Wizara zenye wizi na ubadhilifu zapaswa kufanya tathmini (Risk Assessment) za kila mara, vitendo hivyo ni sehemu ya hujuma kwa taifa

Wizara zenye wizi na ubadhilifu zapaswa kufanya tathmini (Risk Assessment) za kila mara, vitendo hivyo ni sehemu ya hujuma kwa taifa

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Wizara mbalimbali zimekuwa zikikabiliwa na matatizo kama ubadhilifu wa fedha, wizi wa kimtandao na wa kughushi na hata matishio ya kusambazwa kwa taharuki kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Kumekuwa na taarifa za vitendo vya udanganyifu katika Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo mijini, wizi wa madawa katika mahospitali yalo chini ya Wizara ya Afya na utoaji wa taarifa za uzushi katika mitandao ya kijamii na wizi kwenye hamlashauri za manispaa au wilaya kadhaa hapa nchini.

Lakini ukiangalia sana utaona kwamba Mawaziri husika hutoa matamko kwamba watu walohusika na majanga hayo wanapaswa kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Pia taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU imekuwa wima katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi sasa ambapo mabilioni ya fedha za walipa kodi yameibwa au kupotea katika mazingira ya ubadhilifu, wizi wa kughushi na matumizi mabaya.

Kwa mfano wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo mijini imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya watumishi wasio waaminifu ambao wanajishughulisha na uuzaji wa viwanja katika maeneo mbalimbali nchini. Pia baadhi ya watumishi wa wizara hiyo wamekuwa wakifanya udanganyifu katika mifumo ya kanzidata ya wizara hiyo kwenye kuingiza taarifa zisizo za kweli.

Wizara ya Afya nayo imekuwa katika wakati mgumu ambapo taasisi yake ya ugavi dawa ya MSD imekuwa ikiingiliwa katika mfumo wake wa ambapo wizi wa madawa na vifaa vya kitabibu umekithiri ambapo juzijuzi madawa yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.

Katika taasisi ya MOI watumishi wapatao 23 ambao ni wafamasia walitumia mfumo wa kutunza taarifa kumbukumbu za madawa wa MEDPRO kuingiza taarifa za uongo kwa kuongeza idadi ya dawa kwenye cheti cha mgonjwa na pia kuongeza kiasi kikubwa cha gharama za dawa katika fomu ya daktari.

Halikadhalika wizi na matumizi mabaya ya fedha umekithiri katika wizaya ya TAMISEMI ambapo halmashauri kadhaa zimekumbwa na wizi na matumizi mabaya ya fedha. Halmashauri ya Biharamuro ilikumbwa na wizi wa shilingi milioni 400 ulofanywa na watumishi kumi na mmoja. Pia wilayani Makete watumishi tisa walifikishwa mahakamani kwa kuiba fedha za kodi milioni 39.

Wilayani Mbozi mkoani Songwe watumishi kadhaa walifikishwa mahakamani kwa wizi wa fedha za kodi kupoitia mfumo wa kielektroniki wa POS kiasi cha shilingi milioni 11.

Ntazungumzia kwa upana wizara ya teknolojia ambayo inaisimamia TCRA katika mikala ingine maalum kwa ajili hiyo.

Sasa basi tatizo ni nini kwa haya yote?

Unapata jibu kwamba wizara husika hazinayo tabia ya kufanya tathmini (Risk Assessment) katika wizara zao khasa katika maeneo husika.

Au inawezekana pia kwamba tathmini imefanywa lakini kuna mahali pana kasoro kwa kuzingatia kuwa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani inapenda kufuatilia kila maagizo yake ambayo hutolewa.

Ni dhahiri kwamba TAKUKURU inazo taarifa zote tangu ianze kufanya kazi zake kikamilifu chini ya serikali ya awamu ya tano. Halikadhalika wizara ya ardhi nyumba, makazi na maendeleo mijini nayo imefanaya tathimini na pia hata wizara ya TAMISEMI nayo imefanya tathmini kabkla ya kuanza zoezi la kuorodhesha majengo na nyumba zote nchi nzima.

Tuangalie tathmini au Risk Assessment ni nini.

Kabla hujaanza kufikiria kufanya tathmini ni lazima uwe na mambo makuu matatu ya kuzingatia.

Kwanza uwe na hatari au kw akiingereza "risk" ambayo ni hali inaweza kusababisha hasara au hatari. Pili kuwepo kitu kinachoweza kusababisha hatari kwa kiingereza "Hazard" na mwisho kuwepo udhaifu au kwa kiingereza "Vulnerability" ambayo huitwa pia "weakness".

