Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Tuna dhahabuAngola wana mafuta. Sisi tunategemea tozo tu. Mkono mtupu haulambwi au unataka tuongeze tozo na kodi ili tuweze kujenga barabara za aina hizo unazotamani? Serikali ikiongeza tozo kidogo tu nyie ndoo wa kwanza kupiga kelele sana na kuitukana serikali.
Tuna almasi
Tuna Tanzanite
Tuna gesi
Tuna misitu
Tuna maji
Tuna madini mengine ya kila aina
Tuna mbuga za wanyama
Tuna Uranium
Tuna karibu kila kitu
Shida yetu wala siyo ukosefu wa raslimali. Shida yetu ni ukosefu wa viongozi wazalendo na wenye maono. Na adui yetu mkubwa ni ufisadi.
Hata kama tungepewa mafuta yote yaliyopo hapa duniani kwa viongozi hawa tulionao hakuna kitakachotokea bali pesa zote za mafuta zitaishia katika akaunti za siri huko Uswizi/Uarabuni; na kwenye miradi binafsi ya ndugu na marafiki.