SoC04 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu itumie mfumo wa kidigitali kupokea na kufuatilia matukio ya kijamii

SoC04 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu itumie mfumo wa kidigitali kupokea na kufuatilia matukio ya kijamii

Tanzania Tuitakayo competition threads

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
JINA LA MFUMO: JAMII SALAMA (JASA)

UTANGULIZI.

Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu inakabiliwa na ukosefu wa mfumo bora wa kupata na kufuatilia taarifa za kijamii zinazohusu matukio mbalimbali ambayo yapo kinyume na sheria kitu kinachopelekea watu wengi kufanyiwa ukatili pasipo kupatiwa msaada na kisheria haraka ama kutopatiwa kabisa.

Kwa sasa njia ya simu ya mkononi ndio inayotumika na imefeli kuwa njia mbadala na kupelekea watu wengi kushindwa kufikisha tarifa zao kwa mamlaka husika ili kuhughurikiwa.

MUUNDO NA UTENDAJI KAZI.

Mfumo tendaji wa kompyuta.

Utatumiaka na wizara ,jeshi la polisi kitengo maalumu cha dawati la jinsia, na maafisa ustawi wa jamii.
Utaunganisha jeshi la polisi,wizara na mwananchi kwa msaada wa programu ya simu,Utatumia akili bandia ili kuchuja uhalisisa wa taarifa ,na mtiririko wa taarifa.

Utaundwa na sehemu zifuatazo;
  • Social welfare.
Ni maalum kwa Maafisa maendeleo ya jamii,wamiliki wa vituo vya kulelea watoto yatima na wadogo Katika shule.

Kutakuwa na vitufe vya “Welfare Officers” na “Welfare Centres”,katika “Welfare officers” afisa ataachagua mkoa anaofanyia kazi, wilaya na kata kulingana na nafasi yake,na kuingia (LOG IN) kwa kutumia jina tumizi na nywila,vitatokea vitufe “Welfare centres “ na “Reported Issues”.

katika“Welfare centres “ yatapatikana majina ya vituo vyote vya kulelea watoto wadogo (day cares),yatima na wengine wenye uhitaji vinavyopatikana katika ngazi aliyopo na anaweza kupitia kituo kimoja kimoja na kupata taarifa mbalimbali kuhusu watoto au wahitaji.

katika kila mwisho mwa jina kutakuwa na kitufe cha “Status” ambapo atapata taarifa kamili za mtoto huyo kama maendeleo ya afya ,pia atapata taarifa jumuishi ya kituo husika kupitia kitufe kingine cha “status” kilichopo mwisho mwa orodha ya majina ya watoto wote,taarifa zote zitajazwa na wamiliki wa vituo husika.

katika “Reported Issues”kutapatikana taarifa zote za kijamii ambazo ni matukio yaliyo ripotiwa na wakazi katika mkoa,wilaya ama kata husika,kutakuwa na orodha ya taaarifa zote na mwishoni mwa kila taarifa kutakuwa na kitufe cha “VIEW”, ambacho kitakuwa na video ya mlalamikaji au mtoa taarifa yenye maelezo,na chini ya video kutakuwa na vitufe “Contact”,“Print” na “Submit”,afisa atawasiliana na mtoa taarifa kupitia kitufe cha “Contact” ambapo kuna “Phone number” na “video call” ,atatakiwa kugusa kitufe cha “Video Call” ambapo itakwenda kuita katika programu ya simu ya mtoa taarifa.
kama hatakuwa hewani,mfumo uta badiri na kupiga kwa simu ya kawaida kwa kurejea namba iliyohifadhiwa katika mfumo,ambapo atatakiwa kujitambulisha na kumuomba aingie katika akaunti yake ya programu ya simu ya wizara kwa ajili ya majadiliano,lengo ni kuhakikisha mawasiliano yote yanahifadhiwa na kuhakikiwa na mfumo, lengo la mawasiliano ni kuthibitisha ukweli wa taarifa hiyo kabla haijatumwa kwa jeshi la polisi ama kutafuta suluhu.