Nikitoa mfano ni kwamba mtu anaweza kuwa mdhaifu au ana udhaifu katika kukataa ushiwishi wa pombe na akanywa kisha kwa kutojali udhaifu wake akaamua kuendesha gari ambalo ni hatari (risk) kwa maana ya kitu kitakachosababisha ajali (hazard) na mwishi wake huwa ni majanga au kukamatwa na polisi ukiendesha gari ukiwa umelewa.

Lakini ukiomba mkopo benki CRDB wao watatumia tathmini iliyomo katika mfumo wa computer ili iwaeleze tathmini ya uloyaeleza katika fomu ya maombi ya mkopo. Hivyo kama una historia ya kutolipa mkopo kwa wakti, huna kazi ya kueleweka au permanent job wewe ni hatari kwa benki kwa maana ya (risk) na sio (hazard) hivyo neno neno risk limejigawa kwa maana ya "hali inayosababisha" na "kitu kinachosababisha" hasara, majanga, matukio mabaya kama ugaidi, kuharibiwa taswira kama nchi na majanga mengine mengi tu.

Halafu kuna mali au Assets yaani taasisi, shirika, kampuni, watu, mashine na vifaa mbalimbali na mali zingine zinazohamisha na zisizohamishika.

Ili uweze kufanya tathmini ni lazima uzingatie misingi mikuu mitano ambayo bila hiyo huwezi kupata majibu halisi ya tathmini yako.

Kugundua na kuainisha au "identification and analysing" ni lazima utambue matukio yaliyomo katika sehemu tatu nilozieleza hapo juu yaani hatari, udhaifu na udhoofu ambayo yanaweza kusababisha adhari kwa mali au asset uliyo nayo.

Pili, ni lazima uchambue udhaifu na kuupanga kulingana na uzito wake. hapa ndipo utaona ni yapi yanaweza kuleta athari au majanga zaidi na kwa kiasi gani.

Tatu, kufanyia tathmini madhaifu yote uloyagundua na kutengeneza taratibu za kudhibiti au "control measures". hapa ndipo unapoweza kulinda mali zako au assets zote kwa kuiondoa au kuidhibiti hatari.

Nne, kuweka kumbukumbu ya yale yote uloyagundua na kuanza kuyashughulikia. Hii ya kuweka kumbukumbu huitwa "risk register". Risk register hujazwa matukio na matishio yote na huwa ni kielelezo kizuri kwa mafunzo au hadidu za rejea.

Tano, ni kuipitia upya tathmini na kurekebisha au kuongeza zaidi madhaifu mengine na matukio ambayo yanajitokeza upya.

Tathmini ni endelevu na hupaswa kufanywa kila mwaka ili kuweza kutambua matukio mapya yanayoweza kusababisha athari.

Kwa mfano wizara ya afya inaweza kufanya tathmini ya kinachoendelea kuhusiana na vitendo vya wizi katika mahospitali yake nchini.

Inaonyesha dhahiri kwamba wizi na ubadhilifu hufanywa na wafamasia, wakishirikiana na madaktari na watumishi wengine waso waaminifu.

Baada ya kugundua matukio na hali zinazopolekea vitendo hivyo wizara inaweza kuweka udhibiti kwa kuhakikisha inaajiri maofisa watendaji wa hospitali nchi nzima.

Hivyo kila hospitali itakuwa yaongozwa na huu utawala ambao ni "Corporate" na uko juu ukishughulikia utawala, fedha, ugavi, usimamizi wa vyanzo vya mapato na rasilimali watu wakiwemo madaktari.

Kukiwepo ofisi ya mtendaji mkuu kutaleta nidhamu ya kazi na hawa wanaweza kuajiri watalaam wa kufanya tathmini ili kupata picha halisi ya taasisi zao kifedha na kiafya kuhusu hujuma dhidi yake.

Hivyo basi, napenda kutoa ushauri kwa serikali kupitia wizara zake kutambua kufanya tathmini ambazo zitasaidia kudhibiti wizi na ubadhilifu unoendelea kwa sasa.

Azimio la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kila Mtanzania anajikomboa kiuchumi na kuona maendeleo ya kweli.

Hizi kesi ya wizi na ubadhilifu hata katika mashine za kielekroniki ni sehemu za hujuma ambazo serikali inapaswa kuzifanyia tathmini.

