Wizara ya Maji yaangalieni haya kabla ya kukimbilia mfumo wa kulipia bili ya maji kabla ya matumizi (prepaid bill system)

Wizara ya Maji yaangalieni haya kabla ya kukimbilia mfumo wa kulipia bili ya maji kabla ya matumizi (prepaid bill system)

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Habari wanajamii!..
Naona mfumo huu wa kulipia huduma kabla ya matumizi umeanza kuwa mfumo pendwa licha ya kuwa mfumo unaomuumiza zaidi mtumiaji au mlaji hususani huduma inapokosa ubora.

Ni kweli wananchi tunapaswa kulipia huduma tunazopatiwa na Serikali ili kusaidia suala zima la uendeshaji na uendelevu wa huduma hizo.

Lakini, ni jambo la wazi kabisa kuwa bado mifumo ya ubora wa huduma haijaangaliwa vyema ili kusadifu mfumo wa ulipaji bili kabla.

Mathalani, yapo maeneo ambayo maji yanaweza yakakosekana mwezi mzima na ukifuatilia unaambiwa kuna matengenezo yanaendelea. Hali hii inazidi kumuumiza mlaji.

Ushauri wangu, huduma ya maji iboreshwe kwanza ndipo mifumo ya kulipia kabla iangaliwe na siyo mifumo hiyo kuangaliwa kabla ya ubora wa huduma. Kinachofanyika kinachefua sana kwa mfano Mtu analipia maji Benki kwenye account ya mradi wa maji halafu anafuatwa na kuambiwa apeleke payslip za malipo kwenye ofisi ya maji ili apewe risiti ya mradi. Utaratibu huu ni mbovu na unatoa mianya ya ubambikizwaji wa madeni na kufubaza ukaguzi wa kina wa mradi.


"Kupata maji safi na salama ni haki ya binadamu"..tuanzie hapo kwanza.
 
Back
Top Bottom