania. Kabudi kashindwa hii kazi akiwa Waziri atawezaje nje?

Wizara ya Katiba na Sheria inasimamia mikataba na majadiliano yote ya kisheria ya Tanzania. Kabudi kashindwa hii kazi akiwa Waziri atawezaje nje?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Wizara ya Katiba na sheria ni msimamizi wa majadiliano ,mikataba na maduala yote yanayohusu sheria. Kabudi alipokuwa Waziri alikuwa mshauri Mkuu wa mambo haya. Kutumbuliwa kwake means ameshindwa kutekeleza Wajibu wake.

Najiuliza, kazi mpya anayoyokwenda kufanya ataifanya bila kuelekezwa au kumshirikishikisha Waziri mwenye dhamana? Najiuliza kazi anayokwenda kuifanya atafanya bila shiriki ya Mwanasheria Mkuu? Kwamba Kabudi atakuwa na ofisi yake? Wasaidizi wake watakuwa wakina Nani?

Tukubali tu Kwamba wametumbuliwa na nafasi pekee waliyobaki nayo ni Ubunge Hadi pale ofisi zao zitakapotengenezewa muundo kama zikifunguliwa. Wanaungana na Mkuchika kukaa benchi siku ziende.

Mwisho najiuliza stahiki za hiyo ofisi zitapitishwa na Bunge au zitatokaje hazina? Au ni kazi isiyo na salary au marupurupu? Hapa CAG ataibuka na hoja huko tuendako, Haina tofauti na kununua ndege cash,. Fedha za umma lazima ziwe na utaratibu siyo zinatumika kwa fadhila.

Marekani pamoja na utajiri wao wote Rais akimteua mtu nje ya mfumo au akimpa kazi nje ya mfumo rasmi wa serikali lazima aeleze utaratibu wa malipo. Sisi kqetu na umasikini wetu hakuna anayetafsiri haya mambo . Tubadilike tuwe serious
 
Kapu la tozo limejaa pesa na hakuna mahali pa kuzitumia kwa hiyo ni lazima vyeo hewa viundwe ili kapu la tozo lipumue kidogo
 
Wizara ya Katiba na sheria ni msimamizi wa majadiliano ,mikataba na maduala yote yanayohusu sheria. Kabudi alipokuwa Waziri alikuwa mshauri Mkuu wa mambo haya...
Taarifa kuwa ameshindwa umezipata wapi mwenzetu. Nafikiri wewe ni great thinker na unajua masuala ya kushinda na kushindwa yanahitaji uthibitisho.

Kama Mkuu wa nchi mwenye taarifa zote za wazi na za siri amethibitisha kuwa amefanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Wewe unakuja na story tu bila ushahidi wowote kuwa ameshindwa!!!. Uzi huu umekushusha thamani sana! Jali zaidi ubora wa uzi zako siyo tu uwingi.
 
Jamani mnashindwa kuunganisha matukio?

Hapa mama ametumia cheap propaganda.

Juzi kati alisema kuna watu atawaacha ili wakajiandae na 2025!

Tafsiri yake ni kwamba, hao wakioachwa, ndiyo walikuwa wanajiandaa na 2025.

Muda ni msema ukweli. Baada ya miezi miwili tutamuuliza Kabudi na Lukuvi, vipi mnashirikishwa? "Watajibu ndiyo, tunaendelea na kazi vizuri" hata kama hawashirikishwi, na ndio maana wamepewa vyeo ambavyo havimo kwenye muundo. Wakijibu hapana, ina maana majina yatakatwa 2025.

Siasa ni mchezo mchafu!

Jiulize. Kabudi anapewa cheo ambacho hakipo kwenye muundo, je, atawezaje kwenda kuanzisha majadiliano na wawekezaji wakati kuna watendaji wa wizara husika?

Kwa cheo hicho, tafsiri yake ni kwamba, kwa sasa Kabudi ni mtumishi wa wizara inayohusika na wawekezaji! Na atakuwa anaagizwa na waziri husika!
 
Back
Top Bottom