Richard JF.
 
Umezunguka weweeeeeeeeeee lakini umeogopa kugusa mapapa wa ufisadi, unataja vidagaa unaacha ujenzi, maji, ununuzi wa ndege, umeme mkubwa, sijui SGR n.k kweli? huko kote umewahi kuona CAG anakagua na kutoa report?
 
Tiririka tofauti yake
RA nimeeleza hapo juu na CAG ni financial MOT ya fedha za serikali na idara zake.

CAG huwa hagusii RA na ni fani mbili tofauti.
 
Umezungukaaaaa weeee umeshindwa kuitaja wizara ya ulinzi,mambo ya ndani na ofisi ya Rais hizi ndizo wizara zenye ubadhilifu mkubwa na hazifanyiwi ukaguzi wa uhakika.
 
Umezungukaaaaa weeee umeshindwa kuitaja wizara ya ulinzi,mambo ya ndani na ofisi ya Rais hizi ndizo wizara zenye ubadhilifu mkubwa na hazifanyiwi ukaguzi wa uhakika.
Lengo la mada ni kuelezea umuhimu wa RA na si kuchambua wizara zote na yote usemayo.

Ndo maana nimetumia maneno kama "kwa mfano" na kadhalika.
 
Mtaongea sana ila siku nitaamini ni pale viongozi wote wa juu watakapoorodhesha mali zao hadharani na pia ikaidhinishwa ni kweli walizipata kihalali tofauti na hapo nyie kaeni kusikiliza hekaya miaka nenda rudi.
 
Bandiko zuri Richard, mimi nauliza ninini kitakuwa madhara ya watumishi wa umma kupewa mikataba ya muda mfupi? mfano mwaka 1-3. Matokeo chanya ndio yatadermine kurenew mkataba wa mhusika au kutokurenew, walau basi katika level fulani ya utumishi.
 
Bandiko zuri Richard, mimi nauliza ninini kitakuwa madhara ya watumishi wa umma kupewa mikataba ya muda mfupi? mfano mwaka 1-3. Matokeo chanya ndio yatadermine kurenew mkataba wa mhusika au kutokurenew, walau basi katika level fulani ya utumishi.
Kwa mshahara upi?makato Kama yote,mtumishi afisa Ana daraja la kwanza anapokea laki 3 mwisho wa mwezi baada ya makato si aibu hii?hebu axheni unaa huo,hata ufanisi atatoa wapi huyo mtumishi?
 
Kwa mshahara upi?makato Kama yote,mtumishi afisa Ana daraja la kwanza anapokea laki 3 mwisho wa mwezi baada ya makato si aibu hii?hebu axheni unaa huo,hata ufanisi atatoa wapi huyo mtumishi?
Walau katika level fulani ya utumishi, ama haujaona hilo nililoandika. Mf. managerial level.
 
Nimependa kweli kichwa cha mada yako.

Natumaini uliyoandika humo ndani yanaendana vizuri nacho!

Kwa sasa naunga mkono hoja kama inavyoonyeshwa na kichwa cha habari.
 
Bandiko zuri Richard, mimi nauliza ninini kitakuwa madhara ya watumishi wa umma kupewa mikataba ya muda mfupi? mfano mwaka 1-3. Matokeo chanya ndio yatadermine kurenew mkataba wa mhusika au kutokurenew, walau basi katika level fulani ya utumishi.
Hilo litatokana na matokeo ya process ya kwanza yaani kwenye identification process.

Pale unaangalia watumishi, historia zao za nyuma, elimu zao, uwezo wao kupitia KPIs, mishahara yao kisha mikataba.

Baada ya hapo waingia hatua ya pili ya kutanabaisha na kuwaweka kwenye makundi kulingana na risks zao.

Hivyo kama ulikosea huko nyuma kumwajiri mtu kumbe ni analeta risk ya wizi kwa kutumia udhaifu (vulnerability) ya ukusefu wa usimamizi, basi warekebisha kwa kuweka measures.

Kwa mfano wizarani ardhi mtumishi aingiza taarifa za uongo kwenye mfumo wa computer kwamba hoteli iko kwenye eneo la 800 mita za mraba lakini kumbe eneo ni mita za mraba 1000 huo ni udanganyifu na wakosesha serikali mapato.

Hivyo nikirudi kwenye suali lako ni kweli kabisa kwamba waweza kuweka kiwango cha mshahara na kukipandika kutokana na perfomance ya mwajiriwa.