Kwa taarifa ambazo ni za unyanyasaji wa watoto,kulawitiwa kubakwa ,afisa atalazimika kuzituma moja kwa kwa jeshi la polisi kupitia kitufe cha “Submit” baada ya kubonyeza kitufe cha-print,kitufe hiki hakimaanishi kwamba ana chapisha taarifa hiyo,isipokuwa ni amri ambayo inaifanya taarifa husika iwe katika mpangilio mzuri na iunde taarifa ya maandashi ili iweze kutumwa baada ya kubonyeza kitufe cha “Submit”,kama hatabonyeza print taarifa haitaweza kutumwa na atapata ujumbe kwamba hawezi kutuma kabla ya kuprint.
  • Police.
Zitapatikana taarifa zilzo tumwa na maafisa wa jamii,polisi watakao kuwa na uwezo wa kuingia hapo ni wale walioteuliwa kushughurikia masuala ya kijamii tu ataingia (LOG IN)kwa Jina tumizi na Nywila ambayo alisajiriwa,na kuona vitufe “Reported Files” ambapo zitapatikana taarifa kwa ajili ya uchunguzi.

“Pending Files” ambapo kuna mafaili ambayo yanasubiri ripoti za uchunguzi zikamilike ama ripoti zake zimesha kamilika na zinasubiri kufunguliwa kesi mahakamani,kutakuwa na orodha ya kesi zote zilizoripotiwa na mbele ya kila jina la kesi kutakuwa na kitufe “Investigation status” ambapo ataona Neno “In Progress” kama bado uchunguzi haujakamilika, “Complete” ,kama uchunguzi umekamilika na katika.

“File case”
kesi zote ambazo upelelezi wake umekamilika zitaonekana hapa,Katika kila jina la faili kutakuwa na vitufe “REVIEW” ambapo ripoti ya uchunguzi itakayoambatanishwa na maelezo ya mlalamikaji iaonekana,chini ya ripoti hiyo kutakuwa na vitufe “ACCEPT” ambacho kikibonyezwa ripoti itaenda kuonekana sehemu ya “FILE”ambapo yatapatikana mafaili yote yaliyokubaliwa baada ya kuyapitia.

Mfumo utaruhusu kuchagua faili moja moja ama kwa ujumla,baada ya kuchagua,chini mwisho wa mafaili kitatokea kitufe cha “Magistrate” kitajacho jumuisha orodha ya mahakama ilikumuwezesha kuchagua mahakama sahihi kwa ajili ya kusajiri kesi hiyo,baada ya kuchagua kitakuja kitufe “Confirm” kwa ajili ya kuthibitsha usajiri na kurudishiwa ujumbe kuwa kesi imesajiriwa ,na ataweza kuona katika kitufe cha “Notification” katika akaunti yake.

Mfumo huu uta unganishwa na mfumo wa mahakama ili kuraisisha usajiri wa kesi na ufuatiliaji.

"COMMENTS” kitatumika endapo tu kuna kasoro ambapo atabonyeza na kueleza kasoro zilizoonekana kisha atatuma kupitia alama ya kutuma iliyopo kulia na “Notification” itaonekana katika akaunti ya polisi aliyeandaa ripoti ya upepelelezi kwa ajiri yakufanyiwa marekebisho
  • Ministry .
Patatumiwa na watumishi wa wizara kwa ajiri ya kufuatilia utendaji kazi na mienendo ya utendaji kazi wa ustawi wa jamii,kutakuwa na kitufe cha Minster,Deputy Minister,General secretary na Deputy General secretary na vinginevyo muhimu,kwa kufungua kitufe husika aingia kwa kutumia Jina tumizi na nywila.

Waziri ataweza kuingia sehemu zote za mfumo lakini hataweza kubadiri chochote ila ataweza kuacha ujumbe katika sehemu husika endapo atagundua kuna suala halijafuatiliwa kikamilifu,katika kila kitufe kutapatikana orodha ya vipengele vyote ambavyo vimehusishwa katika mfumo na katika upande wa kulia ataona orodha ya watendaji wote wa wizara na ustawi wa jamii waliopo mtandaoni,na ataweza kuwasiliana nao.

Programu ya simu.
Itatumiwa na wananchi kuripoti matukio na kufuatilia mwenendo wa matukio yaliyo ripotiwa ,mwananchi atajisajiri kupitia “Register” ndipo aweze kuingia (LOG IN) katika mfumo kwa kutumia jina tumizi na Nywila mbazo ataingiza wakati wa kujisajiri.

