Wizara ya Maliasili na Utalii yatuhumiwa kutumia Tsh. 2.5B kuanzisha chaneli ya Urithi Festival nje ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge

Wizara ya Maliasili na Utalii yatuhumiwa kutumia Tsh. 2.5B kuanzisha chaneli ya Urithi Festival nje ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
HAYA ANAYOONGEA HUYU MBUNGE YANA UKWELI?

Na Thadei Ole Mushi

FB_IMG_1586249504561.jpg


2360661_IMG_20200407_082820.jpg


Mbunge wa Chadema Catherine Ruge amesema kuwa wizara ya maliasili na utalii imetumia bilion 2.5 kuanzisha televesheni ya Urithi Festival. Kwa madai ya Mbunge huyu Ni kuwa Chanel hiyo pesa yake haikupitishwa na bunge.....

Kama ni kweli nimesikitika sana, sio kwa sababu ni kitu kibaya au Sio kwa sababu budget yake haikupitishwa na Bunge Bali nimechukia kwa sababu tayari TBC Wana Safari Chanel hii nyingine ni ya nn? Mbona tunashindwa ku link Mambo madogo hivi? Tofauti ya Chanel hizi mbili ni Nini?

Anyway tuachane na hiyo Issue....

Bunge linaloendelea kwa Sasa wabunge baadhi wa CCM wameonekana wakiaga kabisa Bungeni kuwa wanaweza wasirudi tena Bungeni.

Kuna kipindi niliandika kuwa CCM ni wakati wa kumsaidia Rais kupata wabunge wazuri na akili kubwa ili wakamsaidie kazi vizuri. Nilionyesha jinsi ilivyokuwa ngumu kuunda Baraza la mawaziri hadi ikabidi Rais atafute njee ya wabunge wa kuchaguliwa, tuliona jinsi ambavyo amekua akiwatumbua kila kukicha nk.

Hii ni ishara Tosha kuwa tulishindwa ku screen wagombea wazuri na ambao ni akili kubwa. Siku zote huwa nasema akili kubwa ni Mali ya Rais ndio inayotakiwa imzunguke Rais....

Tanzania tuna rasilimali nyingi mno, kinachotuangusha ni aina ya Viongozi tunaowachagua kwenye ngazi mbalimbali. Wananchi huko vijijini wanasubiri kanga, t-shirt, na kofia. Atakayegawa vitu hivi na Rushwa nyinginezo ndiye atakayekwenda kumzunguka Rais.

Idara ya Usalama hili eneo msiliache kabisa linawahusu katika kuchunguza (Vetting) ya wagombea sio CCM tu hata vyama vingine mnaweza kutusaidia kuingiza mkono. Usalama wa Taifa unahusika Sana katika ujenzi wa taifa kwa hiyo tukipata Viongozi wabaya itakuwa hamkuwatendea haki watanzania.

Niliwahi kusema Rais huu ni wakati wake wa kuachana na wabunge aliowarithi toka awamu nyinginezo. Waanze kushawishiwa watu tunao wahitaji. Sio lazima wawe maprofesa ila watu wenye vision kubwa.

Mzaa sio mzaa? Huu kwangu ni Mzaa HK anatakiwa pushup nyingi Sana.

Ole Mushi
0712702602.
 
Duh heading yako na content ni mbingu na ardhi...

USALAMA WA TAIFA,
Kulisaidia Taifa, kwani blaza ni yapi hasa majukumu ya taasisi hiyo hata waende kufanya kazi za chama na wananchi ya kupitisha wagombea wa vyama na kuwachagulia wananchi nani awe kiongozi wao.

VETTING
Sina uhakika kama timu hii inahusika moja kwa moja na hao usalama wa Taifa na vyovyote iwavyo, nguvu kubwa ya kuipata cream ya Taifa inatakiwa kuwa hapa na kwakua Rais anayo nafasi ya kuteua wabunge 10 hivyo iwapo cream inapelea kwenye wabunge wakuchaguliwa basi anaweza kuongeza kupitia nafasi hizi...

Msalimu huyo Mzee
 
Bilioni umesema!? Tuletee na mnyumbuisho wa matumizi vs kilichokwapuliwa kabla ya kumtuhumu huyu njema!
Maana watu wa ufipani hawachezi kukaa mbali na bla kadabra!
Usipate tabu, hii hapa
 

Attachments

  • IMG_20200407_082820.jpg
    IMG_20200407_082820.jpg
    341.7 KB · Views: 1
Hii ndio "kunya anye kuku,akinya bata kahalisha"...yaani bongo mtu akiiba kuku au kisimu cha tochi tu ujue kifo kinamuita,lakini kunawatu wanakwapua mabilioni tunawaangalia tu...mwizi ni mwizi mura,kamata wote tia kibiriti.
 
Kama source aliyotumia huyo mbunge ni hii, hasa hapo kwenye Urithi TV, napata wasiwasi na uwezo wake wa Kiinglish, lakini pia na mleta mada naye hapo ameonyesha ukihiyo kwenye hilo eneo.
 
Amani iwe nanyi.

Kwa wa kristo wote duniani kipindi cha kwaresma ni kipindi cha toba ambacho watu hukitumia kujirudi kwa muumba wao kwa kuomba na kusamehewa zambi zao.