Na pia mkataba wa kazi wategemea ukubwa wa kampuni au taasisi au wizara na nafikiri wizarani mtu akiajiriwa inakuwa ndo mpaka anastaafu na hapo ndipo udhibiti watakiwa kwasababu mtu anakaa sehemu nyeti miaka nendarudi kumbe aishiri vitendo viovu vya rushwa na ubadhilifu.

Ila huko tunakokwenda kuna taasisi zitahitaji watu waajiriwe kwa mikataba maalum na itaangaliwa upya pindi itapokaribia kuisha.
 
Eeeenh, mkuu Richard, kwa mvuto wa 'Heading' ya mada yako, nimeshindwa kuendelea na mengine humu JF, kabla sijachungulia humo ndani umeandika nini.
Sasa mara nyingi huwa mvivu wa kusoma 'essays' hizi ndefu - basi nikaona nianze na yaliyochangiwa na wengine kwenye mada.

Bado nikawa na duku duku la kutaka kujua umeandika nini, lakini bado sikuwa na ujasiri wa kuanzia mwanzo wa mada.

Hapo ndipo nilipoamua nianzie mwishoni. Nikasoma hadi katikati ya 'essay' yako.

Umeeleza vizuri, ila umeifanya kuwa kama "home work" hivi.

Sikiliza mkuu wangu: haya yote ni mazuri, lakini kuna haja kweli ya kwenda kuvumbua gurudumu ambalo lilishavumbuliwa siku nyingi?

Nenda kwenye Pharmacy yoyote kubwa hapa nchini inayoendeshwa vizuri. Utajua kwamba ma-pharmacist hapo hawana nafasi yoyote ya kudokoa chochote kwa kushirikiana na yeyote.

Na siyo hivyo huko tu - nenda kwenye hospitali hizi kubwa kubwa binafsi, kama pale Shree Hindu Mandal; utakuta matatizo kama yaliyoko huko kwenye mahospitali ya serikali?

Hii ni enzi ya Tekohama mkuu, pendekeza serikali iwekeze nguvu zake huko kupata wataalam wazuri na nyenzo za kufanyia kazi kuondoa hizi takataka zinazopoteza mali za taifa.

Kuongeza 'layer' nyingine ya walaji huko mawizarani haitasaidia kitu. Historia inaonyesha hivyo. Hebu angalia hao sijui viongozi wanakwenda kuandikisha mali zao, sijui kwenye ofisi gani - imesaidia nini?

Wazo lako ni zuri, lakini umeliweka ki'textbook' zaidi kuliko uhalisia ulivyo.

Sasa kama nimekosa mengi mazuri zaidi uliyoandika katika hiyo sehemu ya mwanzo, basi utanisamehe kwa huu uvivu wangu wa kusoma maandiko marefu refu sana.
 
Ukisema taasisi ijifanyie tahmini huko itakua ni kujidanganya wenyewe ,

Nadhani labda unazungumzia CAG kuongezewa meno na bajeti katika utendaji wake.

Ripoti itayokuwa unbiased lazima iwe ni ile toka nje ya taasisi husika.
 
Mkuu, ni kweli TEHAMA ipo na wataalam wapo wamefoma fani kama IT.

Ila kwa upande wetu sisi (kwenye hospitali zetu) tunahitaji mabadiliko yatakayotokana na mpango niloulezea wa kufanya RA.

Bado yaonyesha wazi kuwa madaktari na wafamasia kuwa kutumia mfano wa MOI wanashirikiana kuiba dawa ili kuziuza pembeni.

Na mfano mwingine kule Mara (kama sikoei) madawa yalokwisha muda wake yaliingizwa kwenye mfumo wa ugavi wa MSD.

Au iweje mtumishi wa halmashauri atumie mfuma wa POS achepue fedha zisiiingie kwenye mfumo wa halmashauri bali uende kwenye akaunti fulani?

Hiyo yaonyesha wazi tunao watalaam ambao endapo wizara zitawabaini (kupitia identification process) tunaweza kuwa na picha halisi na nini kinaendelea.

Hivyo kama wanaelewa ninachomaanisha wataweza angalau kubaini wizi huu wafanywa na watu wa aina ipi, je ni syndicate? au kuna mfumo mzima wa wizi uliopo nchi nzima?

Ndo maana nasisitiza na kushauri hizi RA ziwe real deal kama zipo na zisiwekwe makabatini endapo zinafanywa.
 
Back
Top Bottom