Wizara ya Maliasili na Utalii yatuhumiwa kutumia Tsh. 2.5B kuanzisha chaneli ya Urithi Festival nje ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge

Wizara ya Maliasili na Utalii yatuhumiwa kutumia Tsh. 2.5B kuanzisha chaneli ya Urithi Festival nje ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge

HAYAA SASA NASUBIRIA SALAM ZA MWISHO ZA MKULU AKIEIPOKEA ANASEMAJE...

BIL 2.5 ZIMETUMIKA KUANZISHA TV ...JE HIO TV ILIPITISHWA NA BUNGE ...NGOJ TUSUBIRIE

Screenshot_20200407-233430.png
Screenshot_20200407-233405.png
Screenshot_20200407-233314.png
Screenshot_20200407-233304.png


===
RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania (CAG) imebaini matumizi ya Sh2.58 bilioni yaliyofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii nje ya bajeti na kabla ya kupitishwa na Bunge.

Hayo yamebainishwa katika ripoti kuu ya mwaka kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha za serikali kuu kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2019. Fedha hizo zimetumika kufanikisha kampeni ya Urithi Festival Celebration and Channel maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kinyume na taratibu.

“Nilipitia matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kubaini kiasi cha Sh 2.58 bilioni kimetumika kuanzisha chaneli ya Televisioni “Urithi Festival” ili kutangaza vivutio vya utalii,” imeeleza ripoti hiyo.

Imeeleza kuwa katika kutambua chanzo ya kugharamia matumizi hayo, hayakuwa na kifungu cha bajeti kama ilivyopitishwa na Bunge.

Imeeleza kuwa fedha hizo zilitolewa katika vifungu vingine vya matumizi ya wizara na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo ambazo ni Tanapa, NCAA, Tawa na TFSA.

“Nilijulishwa kuwa bajeti ya Urithi Festival ilipitishwa na menejimenti ya Wizara katika vikao mbalimbali vilivyofanyika,” inaeleza taarifa hiyo.

Akinukuu Ripoti ya CAG, Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Catherine Ruge, amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania ilitumia TZS 2.5 bilioni kuanzisha Channel ya runinga-Urithi Festival nje ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Naye Waziri Maliasili, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amesema; “Mimi siyo mwizi, siibagi, na sichukuagi rushwa. Kwenye maeneo ambayo mtu yeyote anayenitafuta kuniharibia hadhi na heshima yangu kama kiongozi msafi huwa mara zote anakwama ni hapo kwenye tamaa ya pesa ya umma. Huwa sina. Hivyo hii vita ni rahisi sana kwangu.

“Ukitaka kunichafua mimi, tafuta kasoro zangu zingine, lakini hautonipata kwenye rushwa, uonevu, dhulma, wizi, matumizi mabaya ya ofisi, uzembe, uvivu wala ujinga/upuuzi. Nitafute kwingine. Nitatoa ufafanuzi juu ya utaratibu baada ya masaa matatu,” amesema Waziri Maliasili, Dkt. Hamis Kigwangalla.
 
kwa watu wenye akili timamu kama mimi, hatuwezi kufuatilia hii sinema kwa sababu hicho kituo hakikuanzishwa na kigwangala na wala sio yeye aliyetoa wazo, huu ulikua ni mpango wa serikali kabisa kama mtakumbuka so haiingii akilini uwe rais wa nchi alafu kianzishwe kituo cha tv hujui pesa imetoka wapi au zitumike bl 2 alafu ukae zaidi ya miaka 2 hujui mpaka CAG aje akwambie
 
Huu uongozi haufai kabisa tuitafute October.
 
Mwache ndugu yetu amalizie ujenzi wa Hospitali yake pale PUGE ,huyu ni chaguo la Mungu namba 2,bahati mbaya nilipita usiku ningetupia kapicha.
 
Huyu jamaa ntamkumbuka kwa imani za kiahirikina pamoja na kutengeneza mbuga mpya ya wanyama rip
 
Back
Top Bottom