Wizara ya Vijana ni changa la macho kwa vijana

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,449
Reaction score
10,310
Moja ya wizara za kwanza kabisa kuundwa mara baada ya Tanganyika kupata uhuru ni ya vijana, iiitwa "wizara ya utamaduni wa taifa na vijana" (ministry of national culture and youth).

Waziri wa wizara hiyo aliitwa Leo Nang'wanda Sijaona akitokea huko huko kwa akina Nanauka. Lakini Leo Nang'wanda Sijaona alipewa wizara hii akiwa kijana kweli kweli, miaka 35, wakati Nanauka ni mzee mwenye miaka 42.
*Kumbukeni: Kwa mujibu wa sera ya vijana ya taifa, kijana ni mtu mwenye umri wa miaka 18 - 35.

Kuanzia wakati huo vijana wakawa modomoni mwa wanasiasa mpk leo hii, lkn hakuna kilichobadilika. Sana sana tumefanikiwa kupata misemo tu. Mfano, vijana ni viongozi wa kesho.

Imekuwa ni tabia ya wanasiasa, kila panapoinuka kelele au changamoto za kundi fulani wanaunda wizara ili kulituliza kundi hilo. Nitatoa mifano michache:-
1. Baada vugu vugu la wanawake kudai usawa (50/50) kuenea sana hapa nchini kufuatia mkutano wa Beijing wa 1995, serikali ikaunda wizara ya wanawake. Je, matatizo ya wanawake yameisha nchi hii??
2. Baada ya migogoro ya wakulima na wafugaji kutamalaki sana na kupelekea awamu ya nne kuanza kuwahamisha wafugaji, wizara ya kilimo ikabadiliahwa jina na kuitwa "wizara ya kilimo na mifugo". Ili mradi tu wafugaji wajione wametambuliwa. Je, matatizo ya wafugaji yameisha nchi hii?
3. Mauaji ya albino yalipokithiri, walemavu wakatambuliwa kwa kuongezwa kwenye wizara ya wanawake. Ikaitwa wizara ya jinsia, wanawake na watu wenye ulemavu. Mxiuuuu!!! Imesaidia nini??
4. Sasa hata uundwaji wa vizra ya vijana umekuja ili kuwatuliza Gen Z. Eti vijana wameenguliwa kutoka huko walikokuwa, na kupewa wizara ya peke yao. So what??

Kwani kuwa na wizara ndiyo kunatatua matatizo ya kundi husika? Mbona kuna:-
1. Wizara ya kilimo......wakulima wanalia kila siku.
2. Wizara ya maji..... Maji mpk leo tabu.
3. Wizara ya afya..... Mpk kesho watu wanataabika kwenye matibabu.
4. Wizara ya ajira.......ajira tabu mpk kesho .
5. Wizara ya viwanda na biashara......matatizo ya biashara na viwanda yameisha?

Waziri wa vijana anakuja na mikakati ya kizee inayoakisi uduni wa kifikra unaoendana na umri wake wa miaka 42. Ktk zama hizi za AI analeta swaga za kujenga makampuni 100,000 nchi nzima eti ataaajiri vijana wengi. Mxiuuu!
Hapa sijui alilenga kutatua nini? Mimi simuelewi kabisaaaaa.

Mwambieni huyu waziri kuwa matatizo ya vijana ni ya kimfumo hayatatuliwi in isolation. Serikali itengenezwe fursa, halafu vijana wachangamkie fursa hizo.
Kwani serikali imejenga kuchangia nini katika haya:-
1. Umachinga.
2. Saloon.
3. Bodaboda.
4. Uwakala wa benki na simu???.
Lkn mbona vijana wengi wamejiajiri katika maeneo haya??

Vijana watakuja wenyewe tu kwenye fursa zitakazokuwa zimeandaliwa kama serikali hii haramu itaweza kuzianzisha. Kilimo, kwa mfano, kikiwekewa mazingira mazuri hasa ya upatikanaji wa mbolea na MASOKO, kinaweza kuwaojiri vijana wote nchi hii.

Msinichoshe. Naishia hapa.
 
Kupitia hiyo wizara mchongo ndipo linapozaliwa taifa analolitamani Habibu Mchange na washirika wake kwenye ufisadi na kulitafuna taifa hili kwa manufaa yao na familia zao
 
Joel Nanauka sio mtendaji ni muongeaji(motivational speaker) aliyekuwa akipiga vijana hela kwa kuwauzia vitabu na seminar akitumia kigezo cha kuwa TO kama qualification.
 
Back
Top Bottom