Wizi kwenye Mataa ya barabarani

Mi mbona sikutanagi nao wa hivyo? Tena na kamwili kangu kalivyo kadogo naamini kuna siku atajaa, nitapiga Kombat moja akipona na wizi ataacha
 
Wewe kweli,ni jasiri na mkakamavu.
 
Daah, mi ilinitokea mchana kweupe pale mataa ya Fire, sikufunga kioo changu cha mbele, teja alinitolea wembe wenye kutu akawa anaulengesha shingoni, akala 70,000/= yangu kiulaini kabisa, daaah, hii nchii hiii
Ungepandisha kioo,kikambana mkono,angeomba samahani,yeye mwenyewe.
 
Wiki ijayo nakuja huko dar na athlet crown langu nikifika hapo sijui mataa gani kioo kitakuwa wazi nisipomkuta ntazunguka ntarudi tena halafu aje na wembe wake aone .kibaka mkubwa ahangaishe wanaume .
 
Kuna tena mmoja mwenye kipara pale ubungo mataa kuna siku nimeshusha kioo akaniwekea sindano nilimkunguta na rungu la uso pwaaaa akaanguka nikakanyaga mafuta nikasepa
 
Yeah, kila nikichomoa hatosheki, anazidi kusogeza wembe shingoni, ila leo nimenunua sime la kimasai natembea nalo pembeni ya kiti, ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Duh๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ bora hilo sime tu akikusogezea huo wake wewe unamsogezea sime atajuta๐Ÿ˜‚
 
Ha ha ha!!! Mkuu wewe hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