Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi: Mabehewa yaliyokuja siyo ya SGR ni ya MGR

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi: Mabehewa yaliyokuja siyo ya SGR ni ya MGR

Ufisadi tayari. Kulikuwa na haja gani ya kununua mabehewa mapya ya MGR, wakati tupo kwenye transformation ya kwenda SGR?
Halafu kuna mabehewa mapya yanayotengeneza treni ya Deluxe. Hapa pana uhuni unafanyika.
 
Ufisadi tayari. Kulikuwa na haja gani ya kununua mabehewa mapya ya MGR, wakati tupo kwenye transformation ya kwenda SGR?
Hapo sasa ndo inashangza c bora wangenuna ya SGR hata ma 5 tu basi kuliko kuleta mibeheea ya MGR...
 
MGR ni nini tena? Kuna hu msemo "If you can't convince them confuse them"......mtupe tofauti ya SGR na MGR tafadhari

..MGR ni meter gauge rail. Hicho ndicho kiwango cha reli yetu ya kati.

..SGR ni standard gauge rail. Ni kiwango cha reli mpya inayoendelea kujengwa.

..CGR ni cape gauge rail. Ni kiwango cha reli ya Tazara.
 
Kelele zilizopigwa ndio zimewafanya wakabadilisha msimamo, wasitudanganye, zile behewa zilikuwa kwa ajili ya reli ya SGR.

Bora wafanye hivyo, kwasababu pale palionekana kuna upigaji wa wazi, na wahusika ilikuwa lazima wawajibishwe kisheria, sasa ngoja tuone hayo mabehewa mengine kama yataendana na ubora unaotegemewa.
Hilo nalo ni neno mkuu, haiwezekani unajenga majengo kwa ajili ya kuanzisha skuli, unakamilisha kila kitu na kuanza kuutangazia umma usajili wa awali mara paaap unaambia umma haya majengo ni kwa ajili ya mifugo (kuku)
 
Ufisadi tayari. Kulikuwa na haja gani ya kununua mabehewa mapya ya MGR, wakati tupo kwenye transformation ya kwenda SGR?
Hilo la kwanza, la pili ni swali: inamaana viongozi wote wakuu wa Serikali kuanzia Rais, Waziri mkuu pamoja na Mkurugenzi Kadogosa waliamuaje kuudanganya umma kuwa mabehewa hayo ni ya Sgr au wote hawa hawakuwa na taarifa sahihi kuyahusu mabehewa hayo?

Je yaweza kuwa sahihi viongozi kudanganya na likitokea jambo kama hilo lenye kuleta mkamganyiko na mtafaruku mkubwa kiasi hiki, linaachwa tu lipite hivi hivi au kuna mtu wa kulaumiwa hapo?
 
Walinunua Seti mbili ya MGR na SGR, hopefully hawakutaka Watanzania wajue

Nadhani huu ni part ya huo mchongo..

Tanzania ikipata mtu Kama Magufuli, Kesi ya Kwanza ya Kadogosa, Mbarawa na Manaibu wake ni hii hapa, yaani huwezi ukafanya kosa kubwa usiache ushahidi
Hapana, hayo ya MGR itakuwa wametupa bashishi (zawadi). Tatizo wametupa by surprise, Kadogosa na Mbarawa wakafikiria ni yale ya SGR waliyoagiza na kuanzakufanya sarakasi kuyatetea. Wakorea noma sana. Wakatuletea na mkopo wa trillion tatu yenye grace period ya miaka 15. Yaani ni kama wametukopesha tu hayo mabehewa ya SGR.
 
Behewa ni 22 zilizokuja kwa reli ya Kati MGR na si miongoni mwa behewa za @SGR_tz. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Asieamini kuwa kuna uhuni CCM na serikali huyo atakuwa na matatizo ya akili.

Sasa Mbawala, Msigwa na Kadogosa wote hawa kujua kuwa hayo siyo mabehewa ya SGR bali ni MGR!? Kwa nini waendelee kuaminiwa tena baada ya kuwadaganya Watanzania!? Na sababu za wao kufanya hivyo ni nini!?

Kama Maza yuko serious walau tu kwa 10 %, hawa watu wanatakiwa kutimuliwa kazi kwa uongo wao.
 
Tunachezewa sana.

Ukishaona maelezo yanakuwa mengi sana, jua kuna tatizo mahali
 
Hivi Mama Samia anaona haya majibu yanayobadilishwa kila siku kweli Au ndio anashauriana na watendaji wake kwamba tafuteni jinsi ya kuwajibu hawa wananchi
 
Mbona sasa kila sekta inaonekana kuchanganyikiwa akili? Kule nishati sarakasi na huku uchukuzi nako sarakasi. Kwanini wabunge wetu walipoanza kufanya sarakasi huko bungeni, mama spika aliwapiga marufuku? Kweli iko haja ya raisi kufanya mabadiliko.

Serikali sasa haiko chini ya washamba kama iliyopita. Sasa iko chini ya watoto wa mjini. Waerevu. Kwa hiyo mtulie tu sindano iwaingie.
Kisima CAPO DELGADO Semahengere
 
Hio nauli, Dsm to bahi 65,000, Sijui Dar to Mza itakua TSH ngapi!? Ni kama hayo mabehewa yapo Kwa ajili ya tabaka Fulani hivi la watu.
 
Dar -Dom 70k?
Nisaidieni Dar- Dom kwa basi ni bei gani, na muda wa safari saa ngapi kulinganisha na treni?
Kama ndiyo ile treni inayotrend itatumika, basi ni afadhali mara 1000 upande basi maana ni elfu 20-25 tuu na masaa kati ya 7-9.
 
Hilo la kwanza, la pili ni swali: inamaana viongozi wote wakuu wa Serikali kuanzia Rais, Waziri mkuu pamoja na Mkurugenzi Kadogosa waliamuaje kuudanganya umma kuwa mabehewa hayo ni ya Sgr au wote hawa hawakuwa na taarifa sahihi kuyahusu mabehewa hayo?

Je yaweza kuwa sahihi viongozi kudanganya na likitokea jambo kama hilo lenye kuleta mkamganyiko na mtafaruku mkubwa kiasi hiki, linaachwa tu lipite hivi hivi au kuna mtu wa kulaumiwa hapo?
Hii nchi ilishawai kuokota hadi vichwa vya tren bandarin na hakina kilichotokea kwahiyo mambo mengine usishangae.Tunaposema hii nchi watu imewashinda ndo kama hivyo sasa.Mauza uza kila kona.
 
Back
Top Bottom