Matukio yote yatarekodiwa katika mfumo wa video na sauti na hakuna atakayeweza kufuta,bali ataweza kufuatilia mlolongo wa taarifa kujua hatua iiyofikia kama vile kwa Afisa ustawi.nk.

Pia kutakuwa na namba maalumu ya simu kwa ajili ya kuripoti matukio kwa nji ya simu ya kawaida,mtoa taarifa atapewa maelekezo akitakiwa kusubiri mlio ndipo aanze kuongea, na kunyamaza kwa sekunde kadhaa baada ya kumaiza na kupewa taarifa kuwa taarifa yake imerekodiwa na kuhifadhiwa asubiri mrejesho.
Taarifa hii itahifadhiwa na kuonekana katika mfumo ikimbatanisha nambari ya simu iliyotumika kutoa taarifa.
 
Upvote 2
Utatumia akili bandia ili kuchuja uhalisisa
Sio kasi sana bro, maana.

maana kikanuni akili bandia inapaswa kusimamiwa na mwanadamu (hu.an intervention/overseer) je unataka tuiachie akili bandia ifanye maamuzi yote yanayoathiri ustawi wa jamii moja kwa moja. Sawa tuwekeze katika mfumo, na pia tuwekeze katika watu. Haiepukiki.

Nakubali mifumo ni mizuri, ila ije tukiwa tumejiandaa kuwa inakuja kuwasaidia watu kufanya kazi zao kikamilifu. Haiepukiki.
 
Sio kasi sana bro, maana.

maana kikanuni akili bandia inapaswa kusimamiwa na mwanadamu (hu.an intervention/overseer) je unataka tuiachie akili bandia ifanye maamuzi yote yanayoathiri ustawi wa jamii moja kwa moja. Sawa tuwekeze katika mfumo, na pia tuwekeze katika watu. Haiepukiki.

Nakubali mifumo ni mizuri, ila ije tukiwa tumejiandaa kuwa inakuja kuwasaidia watu kufanya kazi zao kikamilifu. Haiepukiki.
Kuna taarifa feki ambazo mtu anaamua kufeki,ndizo hizo ambazo zitachujwa kwa lengo lakupunguza mrundikano wa taarifa zisizo na uthibitisho,akili bandia ni algorithm ambayo machine au mfumo unaelekezwa kwamba ikiwa hivi maana yake ni hivi hivyo ufanye hivi,hapa nalenga kuzuia binadamu kutumika kuchuja maana weledi ni mdogo.
 
Kuna taarifa feki ambazo mtu anaamua kufeki,ndizo hizo ambazo zitachujwa kwa lengo lakupunguza mrundikano wa taarifa zisizo na uthibitisho,akili bandia ni algorithm ambayo machine au mfumo unaelekezwa kwamba ikiwa hivi maana yake ni hivi hivyo ufanye hivi,hapa nalenga kuzuia binadamu kutumika kuchuja maana weledi ni mdogo.
Nimekumbishia hicho kwa sababu AI inatakiwa kusaidiwa baadhi ya maamuzi ili kuhakiki maana mashine (AI) ikiambiwa mtu wa mwaka 2000 anatakiwa aandike ana miaka 24 leo(mwaka huu 2024), halafu mtu akajichanganya akaandika 23 kisa mwezi wa 10 haujafika bado(aliozaliwa yeye) mfumo utamlima X fasta.

Ndiyo maana nasema hatuwezi kuipa mashine uhakika asilimia zote, watu haohao bado watahitajika hata kama ni kwa uchache kiasi ukilinganisha. Na watu wasiwe na asilimia zote watachekiwa na system check and balance.

Japo bro, nimeipata pia pointi uko nayo maana hata baadhi ya watu hutenda kazi kama AI tu, unakuta mtu anasema tu. Utaratibu unasema xyz, hata kama ipo sababu ya kueleweka ya vinginevyo. Na mara nyingine wanadanganyika kwa hizohizo sababu lakini AI itastick na protocali kuepusha hilo. Naiona pointi yako.

Kwa hiyo mwisho mwishoni, inabaki kuwa ni vyote tunahitaji mifumo imara na watu bora.
 
Back
Top Bottom