Si sawa kwenye kipindi cha kwaresma kusema uongo waziwazi na kujilizaliza ili uonekane kwamba unaonewa na kuteseka sana kuliko binadamu wote hapa duniani!

Ndugu yetu huyu Tundu Lisu amekuwa mtu wa kusema uongo na kuzushia wengine mabaya ili waonekane ni wachafu mbele ya jamii, mfano kwa miaka nane alizunguka kote nchini na duniani akimtaja Lowasa kuwa ni fisadi namba moja duniani! Lakini baada ya Lowasa kuinunua chadema na kuwa mgombea urais , ni Lisu huyohuyo tena alizunguka nchi nzima akiwaambia watu kuwa Lowasa siyo fisadi na anafaa kuwa rais wa Tanzania!

Tabia mbaya hii Tundu Lisu aneendelea nayo hata baada ya kupigwa risasi zaidi ya 38, kwanza aliwaahidi wa Tanzania kwamba akipona tu atarudi nyumbani mpaka leo hajafanya hivyo maana yake alisema uongo. Pili ndani ya mwezi huu wa toba Tundu Lisu amelifurumshia uongo na uzushi bunge kwamba hajalipwa madai yake huku akijua si kweli!

Jana Spika Ndugai ameonyesha hadharani nyaraka zote zinazoonyesha Tundu Lisu amelipwa zaidi ya milioni 500 na bunge! ,tena amelipwa hela zingine za kutembelea wapiga kura wakati hajawahi kufanya hivyo! Hapo bado hujaweka mamilioni mengine aliyochangiwa na wana chadema.!

Tunakuambia tu Lisu huku kudeka na kulialia siyo kwa hali ya kawaida huenda una tatizo la malezi mahali na tunakuonya pia ipo siku wanyonge watataka kurudishiwa hela zao ulizolipwa bila kuzifanyia kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usipate tabu, hii hapa
Hiyo bado haina ushaidi kuwa imekwapuliwa! Nilichotaka kujua ni gharama halisi za hayo matangazo vs kilichotumika, maana inaweza ikawa jamaa kweli waliitumia yote kwenye matangazo hayo ya kutangaza vivutio vyetu kwa faida ya taifa letu!

Hiyo taarifa imeweka queries, wisara husika itatuletea uchambuzi wa uhalisia! Kama mleta maada unao huo uchambuzi tuwekee hapa, vinginevyo huu nao ni uzushi tu!
 
Mkuu tatizo linakuja why uanzishe nyingine wakati ipo Tanzania safaris na inatosha sana, na serikali kila siku inatamba kwamba inabana matumizi. Kumbe badala yake inatengeneza wapiga dili kubwa.
Hiyo bado haina ushaidi kuwa imekwapuliwa! Nilichotaka kujua ni gharama halisi za hayo matangazo vs kilichotumika, maana inaweza ikawa jamaa kweli waliitumia yote kwenye matangazo hayo ya kutangaza vivutio vyetu kwa faida ya taifa letu! Hiyo taarifa imeweka queries, wisara husika itatuletea uchambuzi wa uhalisia! Kama mleta maada unao huo uchambuzi tuwekee hapa, vinginevyo huu nao ni uzushi tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tatizo linakuja why uanzishe nyingine wakati ipo Tanzania safaris na inatosha sana, na serikali kila siku inatamba kwamba inabana matumizi. Kumbe badala yake inatengeneza wapiga dili kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu za uanzishwaji wa hayo yote mimi sina detail ila nakumbuka kuna kipindi wabunge hasa wa upinzani walimkaba koo na kuishutumu WMU kuwa hakuna ubunifu, wajifunze kenya! Nafikiri walianzisha hayo kama sehemu ya ubunifu wao mkuu!

Sasa ktk kuanzisha kama matumizi yali 'overshoot' na kama wanamaelezo yanayojitosheleza nafikiri wataleta! Ndio maana nikasema, tupate mnyumbuisho wa matumizi ya hizi bilions vs uhalisia kabla hatujarukia hitimisho!
 
Sasa hapa Said Bagaile atatoka vipi ?Mganga wake alishindwa kuficha hii. Halafu watu wenye vimbelembele ndo hatari sana. Jamaa mwizi wa wezi. Ngonja nikanywe juice yangu ya Limao ili kudumisha immunity yangu niishi muda mrefu na kuona hii issue Ngosha atapita nayo ama la.
 
Hiyo bado haina ushaidi kuwa imekwapuliwa! Nilichotaka kujua ni gharama halisi za hayo matangazo vs kilichotumika, maana inaweza ikawa jamaa kweli waliitumia yote kwenye matangazo hayo ya kutangaza vivutio vyetu kwa faida ya taifa letu! Hiyo taarifa imeweka queries, wisara husika itatuletea uchambuzi wa uhalisia! Kama mleta maada unao huo uchambuzi tuwekee hapa, vinginevyo huu nao ni uzushi tu!
Unabishana na Report ya CAG? Kama una uwezo wa kubishana na Report ya CAG mimi nitaweza kweli kukujibu? Sitaweza Mkuu
 
Back
Top Bottom